Tuesday, January 31, 2017

Wabunge wa uzazi salama wataka bajeti ya afya ya uzazi na mtoto kuboreshwa

Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama Mh. Jenista Mhagama (katikati) akifungua mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salama.


Meneja Mradi wa Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ), Bi. Sizarina Hamisi (mbele) akiwasilisha mada katika mkutano kati ya WRATZ na kundi la Wabunge wa uzazi salama mjini Dodoma.


Mkutano kati ya Muungano wa Utepe Mweupe (WRATZ) na Wabunge wa uzazi salama ukiendelea.

WABUNGE wa kundi la uzazi salama wametakiwa kuhamasisha na kutetea Bajeti ya Afya ya Uzazi na Mtoto ili ipewe kipaumbele katika mipango ya Halmashauri kwa mwaka 2017/2018. 

Hamasa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kundi la Wabunge wa Uzazi Salama, Mh. Jenista Mhagama wakati akifungua mkutano uliowakutanisha wabunge wa kundi hilo wapatao 30 pamoja na Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) mjini Dodoma kujadili kuhusu mchango wa wabunge katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

 Akiwasilisha mada katika mkutano huo Meneja mradi wa Muungano wa Utepe mweupe (WRATZ) Bi Sizarina Hamisi alisema kwa mujibu wa takwimu ya Idadi ya Watu na Afya Tanzania ya mwaka 2015-2016 zinaonyesha kuwa kwa sasa wakina mama 30 na watoto wachanga 180 wanapoteza maisha kila siku kutokana na matatizo yatokanayo na uzazi. 

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wamekiri kuwa pamoja na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali bado vifo vya mama na mtoto vitokanavyo na uzazi ni changamoto hivyo kuna haja yakuongeza jitihada ili kutatua tatizo hilo ikiwemo bajeti ya afya ya mama na mtoto hasa huduma za muhimu na dharura kupewa kipaumbele kuanzia ngazi za halmashauri mpaka serikali kuu.

Viongozi Wanawake Watakiwa Kuwaandaa Viongozi Bora wa Baadaye...









Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi, akimpongeza Anna Abdalah


Na Richard Mwaikenda


MJUMBE wa Bodi mpya ya Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Anna Abdalah, amewataka viongozi Wanawake kukutana na Wasichana kuwapiga msasa wa kuwaaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye. Anna Abdalah ambaye amekuwa kiongozi wa muda mrefu nchini, aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya TGGA, Mikocheni Dar es Salaam juzi.

Alisema ana mpango wa kuwaalika viongozi mbalimbali Wanawake akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akutane na Wasichana wanachama wa TGGA wawafundishe maadili ya uongozi kwa lengo la kuwaandaa kuwa viongozi bora wa baadaye.

Anna Abdalla alisema kuwa hata yeye na Zakia Meghji pamoja na baadhi ya viongozi wengine wanawake walioshika nyadhifa mbalimbali nchini, enzi za usichana wao walipitia kwenye chama hicho na kulelewa vizuri.

Pia katika kikao kijacho cha Bunge, anatarajia kukutana na Wabunge Wanawake na kuwaeleza umuhimu wamara kwa mara kukutana na wasichana kuwafundisha kwa kuwapa hamasa uongozi ili nao wawe kuwa wabunge na hata miongoni mwao kuwa Spika na mawaziri.

"Nataka siku za usoni,tuwaalike viongozi mbalimbali akiwemo, Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika wa Bunge, Wabunge na Mawaziri Wanawake ili mje mjumuike nao pamoja, mjifunze mambo mbalimbali ya uongozi na mhamasike, ili siku moja nanyi mje kuwa kama, Samia, Kamishna, Spika wa Bunge, Wabunge na hata uwaziri pia" alisema Anna Abdalah, huku akipigia makofi na waalikwa katika hafla hiyo.

Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Jaji mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Engera Kileo, ilihudhuriwa na wanachama wa chama hicho, wakiwemo pia wasichana watatu waliotoka Rwanda, Uganda na Madagasca waliokuwepo nchini katika mafunzo ya uongozi, maadili na utamaduni. Wasichana hao ni; Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), Recheal Baganyire (Uganda) na Andriambolamanana Vahatrimama.


Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi, aliwataja Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni; Zakia Meghji, Anna Abdalah, Grace Makenya, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema na Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Tunu Pinda. Mwenyekiti wa Bodi hiyo atateuliwa miongoni mwao.




Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Girl Guides Association (TGGA), Profesa Martha Qorro (kushoto), akimpongeza Mjumbe wa Bodi ya Udhamini wa TGGA, Anna Abdalah wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo, Mikocheni Dar es Salaam juzi. 




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya TGGA, Sophia Mjema (aliyekaa kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wanachama wa TGGA wakati wa hafla hiyo. Aliyekaa kushoto ni Mariamu Kimbisa ambaye ni Kamishna wa Kimataifa wa TGGA. Wa tatu kulia waliosimama ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.




Wasichana Michelline Uwiringiyimana (Rwanda), kulia, Recheal Baganyire (Uganda), katikati, na Andriambolamanana Vahatrimama wa Madagascar ambao wapo nchini katika programu ya mafunzo ya kubadilishana uzoefu katika masuala ya utamaduni, uongozi na maadili.wakiwa katika hafla hiyo.




Wakipiga makofu baada ya kufurahishwa na hotuba ya Anna Abdalah









Anna Abdalah akihutubia katika hafla hiyo




Mmoja wa wabia wa moja kati ya majengo ya TGGA, akisalimiana na Anna Abdalah




Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shebe akitoa shukrani kwa wajumbe wapya wa bodi na wageni waalikwa kwa kuhudhuria uzinduzi huo.




Wajumbe wa Bodi wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA pamoja na wanachama wa chama hicho.




Sasa ni wakati wa msosi
























Wajumbe wa Bodi wakijadiliana jambo na watendaji wa TGGA



Profesa Qooro akimuaga Zakia Meghji. Katikati ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Hangi.




Qooro akigana na Anna Abdalah. Kushoto ni Hangi. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA)

Azam Marine Kusafirisha Abiria Tanga - Unguja na Pemba kwa Meli Kubwa ya Kisasa



Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria na mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine ili kuwanusuru wananchi wa mkoa wa Tanga na changamoto za usafiri huo







Meli Kubwa inayoweza kuingia abiria 1600 na magari hamsini yenye mizigo kwa pamoja ambayo itafanya safari zake kati ya Tanga-Unguja na Pemba ikiwa inaingia bandari ya Tanga leo wakati wa uzinduzi wake ambapo uwekezaji huo mkubwa umefanywa na kampuni ya Azam Marine




Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed wa pili kulia akitazama namna wananchi wanavyoshuka kwenye meli hiyo itakayopunguza adha na usumbufu kwa wananchi wanaosafiri kutoka mkoani Tanga kwenda Unguja na Pemba




Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed katikati akizungumza na watumishi wa mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga wakati wa ujio wa meli hiyo kwenye bandari ya Tanga kulia ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Tryphoni Ntipi kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo,Moni Jarufu.




Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed katikati akisalimiana na Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Tryphoni Ntipi wakati wa ujio wa meli hiyo kushoto ni PRO wa Mamlaka hiyo, Moni Jarufu.




Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa meli hiyo kulia Mkurugenzi Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini (SUMATRA) Kaptain Mussa Mandia.



Mkurugenzi Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya majini (SUMATRA) Kaptain Mussa Mandia katikati akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni Meneja Mkuu wa Azam Marine Husein Mohammed.




Waandishi wa Habari wakiwa kazini kushoto ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania katikati ni Mariam Shedafa wa Azam TV.
 



Vifaa vya uokozi wakati wa majanga ya ajali hivyo.




Baadhi ya Sehemu ya VIP ndani ya Meli hiyo kama inavyoonekana












Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii, Tanga Raha

Halmashauri ya Monduli na Kashfa ya Ugawaji Ardhi, Wananchi Waja Juu

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akionyesha baadhi ya hati ambazo alipatiwa na halmashari kwa ajili ya kumtambulisha kuwa kiwanja ni chake sasa hivi kiwancha hicho kinataka kunyang’anywa na halmashauri ya Wilaya ya Monduli.




wananchi wakiwa wamesimama na mabango yaonayoonyesha unyanyasaji wanao fanyiwa na halmashauri hiyo





wamama wa kijiji cha Lendikinya wakiwa wamekaa kwa huzuni katika mkutano wa hadhara






MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikiny






Mwana kijiji Amina Longitoti akiwa anatoa kero yake katika mkutano huo


Habari/Picha na Woinde Shizza, Arusha

BADDHI ya wananchi wa wilaya ya Monduli wameitupia lawama halmashauri ya wilaya hiyo na kusema kuwa inachochea migogoro ya ardhi na kuwanyima baadhi ya wananchi amani ya kukaa katika vijiji vyao

Hayo wamesema jana wakati walipokuwa wakifanya mkutano wa adhara uliofanyika katika kijiji cha Lendikinya kilichopo ndaniya halmashauri ya Monduli mkutano ambao uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo,ambapo walisema kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na uongozi huu mpya wa halmashauri ambao unaongozwa na chadema kwani katika kipindi kilichopita walikuwa hawanyanyaswi wala awafukuzwi katika maeneo yao ambayo walikuwa wanaishi tangu enzi za mababu zao.

Mmoja wawananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Songoyo Ole Matata alisema kuwa uongozi wa halmashauri hiyo umekuwa ukiwasumbua na kuwafukuza katika maeneo hayo ambayo ,walikaa tangu enzi za mababu wao,huku akibainisha kuwa pamoja na kuwa wanafukuzwa lakini sio wananchi wote bali uongozi huo unafukuza wananchi kulingana na chama ambacho anatokea.

“Tumekuja apa siku nyingi lakini tunashangazwa hatujawai kufukuzwa ila tangu halmashauri hii ichukuliwe na chadema tumekuwa tunanyanyaswa sana haswa sisi tunaotoka na tunajilikana ni wanachama wa chama cha mapinduzi,nasema hivyo kwa sababu hata sisi tunaolalamika ambao tumeambiwa tumevamia msitu ni wanachama wa CCM hamna mwanachama hata mmoja wa CHADEMA ambaye amefatwa akaambiwa amevamia msitu ,mimi mwenyewe pembeni yangu nimepakana na aliyekuwa waziri mkuu mstaafu Edward Lowasa katika maeneo hay o hayo kunashamba la Askofu Laizer lakini hao hawajaambiwa wamevamia misitu waondoke ila sisi ambao ni wanachama wa CCM ndio tunaambiwa tumevamia msitu kwakweli hii sio haki kabisa tunamuomba Rais wetu magufuli aje atusaidie maana tunanyanyaswa sana”alisema Amina Longitoti

Akiogea katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare alisema kuwa halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama chao hakitakaa kimya kwa hilo.

Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi hivyo anashangazwa na kusikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria.

Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi na hatakuwa tayari kuona wananchi wananyanyaswa kwa sababu ya maslayi ya mtu binafsi.

“mimi nilipata shamba hilo kama mwananchi wa kijiji hicho na sikuchukuwa shamba hilo kama kiongozi wa CCM hivyo nashangaa sana kwa kitendo cha kuingiza chama katika mambo yangu binafsi kimenisikitisha sana na kwakweli sita vumilia kabisa na kingine kinachonishangaza sio mimi tu au sisi tu ndio tunamashamba au tunamiliki ardhi katika kijiji hichi kwani hata Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa (Waziri Mkuu mstaafu) ana ekari za kutosha katika eneo hili pamoja na diwani wa Monduli Juu na wengine walioko ndani ya Chadema lakini nashangaa wote amna aliyeambawa amevamia ila ni sisi tu," alisema Sanare.

Kwa upande mwananchi mungine aliyejitambulisha kwa jina la Olais Taiyai alisema kuwa ubaguzi na uchochezi uliopo ndani ya halmashauri hiyo unapaswa kupigwa vita na hautavumilika hata kidogo kwani sio jambo jema linalofanywa na viongozi hao na kuomba serikali kuingilia kati swala hili kwani wananchi hao wanateseka na hawana pa kwenda iwapo wataendelea kufukuzwa katika viwanja vyao

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Monduli, Amani Ole Silanga, aliwataka wanakijiji kuwa na subira, kwani huo ni upepo mchafu unaovuma kupitia. Hivi karibuni Baraza la madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Monduli, lilipitisha azimio la kuchukua ardhi ya kijiji hicho kwa madai kuwa waliochukua ardhi hiyo hawakufuata sheria, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo.

Saturday, January 28, 2017

SHINDANO KUMSAKA MLIMBWENDE MISS KIBOSHO 2017

Shindano la kumsaka mlimbwende wa MISS KIBOSHO 2017 Jijini Mwanza limeanza katika viunga vya Kibosho Luxury Bar iliyopo Kiseke Ilemela Jijini Mwanza ambapo wanyange 10 wanawania nafasi hiyo.

Wanyange hao kama wanavyoonekana pichani ni Caren Nestory, Dorice Ezra, Jullieth Michael, Elizabeth Faustine, Christina Lucas, Nasra Ramadhan, Jacline Moses, Denzry Michael, Kephlin Jacob na Aida Gazar.

Shindano hilo limeandaliwa na Raj Entertainment kwa udhamini wa Kibosho Luxury Bar, Wema Salon na Ngenda Salon huku likiwa limelenga kukuza sanaa ya ulimbwende kuanzia za mitaa hadi kitaifa.



Wanyange wa shindano la Miss Kibosho 2017 wakionesha makeke yao jukwaani
Washereheshaji wakimtambulisha Matron wa Miss Kibosho 2017, Fania Hassan (katikati) ambaye alikuwa Miss Utalii nchini mwaka 2006.
Kila mlimbwende alionesha makeke ya hali ya juu hadi kuwapa wakati mgumu majaji. Kumbuka majaji ni Leonald Kaduguda (kushoto), Mama Ngenda Lutalo (katikati) na Mwl.Tatu Ngelengela (kulia).
Umakini katika kufuatilia kinyang'anyiro cha Miss Kibosho 2017
Majaji wakiahilisha shindano la Miss Kibosho 2017 usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Leonald Kaduguda, Mama Ngenda Lutalo (kulia) na Mwl.Tatu Ngelengela (katikati). Fainali itafanyika leo jioni kuanzia majira ya saa moja kamili.

Wednesday, January 25, 2017

Wasanii 400 wa Afrika kutikisa tamasha la Sauti za Busara 2017 Zanzibar

Mkurugenzi wa tamasha la Sauti za Busara Bw.Yusuf Mahmoud akionesho moja ya kitabu chenye mambo lukuki yahuso tamasha hilo pamoja la habari mbalimbali za wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo la aina yake kwa wakazi wa Zanzibar na wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali za nchi na nje.

Mwanamuziki mkongwe mwenye makazi yake ya kimuziki nchini Japan Fresh Jumbe akizungumza na waandishi wa habari mapema kuhusu ushirika wake pamoja na bendi yake nzima katika tamasha la sauti za busara.

Mwenyekiti wa Tamasha la  Sauti za Busara Bw. Simai M. Said wa pili kutoka kushoto akiwa anaongea na waandishi wa habari juu ya Tamasha la 14 la sauti za busara.

Mkurugenzi wa Tamasha la 14 la Sauti za Busara, Bw. Yusuf Mahmoud (wa pili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam huku akitaja baadhi ya wanamuziki ambao watatumbuiza 'Live' katika Tamasha hilo. 


JUMLA ya wasanii 400 wa Ki-Afrika toka takribani makundi 40 wanatarajia kutumbuiza katika Tamasha la Sauti za Busara 2017. Tamasha hilo litakaloanza kufanyika tarehe 9-12 ya mwezi Februari 2017 litafanyika Mji Mkongwe, Zanzibar.

Akizungumza Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Bw. Yusuf Mahmoud alisema Tamasha litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morrocco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha.

Muziki unalateta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali. Duniani na ujumbe mkubwa kwa Dunia ni kuwa muziki unakuza umoja na urafiki hata kwenye mipaka ya sehemu mbalimbali. Alisema Tamasha la 14 la Sauti za Busara kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa tamasha hilo, lenye kauli mbiu ya ‘AfricaUnited’ mwaka huu tamasha litakua na majukwaa matatu yatakayotumiwa na wasanii wote kimataifa/nyumbani.

Watu mbali mbali wenye rangi tofauti, umri tofauti kwa mara nyingine tena wataunganishwa na tamasha kusheherekea muziki wa ki-Afrika. Matarajio ya mahudhurio ni makubwa kutoka Tanzania na nje ya Nchi kufatia kujaa kwa sehemu za malazi Mji Mkongwe kwa wiki ya tamasha. Wasanii wote watatumbuiza ‘live’ muziki wa Ki-Afrika kila siku kuanzia saa 10:30 jioni mpaka saa 7:00 usiku.

Lengo la tamasha ni kuhakikisha kila mmoja anamudu kiingilio hivyo kwa watanzania ni Sh 6,000 kwa siku na Sh20,000 kwa siku nne za tamasha. Tamasha hili ambalo kwa asilimia 100 huwa live kitu ambacho kinalifanya tamasha hili liwe la kipekee huwapakipaumbele wanamuziki chipukizi kutambulisha kazi zao zenye kutambulisha uhalisia wa utamaduni.

 Tamasha la Sauti za Busara hukutanisha wataalamu wa muziki wa kimataifa na kutoa nafasi kw amuziki wa Afrika Mashariki kufwakifikia watu mbalimbali dunia nzima kupitia jukwaa la Sauti za wanamuziki wa nyumbani amabao hutumbuiza tamashani hupata mialiko kushiriki matamasha mbali mbali Barani Ulaya na Afrika. 

"...Ndani ya siku hizo nne jumla ya wasanii 400 wa ki-Afrika (makundi 40) yatatumbuiza tamasha Sauti za Busara 2017. Tamasha litaanza na gwaride kutoka maeneo ya Kisonge (karibu na Michenzani) kuanzia saa 9:00 jioni Alhamis tarehe 9/2. Tamasha litakutanisha wanamuziki kutoka sehemu mbali mbali ambapo wanamuziki wa Tanzania watashirikiana na wa Morrocco, kutakua na mwanya wa kufahamiana zaidi kupitia vikao vya Movers and Shakers, na hafla itakayofanyika usiku wa wapendanao baada ya tamasha. Muziki unalateta watu pamoja kutoka sehemu mbalimbali. Duniani na ujumbe mkubwa kwa Dunia ni kuwa muziki unakuza umoja na urafiki hata kwenye mipaka ya sehemu mbalimbali," alisema Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara, Bw.Yusuf Mahmoud.

 Kati ya makundi 40 nusu yanatoka Tanzania. Makundi hayo ni Afrijam Band, CAC Fusion, Chibite Zawose Family, Cocodo African Music Band, Jagwa Music, Matona's G Clef Band, Mswanu Gogo Vibes, Rajab Suleiman & Kithara, Tausi Women's Taarab, Usambara Sanaa Group, Wahapahapa Band, Ze Spirits Band.

Tuna hakika makundi kama haya yatawakilisha vema matamasha ya nje endapo yatapata nafasi, Makundi mengine ni pamoja na Batimbo Percussion Magique (Burundi), Bob Maghrib (Morocco), Buganda Music Ensemble (Uganda), Grace Barbe (Seychelles), H_art the Band (Kenya), Imena Cultural Troupe (Rwanda), Isau Meneses (Mozambique), Karyna Gomes (Guine Bissau), Kyekyeku (Ghana), Loryzine (Reunion), Madalitso Band (Malawi), Pat Thomas & Kwashibu Area Band (Ghana), Rocky Dawuni (Ghana), Roland Tchakounté (Cameroon), Sahra Halgan Trio (Somaliland), Sami Dan and Zewd Band (Ethiopia), Sarabi (Kenya), Simba & Milton Gulli (Mozambique).

 Shukrani zetu za dhati na za kipekee tunazifikisha kwa Hotel ya Golden Tulip kwa kuhakikisha kikao hiki kinafanikiwa. Pia tunawashukuru ninyi wote mliohundhuria kikao hiki na kuhakikisha mnafikisha taarifa zetu kwa wananchi. Wadhamini wa tamasha hili ni pamoja na Africalia, Chuchu FM Radio, Zanlink and Coastal Aviation Embassy of Germany, Ethiopian Airlines, Ikala Zanzibar Stone Town Lodge, Memories of Zanzibar, Mozeti, Music In Africa, Norwegian Embassy, Pro Helvetia, Swiss Agency for Development & Cooperation (SDC), Tifu TV, na wengine wengi.

 Kwa mawasiliano zaidi tembelea tovuti yetu www.busaramusic.org.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...