Wednesday, December 22, 2010

Siku Mdau Mkuu wa Blog yetu alipokutana na Rais Jakaya Kikwete


‘Unajua Mh. Nataka kuanzisha Blog ya matukio ya kumbukumbu muhimu za jamii’-Mdau Mkuu. ‘Hilo ni jambo la msingi lakini hakikisha Blog hiyo inakuwa msaada kwa jamii yetu’-JK (Rais Jakaya Kikwete). Kama vile maneno haya yalikuwa majibizano ya Mdau Mkuu na Mh. Rais Jakaya Kikwete. Lakini ukweli ni kwamba Mdau Mkuu Oktoba 31, 2010 alikuwa mmoja wa waalikwa wa wanahabari waliokutana na Rais Kikwete, hafla iliyowashirikisha pia baadhi ya wasanii nyota nchini.


Baadaye Mh. alizunguka kusalimiana na kubadilishana mawazo na wageni waliomtembelea.

Baadhi ya wanahabari walioshiriki kuripoti habari za kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu wakiwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya jioni.



Baada ya ‘kula bata’ vya kutosha Mh JK alizungumza mawili matatu na waalikwa wake. Hii inaonesha namna gani Rais wetu alivyo mkarimu kuwasikiliza Watanzania wote wanapomtembelea.  


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...