Tuesday, December 27, 2011

Harusi ya Bw. Boniface & Bi. Ruth


Maharusi Boniface na mkewe Ruth wakiwa katika pozi


Bi. Ruth akila kiapo kanisani Desemba 3, 2011 cha kukubali kumpokea Boniface kama mumewe katika maisha yao yote.


Boniface na mkewe Ruth wakinyweshana mvinyo kwa ishara ya upendo katika hafla ya harusi yao iliyofanyika katika Ukumbi wa Rombo Green View Hotel - Sinza jijini Dar es Salaam.


Picha ya pamoja na wazazi!


Wapambe mapambo wa maharusi wakiwa katika pozi! Picha zote kwa hisani ya Blog ya Harusini.

Friday, November 25, 2011

Harusi ya Ronald na Nancy


Maharusi Bw. Ronald na Bi. Nancy wakiwa katika pozi!


Bi. harusi Nancy akimfisha pete mumewe Bw. Ronald mbele ya Padre ndani ya Kanisa Katoliki la Segerea jijini Dar es Salaam. Sherehe ya kukata na shoka ya harusi yao ilifanyika katika Ukumbi wa New World Cinema Jumamosi ya Oktoba 29, 2011.


Bw. Ronald na Bi. Nancy (katikati walioshikana) wakiwa na wasimamizi wao siku ya harusi yao.


Na hii ndiyo keki iliyotumika siku ya harusi yao.


Picha za kumbukumbu na watu muhimu!


Hii ndiyo kamati iliyofanikisha hafla nzima. "Asanteni na Mungu awabariki!"


Kwaherini jamani tunaenda kupumzika! Hivi ndivyo wanavyoonekana wakisema Bw. Ronald na Bi. Nancy walipokuwa wakitoka ukumbini mara baada ya hafla yao. Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog.

Harusi ya Bw. Kennedy na Bi. Neema


Bwana harusi Kennedy akiwa na mkewe Neema mara baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa la Azania Front (KKKT), na hapa wakiwa katika tafrija yao kabambe iliyofanyika katika Ukumbi wa kisasa wa Kualalumpa - Sinza, Novemba 12, 2011 jijini Dar es Salaam.


Hapa Bwana harusi Kennedy na mkewe Neema wakilishana kwa ishara ya upendo


Bwana Kennedy, mkewe Neema na wasimamizi wa ndoa yao wakinywa kwa upendo


Mabinti warembo waliopamba ndoa hiyo wakiwa ukumbini


Hivi ndivyo tulivyopendeza! Akina dada warembo (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na akina kaka watanashati (kulia) waliopamba harusi hiyo. Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog)

Sunday, October 16, 2011

Harusi ya Lucas Songoma na Raeli Moses


Maharusi Lucas Songoma (kushoto) na mkewe Raeli Moses (kulia) wakishirikiana kuweka saini cheti cha ndoa yao mara baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki la Mt. Yosef Jimbo Kuu la Dar es Salaam Oktoba 15, 2011. 


Paroko wa Parokia ya St. Josef (kushoto) akiwaongoza maharusi Lucas na Raeli kusaini vyeti vya ndoa yao kanisani mara baada ya kufunga ndoa.


Lucus akimvisha pete mkewe Raeli kanisani ikiwa ni ishara ya kuungana katika maisha mapya ya ndoa yao.


Flowers wa maharusi wakiwa katika pozi. "Cheki pozi letu, mnaonaje!"


Mama mkubwa wa Bwana Harusi, Mektilda Lutabana (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja nje ya kanisa na ndugu wa karibu wa maharusi.


Flowers girls wakiwa kwenye pozi la pamoja. "Tumependeza!"


Maharusi Lucus na Raeli katikati wakiwa na wapambe wao, wakati wa hafla yao kambambe iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi (City Centre) Dar es Salaam. (Picha zote kwa hisani ya familia ya maharusi)

Thursday, October 13, 2011

Harusi ya Roman na mkewe Dorotea


Maharusi Roman na mkewe Dorotea wakiangaliana na kupeana tabasamu la kupongezana kwa hatua waliofikia. Inapendeza sana!


Maharusi wakilishana kwa staili ya pekee tunda kwa ishara ya upendo ndani ya ndoa yao. Hafla kabambe ya harusi hiyo iliyofanyika Septemba 24, 2011 jijini Dar es Salaam.


Hapa ndipo mahali maharusi na waheshimiwa hawa walipumzika wakisherehekea hafla yao ndani ya Ukumbi wa Royal Skyline. Blog ya Harusi na Matukio inawapongeza maharusi hawa kwa hatua hiyo.


"Pokeeni zawadi hii kubwa ambayo tumewaandalieni ili muendelee kufurahia maisha ya ndoa yenu milele" ndivyo anavyoonekana kusema mtoa zawadi hiyo pichani. (Picha kwa Hisani ya Blog ya Harusini)

Saturday, October 8, 2011

Rais Kikwete asherehekea siku ya kuzaliwa, atimiza miaka 61


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimlisha kipande cha keki mumewe Rais Dk. Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kutimiza miaka 61 ya kuzaliwa kwake iliuyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam juzi jioni. Anayeshuhudia ni mwanawe Ridhwani Kikwete na mkewe pamoja na Aziza, mjukuu wa Rais (Picha na Ikulu).

Wednesday, October 5, 2011

Harusi ya Victor Balthazar Minja na Edna Yusufu Bakari


Bwana Victor Balthazar Minja na Bi. Edna Yusufu Bakari wote wa Arusha Oktoba Mosi, 2011 walikata shauri na kuamua kuishi maisha mapya ya mume na mke. Bw. Victor ni Msanifu Majengo wa Wakala wa Majengo Tanzania na Bi. Edna ni mfanyakazi mkoani Arusha. Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Profesa Balthazar Mashindano Minja, Boko-Ununio Beach. Baada ya ibada takatifu ya misa kanisani.


Kama unavyoona kwenye pichani zoezi la nilishe nikulishe lilianza. Hapa safari ya kuelekea kwa wakwe. "Wazazi tulieni mlishwe keki!"


Na baadaye mambo ya picha za kumbukumbu yakafuata. Hata hivyo kwa mapicha zaidi tafadhali mdau ingia; www.prince minja.blogspot.com Picha zote na Prosper Minja



Sunday, October 2, 2011

Harusi ya Joseph na mkewe Maria iliyofanyika Dar es Salaam


Bwana Harusi Joseph (kushoto) akiwa na mkewe Bi. Harusi Maria muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Bwana Harusi Joseph (kulia) akimvisha pete mkewe Maria ikiwa ni ishara ya kuungana katika maisha ya ndoa yao milele, wakati wa ibada ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Maharusi Jeseph na mkewe Maria (kushoto) wakifungua muziki kwenye hafla yao. Kulia ni wasimamizi wao wakicheza kuwaunga mkono maharusi hao. (Picha kwa Hisani ya Blog ya Harusini)

Monday, September 19, 2011

Siku Deogratius Hugo alipofunga ndoa na Irene


Deo akiwa amembeba my wife wake baada ya pingu za maisha 

Safari ya Kanisani kwenda kula kiapo cha kuungana na uaminifu kwenye maisha ya ndoa takatifu.


Deo akila kiapo huku akimfisha pete ya ndoa mkewe Irine kanisani

Zikafuata picha za kumbukumbu baada ya ndoa kufungwa kanisani, Cheki pozi hili!


Hapa ni Deo na kampani yake ukumbini wakipata picha ya ukumbusho.

Wapambe wakisafisha njia kuingia ukumbini tayari kwa kuanza hafla rasmi ya harusi yao.

Wakikata keki na baadaye kulishana kwa ishara ya upendo

Hapa wakipata maelekezo namna ya kukata ndafu na kulishana kutoka kwa mtaalamu wa ndafu, Siunajua mtu asili yake kwao! Ndafu Bwana!

Hapa wakifungua muziki pamoja na wasimamizi wao, pembeni kulia ni wapambe wakishuhudia rumba. Si mchezo!

Sunday, September 18, 2011

Harusi ya Erasto Shirika na Mkewe Sumia


Bwana Harusi Erasto Shirima akiwa na mkewe Sumia wakiwa katika hafla yao iliyofanyika King Palace Hotel, Ukumbi wa Neema Sinza jijini Dar es Salaam Septemba 18, 2011.

Huu ni wakati wa ndafu, Bibi harusi Sumia akiandaa kipande cha nyama kwaajili ya kumlisha mumewe.


Bi Harusi Sumia akimlisha kipande cha ndafu mabinti ambao wamewasimamia katika harusi yao.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa ukumbini kwenye harusi ya Erasto Shirima.


Baadhi ya wageni wakiendelea na viburudisho ukumbini.

Wageni waalikwa wakikata mti panda mti ukumbini.


Baadhi ya wageni waalikwa wakiendelea kupata burudani ukumbini.


Waharusi pamoja na wasimamizi wao wakipata chakula maalumu cha usiku ukumbini


Nahii ndio kamati iliyofanya maandalizi ya Harusi ya Bwana Erasto Shirima na mkewe, hapa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutoa zawadi ya kamati. (Picha zote kwa hisani ya familia)

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...