Waziri wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (katikati )akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi
wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Bi Mwanaidi
Mlolwa akitoa maelezo baada ya
kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600 mjini
Bukoba waliokamatwa
katika kisiwa cha Lubili wilayani Muleba leo.Mwenye koti ni Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu.
Waziri wa
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (aliyenyanyua mikono ) akizungumza na
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustapha Kijuu (mwenye koti)
leo, nje ya ghala la kuhifadhia samaki
katika ofisi ya Uvuvi mjini Bukoba mara
baada ya kushuhudia shehena ya samaki wachanga aina ya Sangara kilo 65600
waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili wilayani
Muleba.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu
Salum Mustapha Kijuu (aliyesimama) akisoma taarifa ya mkoa kuhusu sekta ya
mifugo na Uvuvi kwa Waziri wa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina (alikaa kulia kwake)
leo, mara baada ya kufanya ziara ya ghafla
leo ili kushuhudia shehena ya samaki
wachanga aina ya Sangara kilo 65600 waliokamatwa katika kisiwa cha Lubili
wilayani Muleba. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi
nchini, Mwanaidi Mlolwa.
Mwandishi Maalum,
Bukoba
WAZIRI wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Luhaga
Joelson Mpina
amekamata kilo 65600 za samaki wachanga aina ya Sangara waliokaushwa kwa chumvi
wenye thamani ya shilingi milioni mia tatu katika Kisiwa cha Lubili wilayani
Muleba kwenye Mkoa wa Kagera baada ya wamiliki wa samaki hao
kukimbia.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari
katika Ofisi ya Kitengo cha Doria na Udhibiti wa
Uvuvi wa
mpakani katika Mkoa wa Kagera, Mpina amesema
tukio la kukamatwa kwa samaki hao lilifanikiwa baada ya yeye kupata
taarifa kutoka kwa raia mwema ambapo
aliagiza mamlaka za Wilaya ya Muleba kufuatilia kwa karibu hatimaye
kuwakuta samaki hao wakiwa wameanikwa
chini katika kisiwa hicho.
Waziri Mpina alisema
Sheria ya Uvuvi namba 22 ya Mwaka 2003
na Kanuni zake za mwaka 2009 kifungu cha 90(1) inataka samaki
wanaovuliwa waandaliwe katika mazingira yanayokidhi vigezo vya
usalama kwa mlaji na
kwamba ni kosa kisheria kuwavua au kuchakata samaki aina ya Sangara
walio chini ya sentimeta 50 kwa kuwa ni wachanga na sentimita 25kwa Samaki aina
ya Sato. Pia sentimita 85 kwa Sangara kwa kuwa ni wazazi wanaotakiwa kundelea
kuzaa.
Aidha Waziri aliongeza kwamba Sheria hiyo
imetoa mamlaka kwa watendaji wa Serikali kutaifisha
mali zote zilitumika katika uvuvi haramu kupitia
kifungu cha 37(a) (ii) na (iii) pamoja
na Sheria ya Hifadhi za Bahari
na Maeneo Tengefu
namba 29 ya mwaka 1994.
Waziri Mpina
ameagiza watendaji kufuata
taratibu zote za kisheria ili samaki hao wauzwe kwa njia ya
mnada na mapato hayo yaingie Serikalini mara
moja.
Aidha aliwaonya wafanyabiashara na
wavuvi kuachana na uvuvi haramu kwa kuwa ni kuhujumu raslimali za
taifa ambazo zingetumika kwa kizazi cha
sasa na baadaye.
“Mfanyabiashara yoyote wa samaki na mazao
yake anayetaka
kufilisika na kutafuta matatizo katika
maisha yake aendelee na biashara ya uvuvi haramu,” alisisitiza Mpina
Kufuatia tukio hili, Waziri Mpina
amewapa wiki mbili wafanyabiashara na
wasafirishaji wote wa samaki na mazao yake waliopewa
leseni ya ya kufanya
biashara hiyo kwa mwaka 2018 kuleta cheti cha uthibitisho cha ulipaji
kodi ambapo amesema kama watashindwa
kufanya hivyo hawataruhusiwa kufanya biashara
hiyo.
Alisema kuanzia sasa wafanyabiashara wote
wote
wataruhusiwa kupata leseni hiyo baada ya
kuwasilisha cheti cha uthibitisho wa ulipaji kodi, cheti cha usajili wa kampuni
na mahesabu ya kibiashara yaliyohakikiwa
ili kuepuka utaratibu wa sasa ambao unatoa mwanya kwa mawakala wa ndani na nje
ya nchi kujiingiza katika biashara hiyo kinyemela
na kuikosesha Serikali mapato kwa
kukwepa kulipa kodi
mbalimbali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali
Mstaafu Salum
Mustapha Kijuu alisema Serikali
itahakikisha kwamba uvuvi haramu unakuwa historia
katika Mkoa wa Kagera na kuwataka wananchi kuwafichua
wavuvi haramu
ili vyombo vya Serikali viwakamate na kuwafikisha
katika mikondo ya sheria.
Alisema sekta ya uvuvi
inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa
katika kuinua hali ya uchumi kwenye mkoa wake na taifa kwa ujumla
kama wadau wote watashiriki kikamilifu
katika vita dhidi ya uvuvi
haramu ambapo alisema jumla ya wananchi 26,272
wameajiriwa kutokana
na shughuli za uvuvi katika mkoa huo.
Alisema mkoa utaendelea na kupambana na
uvuvi haramu
ambapo kwa mwaka 2016/17 jumla ya doria
65 zilifanyika na kuwezesha kukamatwa kwa makokoro ya Sangara 422, nyavu ndogo
za dagaa 57,nyavu za timba 3,231, nyavu za makila 14,141, ndoano 711, katuli
16,mitumbwi 133 samaki wachanga kilo 5,621 na watuhumiwa
86.
Hata hivyo Mkuu huyo
alisema katika kuongeza uzalishaji wa
samaki jumla ya mabwawa 584 yamechimbwa kwa mwaka 2016/2017 kutoka mabwawa 181
mwaka 2005/2006 sawa na ongezeko la mabwawa
403.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Mkoa alisema
hivi karibuni Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ngara ilikamata gari lenye namba za uasajili
T 614 CLQ aina ya Mitsubishi Canter likiwa limepakia samaki kilo 2,000 aina ya
Sangara na kilo 530 wa aina ya Sato kwenye mpaka wa Murusagamba
wilayani Ngara.
Alisema Afisa wa Kitengo
cha Doria na Udhibiti wa Uvuvi wa mpakani katika Mkoa wa Kagera
bwana Ayoub Ngoma
na dereva wa gari hilo Ayoub
Sanga walishikiliwa na polisi kwa hatua
za kisheria kwa tuhuma za kushiriki
katika utoroshaji wa samaki wenye kilo 2530
kwenda nchini Burundi zenye thamani ya shilingi 20,850,000/= ambapo Ngoma
ameshasimamishwa kazi kupisha uchunguzi.
Pia Mshauri wa Uvuvi wa Mkuu wa Mkoa,
Efrazi Mkama na maafisa Uvuvi wa Halmashauri ya
Muleba
Wilfred Tibendelana na Maengo Nchimani na Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Bukoba vijijini Renus Ruhuzi wanaendelea kuripoti katika kituo cha polisi
Bukoba kwa mahojiano ya kisheria juu ya utoroshwaji wa samaki
hao.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya
Uvuvi,
Mwanaidi Mlolwa alisema Serikali ina
mkono mrefu na kwamba hakuna mtu
atakayebaki salama iwapo
atajihusisha na uvuvi
haramu. Aidha alisema maafisa uvuvi wanawajibu wa
kuhifadhi na
kutunza takwimu mbalimbali za sekta ya uvuvi ili kutoa picha halisi ya jinsi
sekta inavyochangia katika uchumi wa nchi kwa
ujumla.
“Kimsingi sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa
katika uchumi wa
nchi yetu lakini tatizo kubwa ni ukosefu wa takwimu sahihi.
No comments:
Post a Comment