Thursday, May 5, 2011

Harusi ya mwana Mfalme Prince William na Kate Middleton

Ilikuwa ni harusi ya kifahari;

Aprili 29 itabaki kuwa siku ya kumbukumbu ya milele kwa wanandoa Prince William pamoja na mkewe Catherine (Kate) Middleton baada ya kufunga ndoa yao ya kifahari iliyogharimu mamilioni ya paundi za Uingereza.

Harusi hiyo iliyoudhuriwa na umati mkubwa wa viongozi na watu maarufu inakadiriwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha kuliko harusi zilizowahi kufungwa ulimwenguni. Zaidi ya watu bilioni mbili kutoka nchi mbalimbali walikuwa wakiishuhudia kupitia luninga zao. Zifuatazo ni picha mbalimbali za harusi hiyo:-


Kate akiwasili kwenye makazi ya Mwana Mfalme, Prince William kabla ya kufunga ndoa, akiwa na msimamizi wake pamoja na baba yake Middleton.



Prince William na Kate mbele wakiingia kanisani wakiambatana na msafara wao wa harusi. 


Prince William akimvisha pete Kate kanisani mbele ya Mchungaji.


Maharusi Kate na William baada ya ndoa yao ya kifahari.



Prince William akimbusu mkewe mara ya kwanza muda mfupi baada ya kufunga ndoa. Hata hivyo taarifa zinaeleza maarusi hawa waliahirisha kwenda fungate baada ya sherehe hiyo kwa kuvikwepa vyombo vya habari. Walipanga kulifanya tukio hilo kimya kimya baadaye bila mapaparazi kuwafuatilia.



Mwanasoka maarufu duniani David Beckham na mkewe ni miongoni mwa watu maarufu waliohudhuria ndoa hiyo



No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...