Sunday, September 27, 2015

Harusi ya Dickson Busagaga na Salome Mhozya

Dickson Busagaga (Blogger) na Salome Mhozya katika picha baada ya kufunga ndoa 
dickson busagaga & salome mhozya wedding (9)
Dickson Busagaga (Blogger) na Salome Mhozya katika picha baada ya kufunga ndoa iliyowafanya kuungana na kuwa mwili mmoja tukio lililofanyika katika kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto Yesu jimbo kuu la Tabora mnamo tarehe 23 Sep, 2015.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (8)
Waharusi (Dickson na Salome) wakionesha pete zao mara baada ya kuungana na kuwa kitu kimoja.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (2)
Hakika ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao, hata walipoingia ukumbini katika sherehe ya usiku walidhihirisha kuto kubahatisha kuungana kwao.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (3)
Furaha ilitawala sana miongoni mwao na waalikwa wote.
dickson busagaga & salome mhozya wedding (4) dickson busagaga & salome mhozya wedding (5) dickson busagaga & salome mhozya wedding (6)
MC Ndagula katika ubora wake wa kazi.

ZIFUATAZO NI PICHA ZA SENDOFF ILIYOFANYIKA TAREHE 19/09/2015 ORION

(TABORA HOTEL)

salome_mhozya_sendoff (1)
Picha ya pamoja ya maids, matron na aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa
salome_mhozya_sendoff (3)
Mrs Patrick na Salome (aliyekuwa bibi harusi mtarajiwa) wakiingia ukumbini
salome_mhozya_sendoff (4) salome_mhozya_sendoff (5) salome_mhozya_sendoff (6) salome_mhozya_sendoff (7) salome_mhozya_sendoff (8)
Wazazi wa Salome wakisalimia waalikwa katika sherehe za kumuaga mtoto wao Salome
salome_mhozya_sendoff (9) salome_mhozya_sendoff (10)
Wanakamati katika ubora wao wa kukabidhi zawadi za kamati
salome_mhozya_sendoff (11)
Dickson Busagaga, Mume halala wa Salome.
salome_mhozya_sendoff (12)
Bw. Patrick (Best man)
salome_mhozya_sendoff (13) salome_mhozya_sendoff (14) salome_mhozya_sendoff (15) salome_mhozya_sendoff (16) salome_mhozya_sendoff (17) salome_mhozya_sendoff (18) salome_mhozya_sendoff (19)
Picha na aloyson.com -TBN Tabora

Msanii 'Ray' na Anti Ezekiel Waibukia CCM


Mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (kulia) juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. 
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray akizungumza na wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. 
WanaCCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mikumi Morogoro .
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mikumi Morogoro. 
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (katikati) akijadiliana jambo la baadhi ya wasanii wenzake wanaoisapoti CCM katika kampeni zake.  
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray akipanda jukwaani kuwasalimia wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM.
Msanii Ray akishuka jukwaani baada ya kuzungumza na wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. 
Msanii Ray na Anti Ezekiel jukwaa kuu wakisalimiana na mgombea mwenza na viongozi wa CCM jukwaa kuu juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro.
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (katikati) akijadiliana jambo la baadhi ya wasanii wenzake wanaoisapoti CCM katika kampeni zake.  

Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie ma kada wa CCM waliojitolea kukinadi chama hicho wakiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za CCM.

MSANII maarufu wa uigizaji sinema nchini Vicent Kigosi au kwa jina maarufu Ray pamoja na mwenzake Anti Ezekiel wameanza rasmi kukinadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutangaza kuihama kambi ya upinzani (UKAWA) ambako awali walikuwa wakikipigia chapuo chama cha Chadema.

Ray ambaye juzi ameanza kupanda jukwaa la CCM akikiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika mikutano ya kampeni alisikika akisema awali alikuwa amepotea kuwa upinzani lakini sasa amestuka na kuamua kurudi nyumbani 'CCM' chama alichokiita makini chenye sera na ilani za kueleweka.

"...CCM oyeeeee, Mama Samia Suluhu oyeeeee...Magufuli oyeeeee, Mnenionaaaa...nimerudi nyumbani (CCM) kule (upinzani) nilikuwa nimepotea hivyo nimestukia mchezo na kurudi nyumbani," alisema Ray huku akishangilia na idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mikumi Mkoa wa Morogoro juzi.

Ray ambaye katika msafara huo aliambatana na msanii nyota na maarufu wa uigizaji nchini Anti Ezekiel pamoja na kundi la wasanii linalojulikana kama "Mama Ongea na Mwanao" ambalo linaiunga mkono CCM, walisema wataendelea kukiunga mkono chama hicho kwa kuwa kimefanya mengi kwa wananchi na wasanii kwa ujumla.

Katika mkutano huo wa kampeni uliohutubiwa na mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu aliwaomba wananchi wa Jimbo la Mikumi kuichagua CCM kwani ilani mpya ya uchaguzi imepanga kufanya mengi eneo hilo ikiwa ni pamoja na kukagua mashamba pori kuyapima na kuwagawia wananchi ili kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.

Alisema tayari kwa sasa kuna mashamba manne ambayo yamefutwa hati kwa wawekezaji na yatagawiwa kwa wananchi wa eneo husika, kwani awamu ya serikali ya tano ni kuhakikisha inamaliza na kukomesha migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji. Aliongeza kuwa kero ya maji itamalizika muda mfupi mara baada ya chama hicho kuingia madarakani kwani mradi wa husambazaji maji eneo hilo umekamilika kwa asilimia 80 kwa sasa mkandarasi anasubiri kiasi kidogo cha fedha toka serikalini ili kumalizia mradi huo.

Alisema serikali itakayoundwa na CCM imejipanga kukabiliana na suala zima la wanyama kuharibu mazao ya wakulima eneo hilo ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu ambapo itaijenga barabara ya Ludewa - Kilosa kwa kiwango cha lami na tayari shilingi bilioni 10 za ujenzi wa barabara hiyo zimetengwa.

Bi. Suluhu alisema uboreshaji maslahi ya wazee na wafanyakazi pia ni suala ambalo ilani mpya ya uchaguzi ya CCM imepanga kulifanyia kazi ili makundi hayo yaweze kuishi kwa kumudu changamoto za maisha.

Saturday, September 26, 2015

Viongozi wa CHADEMA Gairo, Mikumi Wakimbilia CCM, Bi. Suluhu Awapokea...!

Msafara wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan ukiwasili Gairo mkoani Morogoro.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akiwashukuru baadhi ya wananchi waliofika kumpokea mpakani mwa Mkoa wa Dodoma na Morogoro alipokuwa akiwasili kuanza ziara ya kampeni mkoani Morogoro leo.
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu (kushoto) akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Morogoro walipofika kupokea akitokea mkoani Dodoma. Mgombea huyo ameanza ziara ya kampeni Mkoa wa Morogoro leo.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili Mkoa wa Morogoro tayari kwa ziara ya kampeni.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
WanaCCM na wananchi wengine wakiwa katika mkutano wa kwanza wa mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Suluhu (hayupo pichani) katika Jimbo la Gairo.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akizungumza na wanaCCM na wananchi waliofika katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza nafasi ya urais wa CCM.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby (kulia) akizungumza jambo na mgombea mwenza wa nafasi ya urais CCM, Bi. Suluhu katika mkutano wa kampeni Gairo.
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu alipowasili katika mkutano mdogo wa kwanza kuinadi ilani ya CCM Jimbo la Gairo leo Morogoro.
Mbunge wa Afrika Mashariki, Angela Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika Jimbo la Gairo.
Baadhi ya vijana wakiwa wamepanda juu ya gari lililoegeswa ili kumuona mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
Aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wanachama wa CCM na wapenzi wa chama hicho wakimpokea mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu alipowasili katika Jimbo la Mvomero leo ambapo alifanya mkutano wa kampeni.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby akiwahutubia wanaCCM na wananchi wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mkutano wa mgombea mwenza wa CCM, alipokuwa akihutubia mkutano wa kampeni Gairo.
CCM Oyeeeeeeee....! Mkutano Jimboni Gairo.
Baadhi ya viongozi wa CCM (kulia) wakimpa zawadi ya sare kada mkogwe wa CCM Jimbo la Gairo.

Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.
Wakereketwa na wanaCCM wakimpokea mgombea mwenza wa CCM Jimbo la Gairo.

Mmoja wa viongozi na makada wa Chadema wilaya ya Gairo (kushoto) akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Bi. Samia Suluhu. 
Katibu wa Chadema Wilaya ya Gairo, Yona Senyagwa (kushoto) akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katibu huyo pamoja na makada wenzake wametangaza kukihama chama cha Chadema na kujiunga na CCM leo.
Bi. Samia Suluhu akiwa amesimamishwa na wananchi njiani alipokuwa akielekea Wilayani Kilosa kufanya mikutano ya kampeni.
Kada mkongwe wa Chadema Kata ya Dumila, Tegemea Mnhambo akitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais, Bi. Suluhu.
WanaCCM na wananchi wakifuatilia mkutano wa kampeni juu ya gari lililoegeshwa.
Wananchi na wapenzi wa CCM wakiwa wamemsimamisha mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu.
WanaCCM na Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM.
Wakitumia mbinu mbadala kumlaki mgombea mwenza wa CCM
Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Inspecta Harun akihamasisha wanaCCM na wananchi mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.  
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akisalimia wananchi.
Mgombea mwenza Bi. Suluhu akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi. 
Mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi akionesha kadi yake kabla ya kumkabidhi mgombea mwenza.

Mgombea mwenza Bi. Suluhu akimkabidhi kadi mmoja wa makada wa Chadema waliojiunga na CCM, katika mkutano wa kampeni Jimbo la Mikumi.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...