Monday, April 11, 2011

Viongozi wa siasa wafanyabiashara maarufu kutekwa

Sheikh Yahya Hussein

Na Mwandishi Wetu

MNAJIMU maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein ametabiri kuwa viongozi wa siasa na wafanyabiashara maarufu watatekwa kuanzia Aprili 19 na kuendelea hadi mwezi Julai.

Utabiri huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na mnajimu huyo na kusambazwa katika vyombo vya habari. Hata hivyo hakuweka wazi kuwa ni viongozi gain watatekwa au kutaja watu au makundi ambayo yatawateka.

“Viongozi wa siasa na wafanya biashara maarufu wajichunge kutekwa nyara na kuibiwa, wao wenyewe na kufanywa kama bidhaa. Viongozi hao wachukue tahadhari nyakati zao za kutembea na wanaposafiri kwani pana uwezekano wasirudi,” alisema katika taarifa yake.

Akifafanua zaidi alisema kuwa utekaji nyara huo ni wa viongozi walioelezwa kwa makundi kama madiwani, wabunge na nyazifa nyingine wa juu na kuongeza wasijiamini wanaposafiri au wakiwa kwenye mikutano wasiwe peke yao na wawe na mipangilio ya tahadhari nyakati zote. Nyota pia zinalenga wake na masahiba ya viongozi hao mashuhuri.

Mwisho


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...