Thursday, December 30, 2010

Ofisa Habari mpya wa TFF, Boniface Wambura alipoagwa


 Baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa Jambo Concepts Ltd, wachapishaji wa gazeti la Jambo Leo na Jambo Brand wakifanya ishara ya kugonganisha vinywaji vyao katika hafla fupi ya kumuaga Ofisa Habari Mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Boniface Wambura ambaye alikuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo kabla ya kuitwa TFF. Kapuni ya Jambo Concepts ilimzawadia lap top mpya ya kisasa kwaajiri ya kumpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya kabla ya kuondoka katika kampuni hiyo. 


 Mdau Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio akigongesha vinywaji kumpongeza Wambura, katikati mwenye tai ni mwandishi mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe.


Mkurugenzi Mkuu wa Jambo Concepts, Juma Pinto akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo (hawapo pichani) kwenye hafla ya kumuaga Wambura, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa kampuni hiyo, Benny Kissaka. Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi mdogo wa Ofisi za Jambo Concepts jijini Dar es Salaam.

Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, Boniface Wambura (wa pili kushoto), ambaye
ameteuliwa kuwa Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
akikabidhiwa zawadi ya kompyuta ndogo iliyotolewa na uongozi wa Kampuni ya
Jambo Concepts Tanzania Limited (JCTL), wakati wa hafla ya kumuaga Dar es
Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa JCTL, Juma Pinto, Meneja
Mkuu, Ramadhani Kibanike, Mkurugenzi, Benny Kisaka na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Perfect Solutions, Evance Aveva ambaye ni Mshauri wa JCTL. Picha zote kwa hisani ya Jambo Concepts Ltd.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...