Thursday, October 25, 2012

Women in Balance Kitchen Party Gala

Women in Balance Kitchen Party Gala ilivyowafungua macho wakinamama na mabinti Dar, hata hivyo wakinamama na mabinti walioko mikoani  mamedai kuwa vitu hivyo vizuri hupatikana tu Dar es salaam na kumlalamikia Mratibu wa Shughuli hiyo na kumtaka kwa mwaka ujao kuipeleka mkoani mbeya, au hata ikiwezekana Mwanza ili iwe ikifanyika kikanda kuliko kufanyika sehemu moja na kuwafanya wao kukosa mambo mengi ya msingi yanayopatikana katika function hiyo ya aina yake.




Msemaji katika Hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Chris Mauki akitoa somo la Saikolojia kwa wakinamama na wasichana waliohudhuria hafla hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall jijini Dar.

Life Style Designer of Sex and Relationships kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai akitoa somo la kuhusiana na masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa wenye ndoa na wasiokuwa na ndoa ambapo amesema vipo vitu vingi vinavyochangia kuboresha ama kuharibu mahusiano hayo ambapo wahusika wanatakiwa kuvifahamu na kuvitilia mkazo ili kudumisha mahusiano yao.



Msemaji wa mwisho alikuwa ni Mama Veronica aliyewaacha hoi kwa vicheko wanawake waliohudhuria Kitchen Party Gala ambapo alizungumzia masuala ya uvumilivu katika ndoa sio tu kukosekana kwa kipato ndani ya nyumba bali hata mikimiki ya Unyumba kwa wanandoa.
Independent Sales Consultant wa bidhaa za Oriflame Bi. Jesca Mwakyulu akionyesha bidhaa ya Feminele Intimate Wash ya Oriflame ambayo ameisifia kuwa na Natural Lactic Acid ambayo inasaidia kutunza hali halisi ya sehemu za siri za Mwanamke.
Amefafanua kuwa kwa asili sehemu hizo zina hiyo Lactic Acid ambayo hutunza unyevu sahihi na Bacteria wazuri ambao husaidi kutoa ulinzi dhidi ya Fangasi, miwasho na harufu mbaya.
Mmoja wa wadhamini wa Women in Balance Kitchen Part Gala Mwakilishi kutoka TSN Super Market Lizbeth akitangaza zawadi kumi kwa wageni waliohudhuria Kitchen Party Gala zikiwemo Vocha za kufanya Shopping katika Super Market za TSN zilizopo jijini Dar es Salaam.

 Aunty Sadaka na Mwanasaikolojia Chriss Mauki.


Wakinadada wakionekana kufurahishwa na mambo yaliyokuwa yakizungumziwa kwenye Kitchen Party Gala hiyo.
Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Juhyna Kusaga (kushoto) na mdogo wake.
Mbunifu nguli wa mavazi nchini Khadija Mwanamboka (kulia) a.k.a Kubwa la maadui alikwa miongoni mwa waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Women in Balance Kitchen Party Gala ilikusanya wakina mama na kina dada kutoka kila kona ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya nje kama inavyoonekana picha na hii kudhihirisha jinsi gani wakimama wanavyopenda kupata Elimu ya kudumisha ndoa zao na familia kwa ujumla.
Palikuwa hapatoshi hakuna hata pakuhemea.
What a beautiful smile.
Salma Msangi wa Channel Ten na Magic Radio.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios akiteta jambo na Mama Veronica.
 Vicheko, nderemo na vifijo vilitawala.

Skylight Band walikuwepo kutumbuiza Hafla hiyo. Uzao wa Bongo Star Search Mary Lukas akitoa burudani.
Aneth Kushaba AK 47 akiimba kwa hisia kali kukonga nyoyo za kinamama waliohudhuria Women in Balance Kitchen Party Gala.
Blogger Shamim Mwasha (kushoto) a.k.a Zeze wa 8020 Fashions katika pozi na Mshehereshaji wa Women in Balance Kitchen Party Gala Gea Habib.
Mratibu wa Women in Balance Kitchen Party Gala Dina Marios (kushoto) na Mgeni wake kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai.(Picha zote na Zainul Mzige).

Harusi ya Mr. Martina Nkurlu na Rachel Sindbard

Harusi ya Mr. Martina Nkurlu na Rachel Sindbard 
Rangi: Paple, Nyeusi na Njano.

 Bwana Harusi Martina Nkurlu na Bi. Rachel Sindbard 
Wakiingia Kanisani kutimiza ahadi ya ndoa.

 Bwana Harusi Mr. Martina Nkurlu akiweka saini kwenye Shahada ya ndoa pembeni ni biharusi

Bwana  na Bibi Harusi wakiwa na nyuso za furaha baada ya kiapo cha ndoa


 Furaha ilioje kwa Mr.Martina Nkurlu na Bi. Rachel Sindbard




SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...