Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Monday, January 15, 2018
DOTTO BITEKO ATAKA MADINI YAWE NA MCHANGO MKUBWA PATO LA TAIFA
Na Mathias Canal, Dodoma
SEKTA ya Madini inachangia kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 katika Pato la Taifa ukilinganisha na sekta zingine ambazo zimejitutumua kwa kiasi kikubwa katika mchango mahususi wa pato la Taifa nchini Tanzania. Naibu Waziri wa Wizara ya Madini, Dotto Mashaka Biteko amebainisha kuwa kiasi cha kati ya asilimia 3.5 mpaka 4 ni kidogo sana ukilinganisha na umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo Wizara ya Madini imekusudia kuongeza tija katika mchango wa pato la Taifa kupitia sekta hiyo muhimu ya Madini.
Biteko amebainisha hayo leo Januari 15, 2018 wakati akizungumza na wakuu wa idara na vitengo pamoja na watumishi wa Wizara ya Madini ofisi Kuu Mjini Dodoma huku akiwataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uzalendo mkubwa kwa manufaa ya Taifa.
Alisema kuwa sekta ya Madini ni muhimu nchini kutokana na rasilimali Madini ilizonazo hivyo watumishi wote wanapaswa kufikiria namna ya kufanya kazi kwa tija ili kuwa na ongezeko la mchango mkubwa katika pato la Taifa. "Natamani nione kwenye taarifa ya robo mwaka ya BOT ikisoma kwamba sekta ya madini inachangia angalau asilimia 10 ya Pato la Taifa kuliko ilivyo hivi sasa na hilo naamini linawezekana kwa ushirikiano wa pamoja," Alisisitiza Mhe Biteko Mhe Biteko.
Alisema kuwa hakuna mtu yeyote ambaye atatutumua mabega kwamba ni mkubwa katika Wizara badala yake ukubwa wa cheo na umri utaonekana katika matokeo muhimu na makubwa katika utendaji kazi. "Mimi kuwa Naibu Waziri hapa So What...kama sitofanya kazi yenye matokeo makubwa kutokana na imani niliyopewa na Rais nitakuwa si lolote, hivyo kwa ushirikiano wenu pekee tutaweza kutimiza utendaji uliotukuka na wenye manufaa makubwa," Alikaririwa Biteko wakati akizungumza na watumishi wa Wizara ya Madini Biteko alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli anafanya kazi nzuri kwa manufaa makubwa ya watanzania wote hivyo watumishi mbalimbali wa serikali, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo pasina kurudisha nyuma makusudi na matakwa ya utekelezaji wa ilani ya ushindi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwaka 2015-2020. Asubuhi siku ya Jumatatu Januari 8, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk. John Pombe Magufuli alimuapisha, Dotto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa madini, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...
-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo ...
No comments:
Post a Comment