Friday, April 15, 2011

Basi la Ngorika lapata ajali laua 9, lajeruhi 16

Basi la Ngorika likiwa limepinduka baada ya kupata ajali ya kugongana na daladala Makumira

Na Mwandishi Wetu
Arusha

WATU 9 wamefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa huku wanne kati yao wakiwa na hali mbaya, baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana na kupinduka katika eneo la Makumira wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya saa 12:30 asubuhi nje kidogo ya Mji wa Arusha.

Alisema ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota hiece lenye namba za usajili T 773 BGT lililokuwa likiendeshwa na Selemani Juma (30) mkazi wa Kijenge na basi la Ngorika aina ya Scania namba T
633 ANF lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam, likiendeshwa na Emanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga, Kilimanjaro.

Kamanda Andengenye alisema alisema ajali hiyo ilitokea baada ya haice kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake akiwemo mwendesha baiskeli, hata hivyo kabla hajalipita aliona basi la Ngorika likija kwa kasi ndipo alipoamua kuingia porini ili kujinusuru asigongane uso kwa uso na gari hilo.

Hata hivyo kabla dereva wa haice hajafika mbali akiiacha barabara basi la Ngorika lilimgonga ubavuni na kusababisha watu 9 waliokuwa ndani ya gari hilo kufariki dunia papo hapo akiwemo dereva wa basi la Ngorika.

Andengenye aliwataja marehemu hao kuwa ni, Kizo Rafael Ndosi (35) mkazi wa Arumeru, Patriki Temba (28), Samsoni Emanuel Minja (60), Hamisi Charles (30), Huruma Safiel (28) wote wakazi wa Usariver na John Kess (38) mkazi wa Majichai.

Wengine ni Emanuel Mchoro (30) mkazi wa Mwanga ambaye ni dereva wa Ngorika na Fatuma Msuya (35) mkazi wa Usariver ambaye ni mwanamke pekee aliyekuwa katika ajali hiyo pamoja na dereva wa
baiskeli aliyejulikana kwa jina moja la Elvisa.

Alisema mpaka sasa jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari ndogo (hiece) mpaka pale upelelezi utakapo kamilika. Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Salashi Toure alisema kuwa wamepokea majeruhi 16 ambapo kati ya hao mmoja amehamishiwa katika hospitali ya Seliani baada ya mapafu yake kuvujia damu nyingi.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...