Friday, December 17, 2010

Waziri Mkuu Kukutana na wahariri wa habri

YAH: WAZIRI MKUU MHE. PINDA KUKUTANA NA WAHARIRI KWENYE UKUMBI WA OFISINI KWAKE, MAGOGONI, JIJINI DAR ES SALAAM IJUMAA DES. 17, 2010, SAA 5.00 ASUBUHI.
 Kama kawaida yake na kadri anapopata nafasi, Mhe. Pinda hukutana na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuwajulisha kwa ajili ya kuufahamisha umma masuala mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa shughuli za Serikali na pia Wahariri kupata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi wa masuala mbalimbali. Safari hii atakutana nao kama ilivyoelezwa katika kichwa cha habari hapo juu.
 Hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu kuundwa kwa Serikali mpya, baada ya uchaguzi wa Oktoba 31, mwaka huu.
Kwa sababu hiyo, Waziri Mkuu Pinda atazungumzia majukumu mbalimbali yatakayotekelezwa na Serikali hii kwa kipindi cha Miaka Mitano ijayo, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Kwa vile kuna maoni mbalimbali yanayotolewa kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Waziri Mkuu anatarajia kutoa maelezo kuhusu suala hilo pia.
 Kila chombo kilete Mhariri mwenyewe, kwa jina, na Mhariri atakayeshindwa kuja mwenyewe amtaje Mwakilishi wake. Kwa ajili ya kufanikisha mkutano huu na taratibu za usalama kuingia Ofisi ya Waziri Mkuu, majina ya watakaohudhuria baada ya kupata mwaliko huu, yatumwe kwa Barua Pepe na/au Simu kwa mmoja wa wafuatao  na anuani na namba zao:-

By Saidi Nguba – Mwandishi wa Habari wa Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...