Sunday, February 28, 2016

UZINDUZI WA INTANETI YA KASI ZAIDI YA TIGO 4G MKOANI KILIMANJARO




Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara kampuni ya Tigo(B2B), Rene Bascope akiongea na wageni waalikwa na wanahabari wakati wa hafla ya uzinduzi wa  intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi.



Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Amos Makala(wa pili kulia) akimkabidhi Emmanuel Kilaga, zawadi kutoka Tigo   wakati wa hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Mtaalam wa mtandao kutoka Tigo Samira Baamar.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mkoani Kilimanjaro 

Mtaalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar(wa tatu kulia), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya washindi waliojishindia zawadi mbalimbali.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria kwenye hafla uzinduzi wa intaneti yenye kasi ya Tigo 4G LTE mjini Moshi juzi.

MWANAHABARI SULEIMAN MSUYA WA GAZETI LA JAMBO LEO AACHANA NA UKAPERA

 Mwanahabari Suleiman Msuya wa Gazeti la Jambo Leo akitafakari jinsi atakavyoyaanza maisha ya ndoa baada ya kufunga ndoa na Shamim Rabim nyumbani kwa bibi harusi Jet Lumo jijini Dar es Salaam leo mchana.
 Mke wa Mwanahabari, Suleiman Msuya, Shamim Rabim katika pozi
 Suleiman Msuya akimbusu mke wake.
 Ndugu, jamaa na marafiki wa Msuya wakiwasili ukweni kuoa.
 Msuya na mpambe wake wakiwa katika gari.
 Ndugu na Jamaa wa Msuya wakipunga upepo wakati wakisubiri ndoa kufungwa.
 Wakina mama wakiserebuka katika ndoa hiyo.
 Bibi harusi akipambwa.
 Wageni waalikwa wakishuhudia wakati ndoa ikifungwa.
 Sheikh Nurdin Ali (katikati), akifungisha ndoa hiyo. Kulia ni Bwana harusi Suleiman Msuya na kushoto ni Kaka yake bibi harusi Habib Hashim.
 Sheikh Nurdin Ali akitoa mawaidha baada ya kufungisha 
ndoa hiyo.
 Ubwabwa ukiliwa baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo.
 Bibi harusi akitia saini kwenye hati ya ndoa.
Bwana harusi Suleiman Msuya akiwa amemshika kichwani mke wake  ni kama anasema "Wewe ndiye mke wangu wa kufa na kuzikana na chochote nitakacho kuomba usininyime"

Wednesday, February 24, 2016

KLABU YA KIMATAIFA LIONS CLUB INTERNATIONAL YATOA MSAADA WA MADAWATI YA CHUMA SHINYANGA

Chama cha Kimataifa kinachotoa misaada mbalimbali ya Kijamii cha Lions Club International chenye makao yake makuu nchini Marekani kimetoa msaada wa madawati 165 yenye thamani ya shilingi milioni 18 katika shule ya msingi Town na Mwenge zilizopo katika manispaa ya Shinyanga ili kumaliza changamoto ya wanafunzi kukaa chini.

MSAJILI WA HAZINA AKAGUA UJENZI WA MRADI WA ECO RESIDENCE UNAOJENGWA NA NHC KINONDONI HANANASIFU

1
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akishuka kwenye gari wakati alipowasili kwenye mradi wa Eco Residence ulioko Kinondoni Hananasifu unaojengwa na shirika la Nyumba la Taifa NHC huku akiongozwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu tayari kwa ukaguzi wa jengo hilo ambalo nyumba zake zote zimeshauzwa na linatarajiwa kukabidhiwa hivi karibuni kwa Shirika hilo.
Akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya ukaguzi wa jeno hilo Msajiri wa Hazina Bw. Lawrence Mafuru amepongeza uongozi wa NHC kwa kazi kubwa wanayoifanya ambapo wamefanikiwa kujenga majengo yenye tahami ya shilingi Trilioni 3.5 kutoka umiliki wa mwanzo ambapo kulikuwa na majengo yenye thamani ya shilingi trilioni 1.
Mkopo uliotumika kugharamia ujenzi wa majengo hayo mapya kutoka mabenki mbalimbali ni jumla ya shilingi Bilioni 300 ambazo kiasi cha shilingi Bilioni 100 zimeshalipwa tayari katika mabenki hayo na kiasi cha shilingi bilioni 200 zinaendelea kulipwa
Naye Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu amesema shirika hilo linao mpango mkubwa wa ujenzi wa nyumba 500 za gharama nafuu kwa ajili ya watanzania wenye kipato cha chini ambazo zitaanza kujengwa mwaka huu huko Luguruni wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam..(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimsikiliza Violet Mafuwe Msanifu wa majengo kutoka kampuni ya CPI Iternational ambaye pia ni Meneja Mradi wa Eco Residence wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
3
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akimuuliza jambo Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu mambo mbalimbali kuhusu miradi ya shirika hilo wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
4
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi wa NHC Bw. Nehemia Mchechu wakati alipokagua ujenzi wa jengo hilo.
5
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
6
Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba NHC akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya Msajili wa Hazina kukagua mradi huo.
7
Bw. Lawrence Mafuru Msajili wa Hazina akiagana na Mkurugenzi wa NHC Bw Nehemia Mchechu mara baada ya kukagua ujenzi wa jengo hilo.
8
Jengo linavyoonekana kwa nje.
9

Friday, February 19, 2016

MANJANO FOUNDATION WAENDELEA KUWAELIMISHA WANAWAKE WA KANDA YA KASKAZINI

Mmoja kati ya wanawake walioshirikia Mafunzo ya Ujasiriamali Kutoka Mkaoni Arusha akiwa kwenye Muonekano tofauti Mara na Naada ya Kutumia Vipodozi kwa Usahihi baada ya Kupata Elimu hiyo na wataalamu kutoka Taasisi ya Manjano foundation.
Mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa arusha yameingia awamu ya pili.Washiriki wamepata fursa ya kufahamu zaidi kuhusu vipodozi vya LuvTouch Manjano na namna ya kuvitumia. Mkufunzi na Mkurugenzi wa taasisi ya Manjano Foundation amependekeza wanawake wa jiji la Arusha kutumia vipodozi kwa usahihi kwa lengo la kujijengea heshima na kujiongezea kipato katika kazi yao ya upambaji.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation na Mkufunzi wa Maswala ya Vipodozi Mama Shekha Nasser Akitoa elimu Kuhusu Matumizi Sahihi ya Vipodozi Kwenye Semina ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Jiji la Arusha 
Akielezea zaidi alisema matumizi sahihi ya vipodozi hasa vya LuvTouch Manjano vitakupa kazi nzuri na bora ambayo kila mteja ataipenda na kulifanya soko la kila mwanamke kukua kutokana na ubora wa kazi ya mikono yake

MAGUGU MAJI YATISHIA HUDUMA ZA USAFIRI ENEO LA KAMANGA FERRY JIJINI MWANZA.

Vita ya Kupambaza na Uwepo wa Magugu Maji katika Maeneo mbalimbali ya Ziwa Victoria, bado haijazaa matunda Chanya. 

Suala la kupambana na magugu maji katika ziwa hilo bado ni changamoto, licha ya kuwepo kwa Miradi mbalimbali ikiwemo ile ya Uhifadhi wa Mazingira ya Bonde la Ziwa Victoria (LIVEMPT I & II) iliyolenga kuokoa uwepo wa Ziwa Victoria ambayo pia ililenga kupambana na magugu maji.

Mara kadhaa huduma za usafirishaji katika Kivuko cha Busisi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, zimekuwa zikitatizwa na uwepo wa Magugu maji ambayo hutanda katika eneo la ferry la kivuko.

Usumbufu kama huo unahofiwa huenda ukajitokeza katika eneo la Kamanga Ferry Jijini Mwanza, baada ya Magugu Maji kugonga hodi na kuanza kutanda katika eneo hilo.

Kumbuka Magugu maji yanaweza kutambaa kutoka eneo moja hadi jingine kulingana na upepo unavyovuma na yanaweza kuleta athari ya usafirishaji majini ikiwa chombo cha usafiri (Meli/Ferry) kitanasa katika Magugu maji.

Suala kubwa ni kuhakikisha mapambazo zaidi dhidi ya magugu maji yanaendelea ikiwemo kuvitumia vikundi vya Kusimamia Rasilimali za  Uvuvi katika Ziwa Victoria (Beach Management Unit-BMU) ambavyo mara moja moja pale vinapowezeshwa, vimekuwa vikifanya shughuli ya kutoa magugu maji Ziwani.

Hata hivyo jitihada za vikundi hivyo zimekuwa zikikwama kuleta suluhisho maana magugu maji yanapotolewa majini, ni vyema yakachomwa moto jambo ambalo huwa ni nadra kufanyika na matokeo yake magugu maji hayo hurudi ziwani kwa njia moja ama nyingine, ikiwemo kwa njia ya shughuli za kilimo katika maeneo ya kandokando mwa ziwa Victoria.
Shughuli za Kupambana na Magugu Maji zikifanyika eneo la Nera Jijini Mwanza mwishoni mwa Mwaka jana
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group

VIJANA WASHAURIWA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI

Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez. Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.[/caption]
Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.
Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.
Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.
“Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,
“Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.
Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.
Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.
Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV)
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
IMG_3639
Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.
Kitenge Africa Volunteerism (KAV)
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.
    Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez. Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa. Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana. Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio. Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata. “Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi, “Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.    

TIGO YATOA MILLIONI 10 WAATHIRIKA WA MAFURIKO IRINGA

Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana .  Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa mabati kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) , ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana . [/caption]
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kusini, Jackson Kiswaga, akikabidhi msaada wa magodoro  kwa Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh Amina Masenza (katikati) ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa,wanaoshuhudia pembeni ni viongozi kutoka serikalini  makabidhiano hayo yalifanyika jana .

 
Magodoro waliyokabidhi tigo ikiwa ni ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana .


Wafanyakazi wa Tigo wakisaidia kushusha mabati yaliyotolewa na Tigo ikiwa pamoja  na msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika kata za Pawaga na Idodi,  mkoani Iringa, makabidhiano hayo yalifanyika jana


Iringa, Februari 17, 2016: Tigo imetoa msaada wa vyakula na vifaa vya kujengea nyumba vyenye thamani ya millioni 10/- kwa familia zilizoathirika na mafuriko katika wodi za Pawaga na Idodi, iliyosababisha watu wengi kukosa sehemu za kulala, mkoani Iringa.
Vifaa hivyo vilikabidhiwa leo kwa waathirika wa mafuriko na Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kusini Jackson Kiswaga, aliesisitiza ahadi ya kampuni kusimama kidete na wananchi katika wakati wa faraja na shida.
“Tupo hapa kujumuika na wasamaria wema wengine katika kuwapa pole walioathirika na maafa hayo, na tunawaombea kila la kheri waweze kurudi katika hali tulivu baada ya kupoteza wapenzi wao na mali zao,” Alisema Kiswaga
Vifaa vilivyo tolewa na Tigo ni mabati 350, magodoro 30 na mashuka 35.
Mvua zilizonyesha katika wodi hizo, iliripotiwa kwamba zilisababisha watu 1,155 kukosa sehemu za kulala, na pia mimea na makazi ya watu yaliharibika au kubebwa na mafuriko, taarifa hii ni kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Iringa mhe.Amina Masenza.
Msaada kutoka Tigo, kulingana na Kiswaga, ni katika mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii, sera hii ni ahadi kwa ajili ya kuwekeza baadhi ya rasilimali za kampuni katika miradi ya kuendeleza na pia katika kusaidia jamii majanga yanapo ibuka.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...