Friday, September 29, 2017

Mwandishi Guardian ashinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona (kushoto), akimkabidhi cheti Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili kwa waandishi wa Televisheni kwenye shindano hilo lililofanyika jana nchini Uganda.

 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye alipata tuzo na kuwashinda wenzake ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uganda na Mjumbe wa Bodi ya ASARECA, Dr. Ambrose Agona, akimkabidhi cheti Mwandishi wa Tanzania wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ambae alishinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.  
Keki ikikatwa katika hafla hiyo

Na Mwandishi Wetu

Mwandishi wa gazeti la Guardian, Gerald Kitabu ameshinda tuzo ya umahiri wa habari za sayansi katika eneo la magazeti huku akiwaashinda waandishi wengine kutoka nchi zingine saba za Afrika.

Kitabu alikuwa anachuana na waandishi kutoka nchi za Nigeria, Burkina Faso, Ghana, Ethiopia, Kenya, Tanzania na Uganda. Shindano hilo lilifanyika jana katika Hoteli ya Speke Resort Munyonyo iliyoko nje kidogo ya jiji la Kampala.

Kwa ushindi huo, Kitabu ambaye ni mshindi wa jumla wa shindano la Tanzania, alijinyakulia kitita cha dola za marekani 1,500 pamoja na simu aina ya iPhone 7+ yenye thamani za dola za Marekani 1,200. 

Mwandishi mwingine wa Tanzania aliyepata tuzo ni Koleta Makulwa kutoka Radio Free Afrika ambaye aliwashinda waandishi wengine ambao walikuwa wanashindana katika eneo la Radio. ambapo Tanzania ilizidi kung'ara baada ya Mwandishi wa Star Tv Dino Mgunda kuwa mshindi wa pili katika waandishi wa televisheni. 

Koleta aliondoka na kitita cha dola za Marekani  1,500, simu aina ya iPhone 7+ ya thamani ya dola za marekani  1,200 wakati  Dino Mgunda alipata zawadi ya dola za marekani  1,000 na simu ya iPhone7+  ya thamani ya dola za marekani 1,000.

Katika shindano hilo jumla ya waandishi 20 waliwakilisha nchi hizo. waandishi hao ni wale ambao walikuwa washindi katika shindano la nchi mahalia, shindano ambalo lilifanyika mwanzoni mwa wiki hii katika nchi hizo ikiwemo tanzania. 

Shindano hilo liliandaliwa na Jukwaa la wazi la Bioteknolojia za Kilimo (OFAB) ambalo linahamasisha matumizi ya bioteknolojia katika kilimo ili kuwezesha nchi za Afrika ziweze kujitosheleza kwa chakula.

Mshindi wa jumla katika shindano hilo la jana ni  mtangazaji wa kituo cha  TVC, Omolara Afolayan kutoka Nigeria. Washindi waliteuliwa na jopo la majai watano.

Mafunzo ya Elimu ya ufundi yana nafasi ya kukuza ajira- Rutayuga

Mafunzo ya elimu ya ufundi yananafasi kubwa ya kuongeza, kusaidia na kukuza ajira kwa vijana wanaosoma masomo hayo kwenye vyuo vya ufundi kwa kuajiriwa au kujitengenezea ajira wao wenyewe. Kaimu katibu mtendaji wa baraza la taifa elimu ya ufundi (Nacte), Dkt, Adolph Rutayuga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu mkuu wizara ya elimu,sayansi na teknolojia, Dkt, Rutayuga amesema nia kubwa ya mradi huo ni kuangalia ufundi unaumuhimu gani kwenye sekta ya uchumi hasa unapozungumzia sekta ya uchumi wa viwanda. Aidha tunaangalia ubora wa mafunzo yanayotolewa kwenye elimu ya ufundi sababu kukiwa na vyuo vingi ambavyo vinaendeshwa katika ubora usiotakiwa, wanafunzi wanaotoka kwenye vyuo hivi hawatakuwa wazuri. 

“Tunalenga kujenga mazingira ya kutoa mafunzo bora kwenye elimu ya ufundi, elimu iliyobora kwa kusapoti walimu wanaofundisha,miundombinu ya kujifunza na kufundishia na pia kujaribu kuangalia mahusiano yaliyopo kati ya viwanda na soko la ajira kwa kile kinachotolewa kwenye vyuo vya ufundi.

Ameongeza, kama suala zima la mambo ya mitaala, linaweza kuboreshwa, na ile dhana potufu ya kizamani iliyokuwepo kwamba kwamba Tivet ni kwa wale walioshindwa,inapaswa iondoke, watu wajue kwamba mchango mkubwa kwenye uchumi unafanywa na hawa watu kwenye sekta ya kati “Malengo makubwa ni kujaribu kuinua ubora wa mafunzo yanayotolewa na vyuo vya ufundi, kuinua umuhimu mafunzo ya ufundi na Jinsi inavyoweza kisaidia kwenye maendeleo ya kukuza uchumi,” amesema.

Naye, Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe amesema warsha hiyo itajadili kwa undani vitendo vya ufanisi, utekelezaji na jukumu la uwezo ambao kila wadau watafanya katika mradi uliopendekezwa chini ya maeneo matatu umuhimu, ubora na mtazamo wa elimu na ujuzi wa kiufundi. “Elimu bora kwa Afrika itatekelezwa kuanzia mwaka huu hadi 2021 kwa lengo la kukuza elimu na ujuzi wa kitaaluma na mafunzo ambayo ni muhimu kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya watu binafsi na jamii”amesema Plathe. Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii.

Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe akizungumza washiriki wa warsha ya kuzindua Mradi wa mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini yaliyoandaliwa na UNESCO warsha hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam leo.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Rutayuga akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia wakati wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Unesco ya kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washririki na Meza kuu wakiwa katika warsha ya uzinduzi wa Mpangowa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Baadhi ya washririki wa Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya washiriki Warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini katika warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Kaimu Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Axel Plathe na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa elimu ya Ufundi (NACTE), Adolf Lutayuga wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


Mtoa maada akizungumza na washiriki wa warsha ya kuzindua mpango wa kuimarisha elimu na mafunzo ya ufundi nchini warsha iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AONGOZA KIKAO KUJADILI KANUNI ZA MAUDHUI MTANDAONI

Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers, Online Media) wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Kanuni  zizojadiliwa ni maudhui yanayorushwa na vituo vya uatangazaji  vya Redio na Televisheni n maudhui mitandaoni (Online Content) Jumla ya vyombo vya habari 76 vilishiriki kwenye kikao hicho. Wadau wamepewa wiki moja kuwasiliasha maoni yao kwenye kamati ya mashauriano ili yajadiliwe na kufanyiwa kazi kwa lengo la kuboresh kanuni.

 Wamiliki wa Wmiliki na wafanyakazi wa Vituo vya Televisheni na Radio wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel (Katikati waliokaa), viongozi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kumalizika kwa kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel akizungumza  kuhusu mambo mbalimbali waliyokubaliana katika kikao cha mashauriano na Wadau kuhusu  huduma ya Utangazaji  (Maudhui) na kanuni za maudhui mitandaoni leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.


 Wadaui wa habari wakiwa katika kikao hicho.




 Meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group,  Nathan Rwehabura akichangia mada wakati wa kikao hicho, ambapo pia alilalamikia ada kubwa inayotozwa kwa mwaka wamiliki wa vituo vya tv ambayo ni dola 25,000 sawa na sh/ mil/ 60.



 Mkurugenzi mstaafu wa Utangazaji wa TCRA, Habby Gunze akifafanua jambo katika kiao hicho.


 Wakili wa Jamii Forum Benedict akichangia mada wakati wa kikao hicho.


  Mkuu wa Vipindi wa EAST aFRICA radio, Nasser Kingu akichangia mada wakati wa kikao.





Asasi za Kiraia Zanzibar zawafunda raia juu ya Utetezi na Ushawishi Sera

 Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuelekea katika vijiji viwili tofauti vya Msowelo na Matombo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.  


 Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao.

  Kundi lililokuwa likielekea Matombo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
 Wakiwasili Msowelo
Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar zimeendelea na mafunzo ya siku mbili kuhusu Utetezi na Ushawishi wa Sera mkoani Morogoro. Asasi mbalimbali kutoka Zanzibar na Pemba ziko katika ziara ya Mafunzo iliyoratibiwa na Foundation for Civil Society (FCS) chini ya mwamvuli wa Association of Non Governmental Organizations of Zanzibar (ANGOZA) inakutanisha wawakilishi Zaidi ya 40 kutoka Zanzibar ambao wamekuja kujifunza namna mashirika ya MVIWATA (Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal Center).
Katika siku ya pili washiriki hawa wamepata fursa ya kwenda uwandani ili kukutana na wanufaika wa kazi mbalimbali zinazofanywa na MVIWATA na MPLC. MVIWATA imewapeleka washiriki wilayani Kilosa katika kijiji cha Msowelo ambapo kijijini hapa kumekuwa na migogoro ya Wkulima na Wfugaji ambapo kijijini hapa MVIWATA imefanikiwa kutumia mtandao wake wa msingi kupaza sauti kwa serikali ili kutenga maeneo ya wakulima. Tayari wilayani hapa kuna mashamba 9, ambayo yamefutwa na yamekabidhiwa katika mamlaka ya wilaya ili yagawiwe kwa wananchi.
Kwa upande wa MPLC yenyewe inawaonesha washiriki hawa kazi zao katika eneo la Matombo ambako huko pia MPLC inafanya kazi za utetezi wa haki za umiliki wa ardhi kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto hiyo. Shirika hilo limejizolea sifa kwa kazi zake mkoani Morogoro na pia ni shirika kongwe ambalo linafanya kazi za utetezi na ushawishi mkoani Morogoro.
Washiriki kutoka Zanzibar wanatumia nafasi hii kubaini changamoto mbalimbali zinazoyakumba makundi mbalimbali katika jamii ilhali kukiwa na mapungufu katika sera na maamuzi hali inahyowahitaji wananchi kufanya ushawishi na utetezi wa haki za kila kundi ili kuchochea jamii kubaki ikiishi kwa mani na ikiendesha maisha kwa mafanikio.
 Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Zainab Kisegele, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Ally Omary, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Washiri wakisikiliza kwa umakini
 Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Msowelo
 Washiriki waliokuwa wakielekea Matombo wakiwa katika gari kuelekea katika mafunzo kwa vitendo.


 Wakiwa katika mafunzo
 Wakiuliza maswali kwa wenyeji wao ili kujifunza zaidi
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
Ushuhuda .......
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Matombo.
 Baada ya mafunzo kwa pande zote mbili Msowelo na Matombo, washiriki walikutana tena na kuungana kwa majadiliano baada ya mafunzo kwa vitendo.



 
Washiriki wakijielezea jinsi walivyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao walokokwenda.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...