Tuesday, February 27, 2018

Shirika la TTCL lazinduwa huduma ya 'Fiber Connect Bundle'

Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba akizungumza katika uzinduzi huo.


SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION) limezinduwa rasmi huduma mpya inayojulikana kama 'Fiber Connect Bundle' inayokwenda pamoja na kauli mbiu ya "Rudi nyumbani, kumenoga" kuchagiza uzinduzi huo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Corporation, Bw. Waziri Kindamba alisema huduma hiyo ni mwendelezo wa ubunifu wa kampuni ya kizalendo katika kuwapatia Watanzania huduma za kipekee, nafuu na zenye ubora wa hali ya juu.

Bw. Kindamba alisema TTCL Corporation imedhamiria kuwafuata wateja nyumbani na kufanya mapinduzi makubwa ya kimawasiliano hasa ya mtandao wa intanenti yenye kasi ya juu.

Alisema kupitia huduma hiyo mpya ya Fiber Connect Bundle, wateja wao watapata huduma nne kwa pamoja zikiwa na unafuu mkubwa wa gharama na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na mitandao mingine ya simu.

Bw. Kindamba amefafanua huduma kwa kuanzia wanatarajia kuzifikia nyumba 500 katika maeneo ya Mikocheni na nyumba nyingine 500 katika eneo la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam pamoja na nyumba 200 eneo la Medeli mkoani Dodoma.

Aidha aliongeza kuwa baada ya hapo wataendelea na maeneo mengine kwani lengo lao ni kuhakikisha kila mahali katika nchi yetu kunakuwa na huduma za mawasiliano ya Shirika hilo hasa kwa kuzingatia wao ndio wanaousimamia mkongo wa Taifa wa mawasilano.

Kindamba amesema kupitia kifurushi cha Fiber Connect, mteja wao atanufaika na huduma mbalimbali ikiwamo ya  kupata intanenti yenye kasi isiyo na kikomo (Unlimited). Pia mteja atapata huduma ya simu za sauti kwa simu za mezani na simu card ambayo ataitumia kwenye simu yake ya mkononi na kupata huduma ya Intanenti sawa na simu ile anayopata katika simu ya mezani.

Ameongeza kuwa mteja wao pia atapata huduma za Wireless Service (WIFI) katika nyumba yake ambapo vifaa vyote vinavyotumia teknolojia ya intaneti vitaunganishwa  ili kutumia kutumia huduma hiyo.

Ametoa mfano kuwa huduma ambayo wameizundua mteja anaweza kuunganisha kwenye Smart Tv, Tablets na kompyuta mpakato.Pia mteja atapatiwa vifaa vyote bure na uhakika wa huduma za baada (After Sell Services) endapo itahitajika.

Amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora kwa ajili ya Watanzania ambao kimsingi shirika hilo ni mali yao na wanatakiwa kuunga mkono jitihada hizo.

“Tumeendelea kujipanga ili kufikia malengo yetu ambayo kimsingi ni kuwatumikia Watanzania kwa kiwango bora katika eneo la mawasiliano na kwa gharama nafuu,” amesema Bw. Kindamba.

Akizungumzia shirika hilo, Kindamba amesema, Februari moja mwaka 2018, Shirika la Mawasiliano Tanzania lilizaliwa kwa sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania Na. 12 mwaka 2017. Amesema kwa sasa shirika hilo limechukua sura  ya iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania( TTCL),  ambayo shughuli zake ziliisha Januari  31 mwaka 2018.

Amemshukuru Rais, Dk. John Magufuli kwa kuona umuhimu wa kuwa na Shirika madhubuti la mawasiliano la Taifa kwa maslahi mapana ya Taifa. Pia amemshukuru kwa kuendelea kuonesha imani kubwa kwa uongozi wao.

WAHUDUMIENI WANANCHI BILA YA UBAGUZI - MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya kikundi cha Teleza wakati alipo wasili, Wilayani Newala, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara  Februari 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati tofauti.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“Watumishi wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”

Waziri Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa wananchi.

Pia aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika kama zilivyoelekezwa.

Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi. 

Benki ya NMB yafungua tawi jipya Ruaha, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi 
la NMB Ruaha Mkoani Iringa. Tawi hili litakua ni tawi linafikisha idadi ya matawi 214 ya NMB nchi 
Nzima. Kushoto ni Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini, Badru Idd na Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakishuhudia tukio hili lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi 
la NMB Ruaha Mkoani Iringa. Tawi hili litakua ni tawi linafikisha idadi ya matawi 214 ya NMB nchi 
Nzima. Kushoto ni Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini, Badru Idd na Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakishuhudia tukio hili lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi 
la NMB Ruaha Mkoani Iringa. Tawi hili litakua ni tawi linafikisha idadi ya matawi 214 ya NMB nchi 
Nzima. Kushoto ni Meneja wa Kanda Nyanda za Juu Kusini, Badru Idd na Mkuu wa Kitengo cha wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) wakishuhudia tukio hili lililofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Iringa


BENKI ya NMB Tanzania imezindua tawi jipya Ruaha ambalo limeanzishwa kwa lengo la kusogeza
huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi wa mkoa wa Iringa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa
Kati wa NMB Bw. Abdulmajid Nsekela alisema,” Benki ya NMB imeendelea kuwa benki yenye
mtandao mpana zaidi wa matawi na ATM; tawi hili likiwa ni la 214 na ATM zaidi ya 800 nchi
nzima huku ikiwa na mawakala wanaotoa huduma za NMB zaidi ya 4000 nchi nzima huku ikijivunia wateja wake zaidi ya milioni 3.

“Mafanikio haya yasingeelezwa leo kama si kuaminiwa na wateja wetu ambao miongoni mwao ni
wana Ruaha na Iringa kwa ujumla kuwa benki wanayoipendelea zaidi na hivyo kuwa ni benki
yenye mafanikio makubwa zaidi nchini.”

Pamoja na ufunguzi wa tawi hilo, pia benki ya NMB ilitoa msaada wa milioni 5 ambazo zitaelekezwa katika sekta ya afya na elimu, ambapo Nsekela aliitaka serikali kusema ni maeneo gani ingependa pesa hiyo itumika.

TENMET kushirikiana na Equality Now kupaza sauti za watoto


Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (kulia) akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatili zinazowakabili watoto, maonesho hayo yameandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) kwa kushirikiana na taasisi ya Equality Now.

Meneja Kampeni wa Taasisi ya Equality Now, Bi. Florence Mashio akizungumza kuhusu unyanyasaji wa watoto hasa kwa mtoto wa kike pamoja na namna ya kuupinga ukatili huo wakati wa maonesho ya  ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatilizinazowakabili watoto lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

MTANDAO wa Elimu Tanzania (TenMeT) na taasisi ya Equality Now imekubaliana kufanyakazi kwa pamoja kuhakikisha inapaza sauti za watoto juu ya changamoto mbalimbali za ukatili zinazowakabili hasa watoto wa kike.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatili zinazowakabili watoto, yalioshirikisha wanachama wa TenMet, Meneja Kampeni wa Equality Now, Bi. Florence Machio alisema matatizo yanayowakumba watoto katika nchi nyingi za afrika yanafanana hivyo kuna kila sababu ya kushirikiana kuyakabili.

Alisema vitendo vya unyanyasaji wa watoto vimekuwa vikiwakatili watoto ndoto zao na 
kurudisha nyuma Bara la Afrika kielimu, kwani wengi wamejikuta wanakatishwa masomo 
kutokana na ukatili wanaofanyiwa kama vile kutiwa mimba utotoni, kuozeshwa, vitendo vya 
ukeketaji na ubakaji dhidi yao.

"Matatizo yanayowakabili watoto nchini Tanzania hayana tofauti na yanayowakabili watoto katika mataifa mengine ya Afrika...hivyo tunapohimiza mabadiliko ya sera na sheria zisizowalinda watoto tuungane kwa pamoja bila kujali unatoka taifa gani," alisisitiza Bi. Machio.

Kwa upande wake, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao akizungumza kabla ya kufungua majadiliano kwa wanachama alisema licha ya kushinikiza mabadiliko ya sera na sheria zinazoshindwa kuwalinda watoto sauti za mtoto mwenyewe hazina budi kupazwa ili zisikike kwa jamii nzima.

Aliwataka wajumbe wa mkusanyiko huo kutoka na suluhisho baada ya majadiliano ya pamoja ili kumsaidia mtoto kufikia malengo yake. Alisema wajumbe watapata muda wa kupitia sauti za baadhi ya watoto wakiwa katika changamoto zinazowakabili na kutoka na suluhisho la pamoja kumlinda mtoto.

Mkutano huo mbali na kushirikisha wanachama wa TenMeT ulihudhuriwa pia na wadau pamoja na wawakilishi wa Serikali kutoka idara husika. Equality Now inafanya kazi katika mataifa ya Sierra Leone, Gambia, Mauritania, Kenya, Uganda na Tanzania.


Mwezeshaji na Meneja Programu wa Mtandao wa Elimu Tanzania, (TenMet), Bw. Nicodemus Shauri Eatlawe akizungumza namna ya kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia hasa kwa mtoto wa kike.

Baadhi ya wadau wakiangalia mabango yenye ujumbe mbalimbali zinazohusu kupaza sauti kwa ukatili wa mtoto wakati wa maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatilizinazowakabili watoto lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Afisa Programu wa TenMet, Bi. Alistidia Kamugisha (kulia) akichangia mada kwenye mkutano huo.

Baadhi ya wadau mbalimbali wakichangia mada wakati wa maonesho ya sauti za watoto juu ya changamoto anuai za ukatilizinazowakabili watoto lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wadau kutoka taasisi Binafsi na serikali wakiwa kwenye mkutano uliowakutanisha ili kuangalia namna ya kusaidia mtoto wa kike wakati wa maonesho ya sauti za watoto.

Thursday, February 22, 2018

Mtandao wa Wanawake na Katiba wajadiliana na wahariri Dar



Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.



Mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.

Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.


MTANDAO wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi leo umekutana na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi nchini.

Akiwasilisha mada kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika mkutano huo, mtoa mada na mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga aliwataka wanahabari kuangalia mfumo mzima wa siasa za vyama vingi na nini kinachoitenganisha siasa ya Tanzania na nchi nyingine bila kujali tofauti za itikadi za vyama kwenye masuala yanayohusu utu wa mwanamke, ushiriki wa mwanamke kuchangia fikra za siasa na uongozi.

Aliwataka kuchambua na kuangalia mambo yapi yatakayounganisha wanasiasa wote katika kutetea masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utu na haki za mwanamke na pia mfumo wa uongozi utakaowezesha vyama vya siasa kuimarisha demokrasia shirikishi yenye mrengo wa jinsia ndani ya vyama.

Pia kuchambua mfumo wa uongozi unaowezesha vyama kutatua migogoro ndani ya vyama vyao bila kutumia vitisho, na hususani vinavyoashiria kumsababisha mwanamke wa Tanzania asipende kushiriki katika shughuili za siasa au anaposhiriki ajisikie yuko salama.

Kwa upande wake Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi, Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza katika majadiliano hayo, alisema malengo ni kujadili kwa pamoja umuhimu wa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika masuala ya siasa na  uongozi nchini nchini.

Kujenga makubaliano ya pamoja jinsi waandishi wa habari watakavyochechemua umuhimu wa kuzingatia misingi ya jinsia kwenye masuala ya siasa na uongozi katika majukumu yao, na kujengeana uwezo wa masuala ya usawa wa jinsia na uongozi kwa ujumla.

Mkurugenzi wa Women Fund Tanzania (WFT), Mary Rusimbi (kushoto) akizungumza kwenye mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi kujadiliana masuala mbalimbali juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi na usawa wa kijinsia katika siasa na uongozi.

Baadhi ya washiriki katika mkutano wa Mtandao wa wanawake na katiba/uchaguzi na uongozi pamoja na wahariri wa habari na waandishi waandamizi wakifuatilia mijadala anuai katika mkutano huo.

Monday, February 12, 2018

UNESCO KUADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI DODOMA

Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari. Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo, usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo. Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni, Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo. Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani. Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio. Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki. Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi. Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika. Si tu redio inatumika kubadilishana Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika. Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii. Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO. Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo. Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii, kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na kuboresha uwezo wao katika kazi.

Waziri Mwakyembe akutana na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo SMZ kujadili ugeni wa viongozi wa FIFA na CAF

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (wapili kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam.

Na Genofeva Matemu –WHUSM

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi Februari.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia  ujio wa viongozi wa FIFA na CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili nchini na kufanya mkutana wao  tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari mwaka huu.

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo  mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha  kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote.

“Ugeni unaokuja kwa kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe.

Naye Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema kuwa hii ni fursa ya aina yake kwetu sisi kwani itatupa nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuona ni namna gani michezo inaweza ikasaidia katika kukuza na kuongeza uchumi kupitia utalii.

“Tunaamini kuwa wageni hao watakua mabalozi wazuri kwa kutuletea watalii kupitia michezo na kuitangaza nchi katika mataifa mbalimbali”  amesema Mhe. Juma.


Ujio wa viongozi wa FIFA na CAF ni bahati kubwa kwa nchi yetu na unatokana na matokeo chanya ya utendaji kazi mzuri unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Serikali lakini pia upigaji vita wa masuala ya rushwa na upangaji wa matokeo wakati wa mechi.

Wakazi Mwananyamala wavutiwa na huduma za 'One Stop Centre' za CRC

Mwanasheria wa Kituo cha Usuluhishi–CRC, Suzan Charles (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jana jijini Dar es Salaam.

Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma.


Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.


Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huza

huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na

msaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi ya

Mtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogeza

huduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.

"...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa na

kesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona

kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"

alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya

akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa na

muitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwa

vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili za

matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikia

muafaka juu ya mvutano wao.

Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa

huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapo

huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na

ushauri wa kisheria utatolewa.

"...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji huduma

hizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa

kuja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwa

pia," alisema Bi. Chonya.

Tuesday, February 6, 2018

MWANAHABARI PATRICK MWILLONGO ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU


Kutoka kushoto ni Wanahabari Hellen Mwango, Careen, Kulwa Mwaibale na mke wa Patrick Mwillongo wakiwa wamekaa nje ya Hospitali ya Mkoa Temeke wakitafakari namna ya kumsaidia Mwillongo walipofika  kumjulia hali yake.


Na Mwandishi Wetu

Ndugu wanahabari mwenzetu, Patrick Mwillongo yupo hoi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambako amelazwa kwa matibabu.

Mwillongo anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji kwenye mapafu ambao umesababisha hashindwe kujimudu kufanya jambo lolote.

Kwa umoja wetu na tabia tuliojijengea kama wanahabari tujitokeze kumsaidia mwenzetu ambaye anapita katika kipindi kigumu.

Mwillongo ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea
 na anafanya shughuli zake wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na awali alikuwa akiandikia magazeti mbalimbali likiwemo Jambo Leo na yale yanayomilikiwa na Kampuni ya New Habari.

Kwa atakayegusw.a kumsaidia anaweza kutoa mchango wake kupitia namba MPESA-0754362990, Tigo Pesa ni 0712727062



SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...