Sunday, December 25, 2016

TTCL yanogesha sherehe za Chrismass Vituo vya Watoto Yatima Dar

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi mfuko wa unga, . TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa  Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi.


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi Mkurugenzi Msaidizi wa  Kituo cha Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. 


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa tatu kulia) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA maji ikiwa ni moja ya bidhaa zilizotolewa. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. 


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mfuko wa unga Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA, Evans Tegete ikiwa ni baadhi ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo. TTCL imekabidhi msaada wa bidhaa mbalimbali vikiwemo mchele, sukari, mafuta ya kupikia, soda, maji ya kunywa na mbuzi kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. 


Picha ya pamoja ya baadhi ya watoto kutoka vituo vyote vilivyosaidiwa na viongozi wao. 


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi mbuzi mmoja wa watoto wa kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi cha Kimara SUCA. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho, Evans Tegete.


Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemus Mushi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa watoto wa kituo cha yatima 'Yatima Group Trust Fund Mbagala Chamazi sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni ya TTCL kwa ajili ya sherehe za Siku Kuu ya Chrismass. 


Picha ya pamoja baada ya shughuli ya kukabidhi misaada hiyo.


Baadhi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu wakibeba sehemu ya misaada waliyokabidhiwa na TTCL.


Saturday, November 26, 2016

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AONGOZA MAHAFALI YA CHUO KIKUU CHA KAMPALA JIJINI DAR ES SALAM

 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
 Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
 Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto) na mgeni rasmi katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Muhammad Ndaula katika mahafali hayo yaliyofanyika jana.
 Baadhi  ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
 Sehemu ya wakufunzi na wahitimu wa Chuo Kikuu cha Kampala wakiwa kwenye mahafali.

Mahafali yakiendelea


Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.

Na Mwandishi Wetu

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.

Rais Mwinyi alitoa kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.

Alisema kitendo cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.

Alisema wahitimu hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika 
maisha yao. 

"...Nawapongeza wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele 
yako kisha uitumie kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.

Aidha Rais huyo mstaafu aliwataka wahitimu hao kuwa wachapakazi, wabunifu na kutumia ipasavyo ujuzi na elimu waliopewa katika ngazi mbalimbali ili 
kuweza kuisaidia jamii na taifa kwa ujumla. 

Alisema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kuhakikisha wanafunzi wote wenye sifa na vigezo vya kujiunga na chuo wanapata nafasi hiyo bila vikwazo kupitia 
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB). 

Akihimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili hasa kufundisha programu katika vyuo vikuu, Mwinyi alivitaka vyuo vikuu kuanza kufundisha programu za lugha hiyo ili
kuchochea matumizi yake kama yanavyofanya mataifa mengine kwenye vyuo vyao iwemo China, Urusi, USA, Iran na mengineyo.

Alisema Afrika lazima iwe na lugha moja ya kuwaunganisha watu wake na lugha pekee inayozungumzwa na mataifa mengi ya Afrika ni Kiswahili hivyo kuna kila sababu ya kujivunia lugha hiyo na kuitumia ipasavyo. "...Naahidi katika mahafali yajayo nitatoa hotuba yangu kwa lugha ya Kiswahili na salamu zangu zote nitazitoa kwa kiswahili," alisema Mwinyi.

Awali akizungumza katika mahafali hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), Profesa Ndaula Muhammad alisema jumla ya wahitimu 1079 wamehitimu masomo yao katika ngazi ya Shahada, Stashahada na Asatashahada katika fani mbalimbali.

Friday, October 28, 2016

Bi. Khadija Kopa Afunika Usiku wa Mshike Mshike Mwanza





Malikia wa Taarabu Afrika Mashariki na Kati, Khadija Omar Kopa, akitoa burudani kwa wakazi wa Jiji la Mwanza usiku wa kuamkia leo ndani ya Villa Park Resort kwenye show ya Usiku wa Mshike Mshike iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.




Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.




Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.





Bi.Khadija Omar Kopa pamoja na bendi yake ya Ogopa Kopa Classic alikonga nyoyo za wakazi wa Jiji la Mwanza.




Wananzengo wakifurahia burudani iliyotolewa kwenye Usiku wa Mshike Mshike na 102.5 Lake Fm





Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo




Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ilitambulishwa kwa Wananzengo kwenye show hiyo





Wananzengo kutoka 102.5 Lake Fm Mwanza




Timu ya Uongozi na Wafanyakazi wa 102.5 Lake Fm Mwanza pia ikijitambulisha kwa Wananzengo kwenye show hiyo




Madjz wa 102.5 Lake Fm, Dj Hcue (katikati), Dj KFlip (kushoto) na Dj Dhifa (kulia)




Dj Dhifa




Dj KFlip (kushoto) na Dj Hcue




Khadija Omar Kopa akihojiwa na wanahabari baada ya show




Hakika 102.5 Lake Fm Mwanza ni Raha ya Rock City na ni Redio ya Wananzengo. Kaa tayari kwa show ijayo.

TTCL, HUAWEI Wazinduwa Huduma ya Teknolojia ya 4.5G

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi  wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) wakishuhudia.


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (katikati) akipiga makofi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang (kushoto) mara baada ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. 

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora akizungumza kabla ya kuzinduwa rasmi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Huawei Tanzania, Bruth Zhang akizungumza katika uzinduzi wa teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni hiyo ambayo ni mshirika wa Kampuni ya TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) akizunguka kupata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. Kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Waziri Waziri Kindamba.






Meza kuu ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayesimamia Sekta ya Mawasiliano, Profesa Faustine Kamuzora (mwenye suti ya kijivu) ikipata maelezo namna teknolojia ya 4.5G inayofanya kazi wengine ni viongozi waandamizi wa Kampuni ya Huawei na TTCL. 

Kulia mmoja wa wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa matumizi ya teknolojia ya 4.5G inayotolewa na Kampuni ya Huawei ambayo ni mshirika wa TTCL katika huduma za teknolojia ya Mawasiliano akicheza gemu kwa kutumia teknolojia hiyo.

Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Peter Ngota (kulia) akipongezwa na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya kampuni ya TTCL kwa kushirikiana na Huawei kuzinduwa teknolojia ya 4.5G jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.






Sunday, October 23, 2016

Duka jipya la mavazi ya maharusi lafanya maonesho ya mavazi ya harusi


Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo pamoja na Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa (kulia). Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania. 

Mmiliki wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) akimlisha keki Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria. 
WABUNIFU wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi wamejitokeza kufanya maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi katika uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaa. Uzinduzi huo uliofanyika jana eneo la Sinza Madukani ulipambwa na mbunifu wa mitindo kutoka nchini Nigeria ajulikanaye kwa jina la Femi, mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mwendeshaji wa duka la Precious Wedding House, Victoria Chuwa ambao ni waandaaji wa onesho alisema waliamua kufanya onesho hilo ili kutoa fursa kwa wananchi hasa wanaoelekea kufanya harusi kujua mitindo mbalimbali ya mavazi ambayo wanaweza wakaitumia katika shughuli zao za harusi na kuonekana tofauti kimuonekano.

Alisema wabunifu walifanya maonesho ya mavazi katika mitindo mbalimbali kutumia mavazi ya hali zote ikiwa ni kuonesha jamii harusi si lazima muhusika au maharusi kutumia gharama kubwa bali wanaweza kutumia gharama za chini na kuonekana wenye mvuto kama watapata ushauri kutoka kwa wabunifu na wanamitindo.


Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) akimlisha keki Mmiliki wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana, Mary Monyo (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria. 

Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki Mwendeshaji wa duka hilo, Victoria Chuwa (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. 

Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimlisha keki mmoja wa wageni waalikwa mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. 


Mbunifu maarufu wa mitindo kutoka nchini Nigeria, Femi (wa pili kushoto), pamoja na mbunifu maarufu nchini Tanzania, Strayton Mashulano (wa kwanza kulia) wakiwa katika pozi pamoja na baadhi ya wanamitindo chipukizi kutokea nchini Tanzania, kwenye maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanyika katika duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. 
Alisema duka lao pamoja na kuuza nguo za maharusi watakuwa wakitoa ushauri bure kwa maharusi endapo watafika katika duka hilo ambalo limekuja kuleta mabadiliko katika mitindo ya maharusi. Alisema duka hilo litahudumia watu wenye kipato cha chini, cha kati na hata cha juu kulingana na mahitaji ya wahusika huku wakinufaika kwa ushauri bure kila atakaetembelea na kuomba ushauri kwa wataalamu wa mitindo.

Alisema duka hilo kubwa la mitindo ya maharusi wa kike na kiume linatumia wataalamu wa mitindo kutoka nchi za Uturuki, Marekani, Italia pamoja na Tanzania. Alisema wamekuja kuondoa dhana iliyojengeka kuwa nguo za maharusi ni anasa kutoka na maduka mengi kuuza bei kubwa kuliko inavyotegemewa, hivyo kupitia kwa wataalam wao maharusi wanaweza kufanya shughuli kwa bei ndogo na kuvutia.

"...Watu wengi wanaona mavazi ya maharusi ni kama anasa kutokana na bei kubwa za mavazi haya, sisi tumeamua kuleta mabadiliko hapa dukani kuna nguo za makundi yote, yaani watu wa kipato cha chini, watu wa kipato cha kati na hata watu wa kipato cha juu...unaweza kuandaliwa nguo yako ya harusi na wanamitindo kutoka nchi tulizotaja wewe ukiwa hapa hapa nchini na ukaipata ndani ya siku 21.

Akizinduwa duka hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang, Emelda Mwamanga alimpongeza mwanamama mjasiliamali na mmiliki wa duka hilo, Mary Monyo kwa uamuzi wa kusaidia kutoa ushauri kwa maharusi jambo ambalo limekuwa likipasua vichwa kwa wahusika. Alisema kitendo hicho kinatoa changamoto kwa akinamama wajasiliamali kuweza kufanya mambo
makubwa kibiashara.

Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo akimkabidhi zawadi ya keki Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' kwenye uzinduzi wa duka jipya kubwa la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulienda sambamba na siku ya kuzaliwa Khadija Shaibu 'Dida'.

Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kushoto) akimwonesha moja ya magauni ya maharusi Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kulia) mara baada ya uzinduzi wa duka la mavazi ya maharusi 'Precious Wedding House' lililozinduliwa jijini Dar es Salaam jana. Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani ulikwenda sambamba na maonesha ya mavazi mbalimbali ya maharusi yaliofanywa na wabunifu wa mitindo maarufu kutoka Tanzania na Nigeria na wanamitindo chipukizi toka Tanzania. 

Mkurugenzi Mtendaji wa jarida maarufu nchini la Bang 'Bang Magazine', Emelda Mwamanga (kushoto) pamoja na Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu 'Dida' wakifungua mvinyo kwenye  Uzinduzi huo uliofanyika Sinza Madukani.

Mmiliki wa duka la Precious Wedding House, Mary Monyo (kulia) akigonganisha glasi ya mvinyo na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...