Thursday, December 28, 2017

KAMANDA WA POLISI MKOA WA SINGIDA ASHIRIKI IBADA KULIOMBEA TAIFA...!

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo(hawapo pichani) kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba( wa tano kulia) akifuatilia kwa makini mahubiri wakati wa Ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida jana  wengine pichani ni viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo  Mkoa wa Singida.

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waumini wa Kikristo kwenye ibada maalum ya kuliombea Taifa iliyoandaliwa na Umoja wa Makanisa Mkoa wa Singida ambapo alisisitiza umuhimu wa wananchi kutii Sheria za nchi bila shuruti.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Deborah Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari namna Jeshi la Polisi lilivyojipanga kuimarisha ulinzi katika nyumba za ibada na kumbi za starehe katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismas na Mwaka Mpya.

Monday, December 25, 2017

Waziri wa Rais Magufuli asherehekea sikukuu ya Krismas shambani

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.  Luhaga Mpina akishiriki kusafisha shamba lake la mpunga lililoko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro alipokuwa kwenye wa mapumziko ya sikukuu ya  Krismas leo.

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akishirikiana na wafanyakazi wake kusafisha shamba lake liliko Kijiji cha Dalla mkoani Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga leo wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas.

Moja ya matrekta yaliyoko katika shamba la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina yakiendelea na shughuli za kulima kwa ajili ya maandalizi ya kupanda mpunga wakati Waziri huyo (hayupo pichani) alipokwenda kushiriki shughuli za shamba wakati wa mapumziko ya sikukuu ya Krismas leo.(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

Sunday, December 24, 2017

JUMUIYA YA WAZAZI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM, WAMPOKEA KWA KISHINDO MWENYEKITI WA TAIFA WA JUMUIYA HIYO DK. EDMUND MNDOLWA


 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akisalimia baadhi wa wana CCM waliofurika katika ukumbi wa Tawi la CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, ambao walifika kumlaki katika mapokezi yaliyoandaliwa na Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam, jana.


 Gari la Dk. Mndolwa likiwasili lango Kuu la Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mapokezi hayo.

 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar  Abdallah Haj Haidar akimpokea Dk Mndolwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Dar es Salaam,

 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo.

 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Saad Kusilawe, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo.

 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisalimiana na  Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Lugano Mwafongo, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo.

 Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk Edmund Mndolwa, akisilindikizwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba kwenda kusaini vitabu wa wageni na kuzungumza na uongozi, alipowasili Ofisi ya CCM mkoa huo.



 Dk. Mndolwa akisaini kitabu wa wageni katika Ofisi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alipowasili. Kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa huo, Frank Kalokola Kamngisha.



 Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Abdallah Haj Haidar akisaini kitabu cha wageni, huku Dk. Mndolwa akiendelea kufanya hivyo pia.



 Abdallah Haj Haidar akisalimia.


 Mama Patricia Rukia Mndolwa akisalimia.


 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Bara Burhan Rutta akisalimia.


 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Kusilawe akisalimia.

 Kalokola akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, amkaribishe Dk. Mndolwa kuzungumza na Uongozi.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba alizungumza kabla ya kumkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza.

 Kate Kamba akimkaribisha Dk Mndolwa kuzungumza na uongozi
 Dk. Mndolwa akizungumza na Uongozi



 Gari lilobeba Dk Mndolwa likiwasili kwenye Viwanja vya Ofisi ya Tawi la CCM Mwinjuma.

 Kijana wa CCM akimvisha Skafu Dk. Mndolwa baada ya kuwasili CCM Mwinjuma.

 Dk. Mndolwa akipokea kwa ukakamavu saluti ya kijana wa CCM baada ya kuvishwa skafu.

 Dk Mndolwa akiongozana na baadhi ya viongozi kwenda eneo la tukio.

 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya wana CCM wakati akienda ukumbini.

 Dk Mndolwa akisalimia baadhi ya viongozi wakati akienda ukumbini.

 TOT wakitumbuiza kumlaki ukumbini Dk. Mndolwa.

 Dk. Mndolwa akienda meza kuu.

 Dk. Mndolwa na Makamu wake- zanzibar wakiwa tayari meza kuu.

 Viongozi wa meza kuu wakiungana na Dk Mndolwa kushangilia baada ya kuwasili eneo hilo.

 Mmoja wa viongozi katika Baraza la Wazee wa jumuiya ya Wazazi Mzee Mkali akisalimia.

 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Ndugu Mwafongo akifanya utambulisho wa viongozi ndazi ya mkoa.

 Viongozi ndazi ya mkoa wakisalimia baada ya kutambulishwa.

 Baadhi ya viongozi waliohudhuria mapokezi hayo wakiwa ukumbini.

 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuia ya wazazi Tanzania Ndugu Rutta akitambulisha viongozi ngazi ya taifa.

 Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi tanzania Seif Shaban Mohammed akifafanua maana na umuhimu wa neno 'Mapinduzi'  baada ya kutambulishwa.

 Ndugu Mwafongo akiendeleza ratiba.

 Mwenyekiti wa CCM Temeke ndugu Almish akizungumza baada ya kutambulishwa.

 Ndugu Kalokola akizungumza kumtambulisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Haj.

 Kakamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania-Zanzibar Ndugu Hajj akizungumza.

 Shabiki wa CCM akimuombea maisha marefu na uongozi bora Dk. Mndolwa tukio ambalo lilikuwa la ghafla.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Sylivia Magdalena Kamba akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Mndolwa kuzungumza na hadhara.


 Omar Kimbau aliyewahi kuhamia CUF akitangaza kurudi CCM mbele ya Dk. Mndolwa.

 Dk. Mndolwa akimpongeza Kimbau kwa kuzinduka na kurejea CCM.

 Dk. Mndolwa akihutubia kweye mapokezi hayo. 
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

Saturday, December 23, 2017

TTCL yatoa zawadi za Chrismas na Mwaka Mpya kwa vituo vya yatima na wazee

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi mbuzi Mchungaji wa Kanisa la EAG, Dennis Shija (wa tatu kulia) ambaye ni msimamizi wa Kituo cha wa Toto na Wazee wasiojiweza Mbagala Kuu ikiwa ni sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wazee.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri w. Kindamba, mwakilishi wa Kituo cha 'Green Pastures Orphanage' cha Mapinga Bagamoyo, Restiel Natai (wa tatu kulia) sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vyote vya jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kushoto) akimkabidhi kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri w. Kindamba, mmoja wa watoto wa Kituo cha 'Green Pastures Orphanage' cha Mapinga Bagamoyo, Restiel Natai (wa tatu kulia) sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vyote vya jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri w. Kindamba, mwakilishi wa Kituo cha 'Green Pastures Orphanage' cha Mapinga Bagamoyo, Restiel Natai (wa tatu kulia) sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa vituo vitatu vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vyote vya jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kamati ya Kuhudumia Wasiojiweza kutoka vituo vya Bethel Center Mbagala Kuu Dar es Salaam, Neema Uronu (kulia) sehemu ya msaada uliotolewa na TTCL kwa vituo vitatu vya watoto yatima.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Mushi (wa pili kulia) akikabidhi mbuzi kwa wawakilishi kutoka vituo vya Bethel Center na Kituo cha Wazee wasiojiweza cha Bethel cha Mbagala Kuu vyote vya jijini Dar es Salaam.

KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imekabidhi bidhaa mbalimbali za vyakula kwa vituo vitatu vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wazee wasiojiweza vyote vya jijini Dar es Salaam, ikiwa ni zawadi ya Siku Kuu za Chrismas na mwaka mpya kwa makundi hayo.

Akikabidhi msaada huo leo Makao Makuu ya Ofisi za TTCL Dar es Salaam kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri w. Kindamba, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Nicodemas Thomas Mushi alisema vituo vilivyopokea msaada huo ni pamoja na 'Green Pastures Orphanage' Mapinga-Bagamoyo, Kituo cha Bethel Center Mbagala na Kituo cha Wazee wasiojiweza cha Bethel cha Mbagala Kuu vyote vya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kugawa msaada huo, Mushi alisema huo ni utaratibu wa kawaida wa kampuni ya TTCL kutoa msaada kwa jamii hasa kwa makundi ya watu wasiojiweza ili yaweze kujumuika na Watanzania wengine katika kusheherekea siku kuu za Chrismas na Mwaka Mpya kwa makundi hayo yanayokabiliwa na changamoto anuai.

"Huu ni utaratibu wa kawaida wa kampuni yetu kila mara hali ya uchumi inaporuhusu huwa tunayakumbuka makundi yenye mahitaji maalum na nikupitia ule utaratibu wetu wa kawaida wa kurejesha sehemu kidogo ya faida yetu kwa jamii, tumechangua makundi haya baada ya kupitia maombi yao na kujiridhisha wana vigezo vya kusaidiwa kutokana na walivyojieleza changamoto walizo nazo," alisema kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo.

Alisema kuwa kampuni ya TTCL itaendelea kuyakumbuka makundi hayo maalum na kuyasaidia kwa chochote kadri inavyokuwa na uwezo wa kufanya hivyo, huku akishauri taasisi zingine na watu wanaojiweza kusaidia pale wanapokuwa na uwezo wa kufanya hivyo kwa wasiojiweza. "...Natoa wito pia kwa makampuni, taasisi na watu wengine wenye uwezo kuunga mkono juhudi hizi za kusaidia makundi ya wasiojiweza ili yaweze kufarijika kwa namna moja ama nyingine," alisema.

Aidha alibainisha bidhaa zilizokabidhiwa ni pamoja na mbuzi watatu, mchele kilo 300, mafuta ya kula ndoo 9, maharage kilo 300, Sukari kilo 150, Unga kilo 300, juisi, maji, soda na aina mbalimbali ya mafuta ya kujipaka na sabuni vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.

Mchungaji wa Kanisa la EAG, Dennis Shija ambaye ni msimamizi wa Kituo cha wa Toto na Wazee wasiojiweza Mbagala Kuu alimshukuru Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Bw. Kindamba kwa msaada walioutoa katika vituo hivyo na kumuhakikishia watautumia kama ulivyo kusudia.

Aliongeza kuwa makundi hayo yanakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo wanapata faraja kampuni kama TTCL kujitokeza kujitokeza kuwasaidia. "...Sisi tunashukuru sana kwa msaada tuliopokea leo kwa ajili ya maandalizi ya siku kuu za mwisho wa mwaka huu, hii sio mara ya kwanza kusaidiwa na TTCL naomba kuwahakikishia msaada huu utatumika kama ulivyokusudiwa," alisema mchungaji huyo.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Kituo cha 'Green Pastures Orphanage' cha Mapinga Bagamoyo, Restiel Natai aliishukuru kampuni ya TTCL kwa kuamua kuwakumbuka watu wasiojiweza ili waweze kusherekea kwa furaha siku kuu hizi za mwisho wa mwaka. Pamoja na hayo alitoa wito makampuni na taasisi nyingine kujitokeza kuwasaidia makundi kama hayo kwani nayo yanaitaji faraja hasa kipindi kama hiki ambapo familia zinakutana na kusherehekea pamoja.

Hata hivyo, alitoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiunga mkono kampuni ya kizalendo ya TTCL ambayo sasa imefanya mageuzi makubwa kihuduma kwa kutumia huduma zake mbalimbali za mawasiliano kama huduma za intaneti, simu za mkononi na mezani na vifaa vya mawasiliano anuai kufurahia huduma bora zenye bei nafuu.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...