Tuesday, April 12, 2011

Yanga Bingwa Ligi Kuu, Simba waanza kutimuana


Kikosi cha timu ya Yanga ya Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam

BAADA ya timu ya Yanga ya Dar es Salaam kutangazwa Mabingwa wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, hali imekuwa mbaya kwa
wapinzani wao wa jadi timu ya Simba na sasa wameanza kutimuana.

Simba imeamua kulifumua upya benchi la ufundi na kuwaondoa
wachezaji 15 katika orodha ya usajili wa Ligi Kuu ya Tanzania.
Akizungumza Dar es Salaam jana mmoja wa viongozi waandamizi wa
klabu ya Simba, amesema klabu hiyo imeona bora ifanye hivyo ili
kuinusuru timu hiyo.

Kiongozi huyo ameongeza kuwa kuna vitu vingi amevigundua kama
baadhi ya wachezaji kujiamini na kufanya kila wanachotaka kwa
faida zao huku wakiiumiza timu.

Alisema baada ya kuangalia kwa kina wamelibaini hilo hivyo kuamua
wawaache watafute timu nyingine za kucheza. "Nimegundua kuna watu
wapo kwa ajili ya maslai yao na si timu hiyo ni bora tuwaache
wafanye mambo yao na kwenda kuchezea timu wanazotaka wao," alisema
kiongozi huyo wa simba.

Alisema kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa wakifanya vitu tofauti
na mikataba yao na bila ya kutambua kuwa mpira ndiyo maisha kwao.
"Tunavunja mikataba ya wachezaji wanne ambao walikuwa bado mwaka
mmoja hii yote tuiweke timu sawa...na kuondoa kirusi kilichopo
ndani ya timu inaaelekea kila msimu tutaendelea kufanya hivi hivi
kama tutaendelea kuwa nao," alisema.

Hata hivyo chanzo kingine cha habari kinasema baadhi ya wachezaji
wanaoachwa yumo mchezaji mkongwe wa timu hiyo, Mussa Hassan Mgosi,
Kelvin Yondani na Mohamed Banka.


Kombe la Ligi Kuu ya Tanzania Bara likiondolewa Uwanja wa Taifa baada ya Timu ya Simba kushindwa litwaa kama ilivyokuwa ikitegemewa.


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...