Thursday, June 7, 2018

WAZIRI MKUU AWATAKA WABUNGE KUDUMISHA MSHIKAMANO

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Wabunge, baada ya futari aliyowaandalia, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma Juni 5. 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasisitiza wabunge waendelee kudumisha  mshikamano ili Tanzania iendelee kuwa nchi tulivu na yenye amani.

Amesema mshikamano na upendo walionao wabunge hao ni vema wakauendeleza ili waweze kutekeleza shughuli zao za kuishauri Serikali.

Waziri Mkuu aliyasema hayo Juni 5, 2018 katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma wakati wa futari aliyowaandalia wabunge. Futari hiyo ilihudhuriwa na wabunge wa vyama vyote.

"Mshikamano na upendo huu tuliouonesha kuanzia mwanzo wa mkutano wa Bunge naomba tuudumishe ili tuweze kuishauri vizuri Serikali na tufikie malengo tuliyojiwekea,” alisema. 

Naye,Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye alitoa neno   la shukurani kwa niaba ya wabunge wote alimshukuru Waziri Mkuu kwa heshima aliyowapa.

"Tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, hii heshima uliyotupa ni kubwa, kualikwa na wewe si jambo dogo si kila mtu anaweza kupata nafasi hii," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mgogoni, Mheshimiwa Dkt. Suleiman Ally Yussuf ambaye alisoma dua alisema watu wanatakiwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliowapa.

“Kuna wenzetu tulioshirikiana nao kwenye mfungo wa Ramadhani mwaka uliopita lakini leo hatunao sababu wametangulia mbele ya haki, hivyo sisi tunatakiwa tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa uhai aliotupa,” alisisitiza.

Wednesday, June 6, 2018

Profesa Mbarawa akagua maendeleo ujenzi wa Tazara Fly Over

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kulia) wakikagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya juu (Tazara Fly Over) leo jijini Dar es Salaam. Ujenzi huo kwa sasa umekamilika kwa asilimia 88.

Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida akijadiliana jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya juu (Tazara Fly Over) leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida (kushoto) wakijadiliana jambo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya juu (Tazara Fly Over) leo jijini Dar es Salaam. 

Muonekano wa juu wa Barabara ya Nyerere eneo la Tazara (Tazara Fly Over) ambao kwa sasa ujenzi wake umekamilika kwas asilimia 88.


Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroards) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaharu Yoshida walipokagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya juu (Tazara Fly Over) leo jijini Dar es Salaam. 

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...