Mdau Mkuu wa Blog ya Harusi na Matukio (kushoto) ambaye pia ni mchezaji wa Jambo Leo akiwa amepokea kombe la mashindano ya NSSF baada ya timu yao kulitwaa juzi, kulia ni kaptani wa Jambo Leo Said Mweshehe akiwa ameshika kitita cha sh. 3,500,000 baada ya kuzitwaa na kombe.
Katika mchezo huo mkali uliofanyika jana, timu ya NSSF ndio walio kuwa wa kwanza kupata bao dakika chache baada ya mchezo kuanza lakini muda mfupi baadae Jambo Leo ilisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Said Abdul na hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilitoka uwanjani zikiwa na bao moja (1-1).
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikitafuta bao la kuongoza, lakini timu ya Jambo Leo ndio waliokuwa wa kwanza kuziona nyavu za NSSF kwani dakika ya 47 mchezaji wa Jambo Leo Stivin Waigaga aliipatia timu yake bao la kuongoza.
Mchezo uliendelea kuwa mkali kwani NSSF walikuwa wakitafuta bao la kusawazisha vhuku Jambo Leo wakitafuta lingine ili kuweza kujihakikishia ushindi, likini hadi mwisho wa mchezo timu ya Jambo Leo iliibuka na mabao mawili na NSSF moja.
Kwa ushindi huo timu ya Jambo Leo imejinyakulia kikombe cha mashindano hayo pamoja na fedha taslimu sh. 3,500,000. NSSF kama washindi wa pili wamejinyakulia sh. 2,000,000, huku washindi wa tatu timu ya Uhuru ikijipatia sh. 1,000,000.
Upande wa mpira wa pete kwa mashindano hayo timu ya Habari Zanzibar ndio imeibuka washindi na kupewa kikombe pamoja na fedha. jipatiameifunga Uhuru 1-0 matokeo ambayo timu ya Uhuru imeonekana kushukuru kwa kufungwa bao moja tofauti na walivyotegemea.
Timu ya Jambo Leo ambayo imekuwa ikigawa dozi ya mabao matatu mpaka saba kwa kila timu ambayo inakutana nayo, katika mashindano hayo kiasi cha kuogopwa; Jambo Leo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi imeingia fainali.
PICHA ZAIDI SIKU YA FAINALI CHEKI.
Baadhi ya wachezaji, mashabiki na wafanyakazi wa Jambo Leo wakipiga picha huku wanashangilia NSSF CUP baada ya kulitwaa kombe hilo.
Nahodha wa timu ya mpira wa Miguu wa Jambo Leo, Said Mweshehe akiwa amebebwa na wachezaji wenzake mara baada ya kukabidhiwa kombe la NSSF CUP.
Gari maalumu la Kampuni ya Jambo Leo lililoandaliwa kwa ajili ya kubeba kombe lililochukuliwa na timu ya mpira wa miguu ya Jambo Leo, likiwa linaandaliwa kabla ya kupakizwa kombe kuelekea makao makuu ya kampuni hiyo Samora.
No comments:
Post a Comment