Sunday, December 19, 2010

Jana ilikuwa siku nzuri kwani mitaa mingi ya Jiji la Dar es Salaam ilichangamka kutokana na sherehe za mahafali katika vyuo kadhaa. Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) cha Kigamboni kilikuwa moja ya vyuo vilivyofanya mahafali. Mdau wa Blog yetu alijirusha katika moja ya hafla ya mdau mwenzetu na mambo yalikuwa kama hivi;



Mary Machaku akiwa na msimamizi wake.



Ilikuwa ni hafla kabambe ya MARY G. MACHAKU iliyofanyika ukumbi wa Makonde Villa, Kigamboni.



 Mary na mpambe wake wakipata maakuli.


Mambo fulani ya kujipendelea, ilikuwa ni kupofya na kufungua unavyopenda.


Kumbe watoto tusiwazuie kuja kwenye minuso. Hapa wanatoa zawadi kwa Mary.

MC akifanya mamboz.

 kumbe MC's wanatoaga zawadi?
 
Kaka wa Mary, Henry Machaku akitoa maneno ya busara kwa dada yake.



 Mambo fulani ya wapendao, ilikuwa ni pea kwa pea.

Mambo fulani ya mitindo yalikuwepo pia.
Mapapalazi nao walikuwepo 
 Sasa ni wakati wa maakuli, menyu ilikuwa haibagui iwe mtoto wala mkubwa uwezo wako tu wa kupakia.
 Baada ya shamrashamra, kunywa, kula kuselebuka, Mary akiwaaga waalikwa na kwenda kupumzika. Hongera kutoka kwa mdau wa blog kwa kupata shahada ya Uchumi. Keep it up!

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...