Thursday, January 20, 2011

Waziri Chami atembelea wajasiriamali

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, amewataka wajasiriamali nchini kufanya kazi zao kwa kuzingatia ubora na mahitaji ya soko la bidhaa husika ili kuleta tija.
Katika ziara yake ya siku moja jijini Dar es Salaam, Waziri Chami amesema Serikali inathamini mchango wa wajasiriamali katika uchumi wa nchi na kuwaahidi ushirikiano wa serikali kuwawezesha kwa kuwatafutia fursa za mafunzo, mitaji, masoko, malighafi na maeneo ya kufanyia kazi.
Aidha, amewaahidi kuwa, wizara yake kupitia SIDO itaandaa mafunzo na baadae ziara ya mafunzo nchini India ili kuwawezesha kujifunza kwa vitendo maendeleo makubwa ya kiteknolojia yaliyofikiwa nchini India.
Ziara hiyo ilianzia Mtaa wa Gerezani Kariakoo na kuendelea Mtaa wa Tabata Dampo na kumalizikia katika eneo la SIDO Vingunguti, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na wajasiriamali wanatengeneza bidhaa mbali mbali katika maeneo hayo na kubadilishana nao mawazo.
Dk. Chami amewataka wajasiriamali hao hasa wanaozalisha bidhaa za chuma kutotumia kisingizio cha ukosefu wa malighafi ya chuma  kama sababu ya kuharibu miundo mbinu ili kupata bidhaa hiyo.
Amesema Serikali iko mbioni kuanza uvunaji wa chuma ghafi katika migodi ya madini hayo iliyopo eneo la Liganga mkoani Iringa ili kuondoa kabisa tatizo la ukosefu wa chuma ghafi hapa nchini na kukomesha biashara haramu ya chuma chakavu inayovutia watu wasio waaminifu kufanya hujma ya kuharibu miundombinu.
Kwa upande wao wafanyabishara hao wameiomba serikali kutatua haraka tatizo la mgao wa Umeme na gharama kubwa za nishati hiyo zinazofanya shughulu zao kutokuwa na tija na kuiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia uwezekano wa kuwaondolea kodi kubwa wanazotozwa wajasiriamali hao.
Katika ziara hiyo, Dk. Chami aliongozona na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Dk. Adelhelm Meru, Mwakilishi wa Kamishna wa TRA, Allan Kiula na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Pius Wenga.
Habari hii na picha vimetumwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Nicodemas Mushi.


Dk. Cyril Chami wa nne kulia akitoa maelekezo katika moja ya ziara hiyo.


Waziri Chami (wa pili kulia) akiangalia moja ya mashine ya vyuma akiwa katika ziara yake.



Waziri Chami akiwa na baadhi ya maofisa alioongozana nao katika ziara yake.


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...