Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa kuadhimisha miaka 47 ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuunda Tanzania.
Rais wa Tanzania, Jakawa Kikwete (wa pili kulia), Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Shein (wa pili kushoto), Mama Mwanamwema Shein (kushoto) na Makamo Rais wa Tanzania, Dk. Ghalib Bilal (kulia) wakifurahia jambo baada ya Chakula Ikulu Zanzibar. Picha zote kwa hisani ya Ikulu.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete jana aliwaongoza Watanzania kwenye maadhimisho ya miaka 47 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kitaifa Zanzibar .
Sherehe hizo zilifanyika jana Uwanja wa Amaan Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Rais alipigiwa mizinga 21 kabla ya kukagua gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama.
Baadhi ya Viongozi waliohudhuria ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi, Rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Salmin Amour.
No comments:
Post a Comment