Saturday, January 14, 2012

Harusi ya Amani Adam na Felister Kiungulia


Bi. Felister Kiungulia (kulia) akiwa na mumewe Amani Adam kwenye hafla ya utambulisho wa mumewe katika ukoo na familia ya Mzee Kiungulila Lushoto mkoani Tanga. Ndoa ya maharusi hawa ilifanyika mwishoni mwa mwaka jana mkoani Arusha.


Bi. Felister Kiungulia akiwa na mumewe Amani Adam

Bi. Felister

Bw. Adam


Kutoka kushoto ni Mzee Kiungilia akiwa na mkewe kwenye hafla ya kutambulishwa mkwe wao Amani Adam iliyofanyika nyumbani kwa Kiungulia Soni Lushoto Desemba 31, 2011.


Ndugu jamaa, majirani na marafiki wa Mzee Kiungulia wakitambulishwa kwa mumewe Felister katika hafla hiyo, wa pili kulia ni kaka mkubwa wa Felister Henry Kiungulia, wa kwanza kulia kwake ni mkewe Grace Mushi Kiungulia.  Picha kwa hisani ya wanafamilia.

Harusi ya Bw. Joseph na Bi. Sylvia



Joseph akiwa na Mkewe Sylvia baada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa la St. Joseph Jumamosi ya Novemba 26, 2011 jijini Dar es Salaam na baadaye kufuatiwa na hafla kabambe iliyofanyika katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Maharusi Joseph na Sylvia wakigongesha glasi zenye mvinyo kwa ishara ya upendo kabla ya kunyweshana katika hafla yao iliyofanyika katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Joseph akiwa na Mkewe Sylvia wakipiga picha za kumbukumbu ya tukio lao na ndugu jamaa na marafiki katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo'


Joseph na Mkewe Sylvia wakiwapungia mkono wageni waalikwa katika hafla yao huku wakiondoka katika Ukumbi wa 'Brigade Mess-Lugalo' baada ya hafla yao. Picha zote kwa hisani ya Harusini Blog.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...