Sunday, October 16, 2011

Harusi ya Lucas Songoma na Raeli Moses


Maharusi Lucas Songoma (kushoto) na mkewe Raeli Moses (kulia) wakishirikiana kuweka saini cheti cha ndoa yao mara baada ya kufunga pingu za maisha katika Kanisa Katoliki la Mt. Yosef Jimbo Kuu la Dar es Salaam Oktoba 15, 2011. 


Paroko wa Parokia ya St. Josef (kushoto) akiwaongoza maharusi Lucas na Raeli kusaini vyeti vya ndoa yao kanisani mara baada ya kufunga ndoa.


Lucus akimvisha pete mkewe Raeli kanisani ikiwa ni ishara ya kuungana katika maisha mapya ya ndoa yao.


Flowers wa maharusi wakiwa katika pozi. "Cheki pozi letu, mnaonaje!"


Mama mkubwa wa Bwana Harusi, Mektilda Lutabana (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja nje ya kanisa na ndugu wa karibu wa maharusi.


Flowers girls wakiwa kwenye pozi la pamoja. "Tumependeza!"


Maharusi Lucus na Raeli katikati wakiwa na wapambe wao, wakati wa hafla yao kambambe iliyofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi (City Centre) Dar es Salaam. (Picha zote kwa hisani ya familia ya maharusi)

Thursday, October 13, 2011

Harusi ya Roman na mkewe Dorotea


Maharusi Roman na mkewe Dorotea wakiangaliana na kupeana tabasamu la kupongezana kwa hatua waliofikia. Inapendeza sana!


Maharusi wakilishana kwa staili ya pekee tunda kwa ishara ya upendo ndani ya ndoa yao. Hafla kabambe ya harusi hiyo iliyofanyika Septemba 24, 2011 jijini Dar es Salaam.


Hapa ndipo mahali maharusi na waheshimiwa hawa walipumzika wakisherehekea hafla yao ndani ya Ukumbi wa Royal Skyline. Blog ya Harusi na Matukio inawapongeza maharusi hawa kwa hatua hiyo.


"Pokeeni zawadi hii kubwa ambayo tumewaandalieni ili muendelee kufurahia maisha ya ndoa yenu milele" ndivyo anavyoonekana kusema mtoa zawadi hiyo pichani. (Picha kwa Hisani ya Blog ya Harusini)

Saturday, October 8, 2011

Rais Kikwete asherehekea siku ya kuzaliwa, atimiza miaka 61


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimlisha kipande cha keki mumewe Rais Dk. Jakaya Kikwete wakati wa hafla ya kutimiza miaka 61 ya kuzaliwa kwake iliuyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam juzi jioni. Anayeshuhudia ni mwanawe Ridhwani Kikwete na mkewe pamoja na Aziza, mjukuu wa Rais (Picha na Ikulu).

Wednesday, October 5, 2011

Harusi ya Victor Balthazar Minja na Edna Yusufu Bakari


Bwana Victor Balthazar Minja na Bi. Edna Yusufu Bakari wote wa Arusha Oktoba Mosi, 2011 walikata shauri na kuamua kuishi maisha mapya ya mume na mke. Bw. Victor ni Msanifu Majengo wa Wakala wa Majengo Tanzania na Bi. Edna ni mfanyakazi mkoani Arusha. Shughuli nzima ilifanyika nyumbani kwa Profesa Balthazar Mashindano Minja, Boko-Ununio Beach. Baada ya ibada takatifu ya misa kanisani.


Kama unavyoona kwenye pichani zoezi la nilishe nikulishe lilianza. Hapa safari ya kuelekea kwa wakwe. "Wazazi tulieni mlishwe keki!"


Na baadaye mambo ya picha za kumbukumbu yakafuata. Hata hivyo kwa mapicha zaidi tafadhali mdau ingia; www.prince minja.blogspot.com Picha zote na Prosper Minja



Sunday, October 2, 2011

Harusi ya Joseph na mkewe Maria iliyofanyika Dar es Salaam


Bwana Harusi Joseph (kushoto) akiwa na mkewe Bi. Harusi Maria muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao hivi karibuni jijini Dar es Salaam.


Bwana Harusi Joseph (kulia) akimvisha pete mkewe Maria ikiwa ni ishara ya kuungana katika maisha ya ndoa yao milele, wakati wa ibada ya ndoa yao iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Maharusi Jeseph na mkewe Maria (kushoto) wakifungua muziki kwenye hafla yao. Kulia ni wasimamizi wao wakicheza kuwaunga mkono maharusi hao. (Picha kwa Hisani ya Blog ya Harusini)

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...