Tuesday, January 4, 2011

WAZIRI DK. CHAMI KUTEMBELEA INDIA KUHAMASISHA UWEKEZAJI

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari kuzungumzia malengo ya ziara yake ya siku saba nchini India.

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, ameondoka
nchini kuelekea nchini India kwa ziara ya siku saba  ili kuhudhuria
mkutano wenye  lengo la kuhamasisha Biashara na Uwekezaji baina
 ya Tanzania na India.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka, Waziri Chami
amesema, nia ya serikali ni kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati
ya Tanzania na nchi rafiki pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji
zilizopo nchini.
Amesema akiwa nchini India, atazungumza na
wafanyabiashara na taasisi mbali mbali za kibishara nchini humo ili
ziweze kuja Tanzania kujionea fursa zilizopo na kuwekeza, hususan
 katika mamlaka ya EPZA.

Katika ziara hiyo iliyoandaliwa na taasisi ya Kamal Steel ya India
yenye miradi mbali mbali nchini Tanzania, Waziri Chami
ameongozana na Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya EPZA Dkt  A.
Meru.  Ziara hiyo itamwezesha Mh Waziri kuhudhuria Mkutano wa
 kimataifa  ujulikanao kama Global Commerece Chambers of
 Maharashtra utakaofanyika katika mji wa AURANGABAD katika
 Jimbo la MAHARASHTRA. Habari na Picha kwa hisani ya Ofisa Habari na Mawasiliano wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
 

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...