Tuesday, October 31, 2017

MKUU WA MKOA GEITA ATAKA KUWAPIMA UWEZO MAOFISA UGANI


Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk. Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akimkabidhi mbegu bora ya mahindi, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi  wakati wa uzinduzi wa mashamba darasa ya mbegu za mahindi, mhogo na viazi lishe uliofanyika nje ya viwanja vya ofisi ya mkoa huo jana. Kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo   (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhiwa mbegu hizo za mahindi zinazokabiliana na ukame  Wema.



 Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Isamilo kabla ya uzinduzi wa shamba darasa la mbegu ya mahindi. Kutoka kushoto ni Mtafiti kutoka COSTECH, Dk. Beatrice Lyimo, Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti cha Maruku mkoani Kagera, Jojianas Kibula, Mtafiti Bestina Daniel na Mshauri wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo   (OFAB), Dk. Nicholaus Nyange.


 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro,  Ismail Ngolinda, akitoa maelezo ya jinsi ya kupanda mbegu ya mahindi.


 wananchi wa Kijiji cha Isamilo wakiwa kwenye uzinduzi huo.


 Mkulima Hernick Elias wa Kijiji cha Isamilo akizungumzia changamoto za kilimo walizonazo.


 Watafiti wakifanya vipimo kabla ya uzinduzi wa shamba la mbegu za mahindi katika kijiji cha Isamilo.

 Wakulima wa Kikundi cha Nguvumoja cha Kijiji cha Isamilo wakiwa shambani wakati wa uzinduzi huo.

 Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Salome Renatus akizungumza na waandishi wa habari.


  Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro,  Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi.

 Ofisa Ugani wa Kijiji cha Isamilo, Issa Pegeege, akionesha jinsi ya uwekaji mbolea kabla ya kupanda mbegu ya mahindi Wema.


 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk. Bakari (kulia), kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akiongoza wakulima kupanda mbegu ya mahindi kwenye shamba darasa katika Kijiji cha Isamilo.

 Mkulima wa Kijiji cha Kikundi cha Nguvu moja katika Kijiji cha Kamhanga, Hamisi King akitoa maelekezo wakati wa uzinduzi wa shamba darasa la mahindi katika kijiji hicho.

 Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro,  Ismail Ngolinda, akionesha namna ya ujimbaji wa mashimo kabla ya upandaji wa mbegu za mahindi katika Kijiji cha Isamilo.

 Wakulima na wananchi wa Kikundi cha Kasimpya katika Kijiji cha Mnekezi kilichopo Kata ya Kaseme wakisubiri maelekezo namna ya kupanda mbegu za mahindi katika shamba darasa.

 Diwani wa Kata ya Kaseme, Andrew Kalamla akizungumza na wananchi katika uzinduzi wa shamba darasa hilo.

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnekezi.

 Mwakilishi wa Mkoa wa Geita, Emiri Kasagala, akihutubia katika uzinduzi huo kwa niaba ya mkuu wa mkoa huo, Robert Gabriel.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, akipanda mbegu wakati wa uzinduzi wa shamba darasa katika Kijiji cha Mnekezi. Kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Emiri Kasagala.

Na Dotto Mwaibale, Geita

MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel Lughumbi amesema ataanzisha utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wa mkoa huo utendaji kazi wao ili kujua uwezo wa kila mmoja wao.

Hayo ameyasema  wakati Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), ilipokuwa ikimkabidhi mbegu bora za mahindi, mihogo na viazi lishe ikiwa ni siku yake ya kwanza kufanya kazi katika mkoa huo tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kushika wadhifa huo.

"Kilimo ni muhimu sana hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaingia katika uchumi wa kati wa viwanda hivyo nitaweka utaratibu wa kuwapima maofisa ugani wote wa mkoa huu ili niweze kujua utendaji kazi wao" alisema Lughumbi.

Lughumbi aliwataka maofisa ugani mkoani humo kuacha kukaa maofisi kwenye viyoyozi badala yake waende walipo wakulima kushirikiana nao kuwapa elimu ya kilimo ili kujikomboa kiuchumi kupitia kilimo.

Mkuu huyo wa mkoa ameahidi kununua viatu vya shambani 'gambuti' na koti na kuwa mara moja ataanza kutembelea wakulima katika maeneo yao ili kujua changamoto zao na kusema anapenda kuona mkoa wa Geita unakuwa namba moja kwa kilimo hapa nchini.

Akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi na Viumbe Hai wa COSTECH, Dk.Bakari Msangi alisema kazi kubwa ya COSTECH ni kuishauri serikali katika masuala yote yanayohusu  Sayansi na Teknolojia na kusimamia tafiti zote za kisayansi katika maeneo mbalimbali na kilimo na kuhakikisha zinawafikia walengwa.

Alisema mbegu hizo walizozikabidhi zimefanyiwa utafiti na zitapandwa katika mashamba darasa na baadae kusambazwa kwa wakulima wengine ili kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mbegu bora kutokana na wakulima kukabiliwa na mbegu ambazo zilikuwa na magonjwa kama batobato na ukame.

Akizungumzia mbegu bora ya viazi lishe alisema mbegu hiyo viazi vyake vinavitamini A ya kutosha ambayo ni muhimu kwa watoto na hiyo itawasaidia baadhi yao kuto kwenda Hospitali kuipata badala yake wataipata kwa kula viazi hivyo.

Msangi aliwaomba maofisa ugani pale wanapokuwa na changamoto mbalimbali za kazi yao wasisite kwenda COSTECH ili kusaidiana na kupeana mbinu mbalimbali za kilimo.

Mkulima wa Kijiji cha Isamilo, Hermick Elias alisema kukosekana kwa mbegu bora, wataalamu wa kilimo na kutofikiwa na pembejeo za kilimo kwa wakati ni moja ya sababu ambayo imewarudisha nyuma katika masuala ya kilimo lakini wanaamini kwa mbegu hizo walizoletewa na COSTECH itakuwa nu mkombozi kwao kwa kupata chakula na ziada watauza na kujipatia fedha za kuwasaidia.

Alisema kwa kilimo walichokuwa wakikifanya ekari moja walikuwa wakipata mahindi kuanzia magunia nane hadi tisa lakini kwa maelezo ya watafiti hao wa kilimo iwapo watatumia mbegu hiyo bora wataweza kupata magunia kuanzia 25 hadi 30.

Mkulima Salome Renatus aliipongeza serikali na COSTECH kwa kuwapelekea mbegu hizo hivyo wanatarajia kupata mazao yenye tija tofauti na awali.

Mbegu hizo zitapandwa katika mashamba darasa katika wilaya zote za mkoa wa Geita, Nyang'wale, Mbogwe,Chato na Bukombe.

Monday, October 30, 2017

Mchekeshaji maarufu Joti atia fora 'miuno' siku ya harusi yake


Mchekeshaji maarufu wa Kundi la Orijino Komedi nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti akiwa na mkewe Bi. Tumaini Salehe mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.



Mchekeshaji maarufu wa Kundi la Orijino Komedi nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti akiwa na mkewe Bi. Tumaini Salehe mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.



Joti na mkewe akiwa na wapambe wake.

  MCHEKESHAJI maarufu nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti huenda akaingia katika kumbukumbu ya mwaka 2017 kuwa bwana harusi aliyecheza muziki akikata viuno kuliko maharusi wowote. Joti ambaye ni mchekeshaji wa Kundi la Orijino Komedi, alifunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Bi. Tumaini Salehe katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

 Mchekeshaji huyo akiwa katika sherehe ya ndoa yake iliyofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, aliongoza kwa kusakata rumba mwanzo mwisho jambo ambalo lilikuwa burudani tosha katika hafla hiyo.

"..Yaani jamani harusi ya leo ni kama show ya Joti...mwanzo mwisho ni kucheza," alisema mwanadada mmoja aliyeshiriki katika harusi hiyo. Katika harusi hiyo, Joti ambaye alikuwa katika muonekano wa mnyoo wa kiduku aliwavunja mbavu waalikwa kutokana na kucheza kwa vituko huku akimwaga miuno, tena mbele ya wakwe zake jambo lilioufanya mkumbi kufurahia kitendo hicho mara zote.

 Joti alimwaga miuno hadi kuona koti la suti yake linamzuia mara kadhaa hivyo kulivua na kuliweka pembeni ili amwage mauno sawasawa. Kundi la wana Orijino Komedi ambao nao walimuunga mkono mwenzao walitoa 'show' kali ya kumwaga miuno kwa zamu ambapo walimuinua tena Joti alipoketi na mkewe na kuendelea kumwaga miuno, kabla ya kuingia tena mwimbaji maarufu wa muziki wa dansi, Christian Bella ambaye pia alimchezesha Joti kana kwamba waliandaa show ya kuwaburudisha waalikwa wake.

 "..Yaani leo bwana harusi huyu atalala hoi...si kwa miuno hii," alisema dada mmoja akiwa anachukua video kwa kutumia simu yake. Kwa historia hiyo huwenda Joti akawa bwana harusi pekee aliyecheza kwa muda mrefu tangu kuanza kwa sherehe yake hadi mwisho.

 
Bi. Tumaini Salehe siku ya send off akiwa na mumewe mtarajiwa.


Mchekeshaji maarufu wa Kundi la Orijino Komedi nchini Tanzania, Lucas Lazaro maarufu kama Joti akiwa na mkewe Bi. Tumaini Salehe mara baada ya kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki la Magomeni jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

Waziri Mwakyembe azindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya Uhuru

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amezindua Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ambayo yanalenga kuonyesha namna mashujaa wa Tanganyika walipambana kupata uhuru, maonyesho ambayo yatafanyika kwa muda wa mwezi mmoja katika Makumbusho ya Taifa- Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam.

  Uzinduzi wa maonyesho hayo ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), kwa lengo ya kuendeleza juhudi za Uhifadhi wa Hifadhi ya Urithi Tanzania,hususani ya Ukombozi wa Afrika yanasimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

  Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maonyesho hayo, Dkt. Mwakyembe alisema mradi huo wa kuhifadhi historia ya Ukombozi wa bara la Afrika ni muhimu kwa Tanzania kwani unaweza kusaidia kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea nchini kuliko ilivyo sasa kwani inawapa nafasi wageni ya kuona mambo tofauti na yaliyozoeleka pindi wanapokuja nchini.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.

  “Tuna mradi ambao utatupeleka mbali sana Watanzania, Afrika Kusini, Namibia, Angola hata wao wametuambia tusije shangaa sehemu hiyo ikawa inaleta watalii wengi zaidi kuliko wanaokuja kuangalia tembo na simba, urithi wa Afrika tumekabidhiwa na bara la Afrika ni wajibu wetu Watanzania kuusukuma huu mradi maana tumeshachelewa, Watanzania wengi labda hawaelewi mwaka 2011 kwa kushirikiana na UNESCO tulipeleka ombi AU la mradi huu wa bara la Afrika na wakaubariki huu mradi na wakaamua makao makuu yawe Tanzania na sisi tukachagua Dar na hapa kitajengwa kituo kikubwa kitakuwa na historia ya Ukombozi wa Afrika, sisi ndiyo viongozi wa huu mradi,” alisema Dkt. Mwakyembe.

Alisema ili kufanikisha mradi huo tayari wameanza kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha pindi watakapojenga kituoambacho kitatumika kuhifadhi vitu mbalimbali ambavyo vilitumika katika kipindi cha ukombozi wa bara la Afrika kuwe na taarifa nyingi kuhusu bara la Afrika. “Tunawatumia wazee walio na historia ya ukombozi wa Afrika tumehoji zaidi ya wazee 100 na tunaendelea na hilo zoezi na tumebaini maeneo zaidi ya 200 Tanzania ambayo yanahitaji kuhifadhiwa, ni wajibu wangu kupeleka muswada bungeni ili tuyahifadhi na kuyalinda kwa kutumia sheria,” alisema Waziri Mwakyembe.

Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.

Kwa upande wa Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer alisema ni muhimu kwa bara la Afrika kuwa na maonyesho ambayo yanaelezea historia ya bara hilo ili yatumike kuelezea kizazi cha sasa na kijacho namna nchi za Afrika zilipambana kupata uhuru na wao kama EU wataendelea kusaidia miradi mbalimbali yenye lengo ya kutunza urithi wa bara la Afrika.

“Ni jambo la kujivunia kwa Umoja wa nchi za Ulaya kusaidia kufanikisha mradi huu … EU tumekuwa tukisaidia miradi mingi na hii yote ni kwa ajili ya kutunza utamaduni na urithi wa bara la Afrika, tumesaidia miradi mbalimbali nchini ikiwepo ya Olduvai na Ngorongoro na tutaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuendeleza maeneo ya kihistoria,” alisema.

Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.

  Naye Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO kanda ya Afrika Mashariki na Afisa Mwakilishi wa Unesco Dar, Ann Therese Ndong- Jatta katika hotuba yake iliyosomwa na Afisa Mpango Kitaifa wa UNESCO, Nancy Kaizilege alisema ni jambo zuri kuwepo na makumbusho ambayo yanaeleza historia ya bara la Afrika na yatawza kuwapa nafasi watu mbalimbali kutoka mataifa ya nje ya bara la Afrika kuona na kujifunza historia ya Afrika.

  “Makumbusho haya ni muhimu kwasababu ni sehemu ya ukumbusho wetu kwa baadae, kupitia makumbusho haya tutaona historia ya bara la Afrika, historia ya mwanadamu na safari ya kutafuta uhuru ilivyokuwa,” alisema Kaizilege.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer wakikata utepe katika uzinduzi wa Maonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa ameongozana na Balozi wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini (EU), Roeland Van de Geer na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuangalia vitu mbalimbali vya kihistoria ambavyo vimewekwa katikaMaonyesho ya Mashujaa na Mapambano ya kupata Uhuru.

Friday, October 27, 2017

SMILE BRINGS THE LOWEST DATA PRICES AT THE FASTEST INTERNET SPEEDS TO TANZANIANS


Linda Chiza, Head of Brand and Communications from Smile Communications Tanzania speaks to the launch of new range of data bundles at the lowestdata prices today.

TODAY Smile Communications Tanzania (“Smile Tanzania”) brings a new range of data bundles at the lowestdata prices with the highest internet data speedsto Tanzanians with ‘BeiyaNdizi’.

With BeiyaNdiziall Tanzanians have access to the lowest data prices with SmileAnytime bundles (daily, weekly and monthly validity), setting a new trend for the best value internetat SuperFast speedover 4G LTE,starting fromonly Tsh 2,000.

Smile Chief Commercial Officer, Arindam Chakrabarty says, “It is our endeavour that everyone in Tanzania is able to fully benefit from the internet world and we now bring our customers’ a wider range of data bundles that is more affordable and still offers the fastest internet in Tanzania”.

He further said that Bei ya Ndizi will see Smile customers being rewarded with BONUS data plus FREE data for Social Media,each time they recharge with SmileAnytime bundles. The FREE data for Social Media gives customers FREE access to Facebook, Instagram, WhatsApp and Twitter.

Smile, known for championing InternetFreedom in Tanzania, is also introducing new bundles for daily, weekly and monthly use, giving customers more freedom of choice and affordability.

“Smile’s SuperFast affordable internet service is available inDar es Salaam, Mwanza, Moshi, Dodoma, Morogoro, Arusha and Mbeya. We’ve reduced our prices that everyone can have the opportunity to experience Smile’s TRUE 4G LTE service and to stay productive and entertained at the fastestdata speeds;daily, weekly or monthly.” concludedMrChakrabarty.

Customers in Dar es Salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Mbeya and Morogorocan now experience the fastest, most reliable internet in Tanzaniaat the best data rates in town and can look forward to further 4G LTE innovations form Smile.

About Smile Tanzania coverage
Smile introduced Africa’s first 4G LTE mobile broadband service in Tanzania in May 2013, revolutionising the way people in East Africa access the internet. Our customers in Tanzania experience the country’s fastest and most reliable SuperFast mobile broadband and SuperClear voice services over 4G LTE across Smile’scoverage areas.


Serikali kuzitwaa ranchi zilizobinafsishwa na kushindwa kuendelezwa

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akilakiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura wakati alipofanya ziara ya siku moja wilayani humo.


 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe.

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi.Abdallah Ulega akisalimiana na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mkinga (OCD) kushoto ni Katibu Tawala wa Mkinga, Joseph Sura.

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili wilayani Mkinga.

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kulia akimsikiliza kwa umakini Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kushoto wakati akisoma taarifa ya wilaya hiyo.

 NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kabla ya kuanza ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali wilayani humo.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiagana na na Katibu Tawala wa wilaya ya Mkinga (DAS) Joseph Sura kulia mara baada ya kusaini kitabu cha wageni na kupata taarifa ya wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akilakiwa na Diwani wa Kata ya Mwakijembe.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga Rashid Gembe kulia ni Diwani wa Kata ya Mwakijembe.

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega katikati akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga, Rashid Gembe.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na Jamii wa Wafugaji wa Kimasai na wakulima katika Kijiji cha Perani ambapo aliwataka kuishi kwa amani kwa kufuata taratibu ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema serikali itazirejesha ranchi zote zilizobinafsishwa na kushindwa kuziendeleza. Amesema ranchi hizo zitagawiwa kwa wafugaji ili kufunguza tatizo la malisho nchini jambo.

Kauli ya Naibu Waziri huyo aliitoa wilayani hapa wakati wa ziara yake ya siku moja ambapo alisema kwamba lengo la kuchukua ranchi hizo ni kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambao kwa mara kadhaa wamekuwa wakigombania maeneo ya ardhi kwa ajili ya malisho na kilimo.

Alisema kwamba serikali imeamua kuchukua uamuzi huo ili kuepusha wafugaji waishio mipakani wasipeleke mifugo yao katika nchi jirani ambako kuna malisho.

HakiElimu wachangia mil20 ujenzi wa kisima Sekondari ya Mukulat, Wafanya usafi

+
 Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo, wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel, Arusha)


 Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii.



Wafanyakazi wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii.

  Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la  Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana.


Mmoja wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu

Wafanyakazi wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana.

Aliyeshika ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji  katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii.



Mwanafunzi shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya umwagiliaji shuleni hapo jana.



Meneja Idara ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka ngumu shuleni hapo.



Mfanyakazi wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi.



Rose Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha



Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Sekondari  Mukulat Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage, zawadi  iliyotengeneza katika klabu yao ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze.

Mkuu wa Miradi HakiElimu - Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili ya umwagiliaji.

Baadhi ya wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu


Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini, John Kalage kwa kutambua umuhimu wa elimu Nchini.

 Picha ya pamoja




Na Pamela Mollel,Arusha

Shirika lisilo la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda mwingi  kwakutafuta maji.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.

Shirika hilo la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat  watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya kifugaji.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii  ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora

Ameiomba jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto  yanaozikabili shule za msingi na sekondari na kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey  amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari 127  katika wilaya ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua ,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi kuapata elimu katika mzngira bora.


Awali wakizungumzi miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat  Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi. 

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...