Thursday, April 14, 2011

JAMBO LEO YAIVUA GAMBA TIMU YA UHURU


Kikosi hatari cha Jambo Leo "Wagumu Star' kabla ya kuanza kwa pambano.

TIMU ya soka ya Jambo Leo ‘Wagumu Star’ jana imeibajua timu ya soka ya Uhuru inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ‘wazee wa kujivua gamba’ katika mashindano ya Kombe la NSSF yanayoendelea jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha vyombo vyote vya habari.

Katika mchezo huo ulofanyika jana kwenye uwanja wa Sigara (TTC) Chang’ombe, Jambo Leo imeifunga Uhuru 1-0 matokeo ambayo timu ya Uhuru imeonekana kushukuru kwa kufungwa bao moja tofauti na walivyotegemea.

Timu ya Jambo Leo ambayo imekuwa ikigawa dozi ya mabao matatu mpaka manne kwa kila timu ambayo inakutana nayo, katika mashindano hayo kiasi cha kuogopwa na kila timu.

Uhuru walionekana kucheza mchezo wa kujiami tangu mwanzo kwani wachezaji wake hasa golikipa alionekana kuchelewesha mipira mithiri timu yake imeshinda jambo ambalo liliwafanya vijana wa Jambo Leo kupunguza kasi kadri ya muda ulivyokuwa ukiyoyoma.

Hadi mapumziko Uhuru ilikuwa ikicheza kwa kujiami huku wakitarajia kumalizika kwa pambano hilo wakiwa sare ili wakabahatishe kwenye penati katika mchezo huo wa nusu fainali.

Kipindi cha pili vijana wa Jambo Leo waliishtukia janja ya wapinzani wao na kuanza kuongeza kasi ya mchezo na kuwachanganya kabisa vijana wa Uhuru na katika dakika ya 72, Aziz Mustafa alifunga goli la shuti kali lililomshinda mlindamlango wa Uhuru na kukubali yaishe.

Hadi mpira unamalizika Jambo Leo ilikuwa na goli moja huku Uhuru wakiambulia patupu. Jambo Leo haijapoteza mchezo hata mmoja tangu kuanza kwa mashindano hayo hadi imeingia fainali. Hata hivyo Uhuru walionekana kuridhika na matokeo hayo kwani walijua katika mchezo huo wangeliangushiwa mvua ya magoli kama ilivyokuwa kwa kila timu inayokutana na Jambo Leo.

“Tunashukuru mungu sisi tumefungwa goli moja wenzetu wamekuwa wakifungwa 3, 4, hadi 7, hivyo tumejitahidi kwa matokeo haya…tumewabana kweli kweli,” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya Uhuru alipozungumza na HM. Mashindano hayo yanaendeleoa tena leo.

Kikosi cha Uhuru katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa pambano hilo.


Mchezaji nyota wa Jambo Leo, Juma Pinto akichuliwa na mmoja wa wahudumu wa kikosi cha msalaba mwekundu (aliye chuchumaa) kabla ya kuanza kwa pambano lao.


Mchezaji hatari wa Jambo Leo, Julius Kihampa (kushoto) mwenye mpira akikabwa na wachezaji wawili wa Uhuru.


Kocha Mkuu wa Jambo Leo, Jerry Cotto akitoa maelekezo kwa mshambuliaji wake, Said Abdul mmoja wa wachezaji wake wakati mpira ukiendelea.



Baadhi ya wafanyakazi wa Jambo Leo (waliosimama) wakifuatilia mpambano. Kutoka kulia waliokaa ni mmoja wa Wakurugenzi wa Jambo Leo, Benny Kisaka akifuatilia mchezo huo kwa makini, Jerry (kocha) na mchezaji wa akiba Julian Msacky.


Kocha wa Jambo Leo (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake namna ya kuwavua gamba vijana wa Uhuru wakati wa mapumziko, wa kwanza kushoto ni mmoja wa wajumbe wa benchi la ufundi la Jambo Leo, Edson Kamukara. Picha zote na mdau wa Harusi na Matukio


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...