Thursday, January 18, 2018

MAKAMU WA RAIS AKAGUA MIFEREJI ENEO LA BUGURUNI MIVINJENI na MTONI KWA AZIZ


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Mtaro wa Maji katika eneo la Buguruni Mivinjeni na Ilala Sharifu Shamba wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa mtaro wa maji wenye urefu wa mita 475. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi waliojitokeza kwa wingi Mtoni kwa Azizi Ali alipoenda kukagua mradi wa ujenzi wa mtaro wenye urefu wa mita 550. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akizungumza katika ziara hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Buguruni Mivinjeni na Ilala Sharifu Shamba wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa mtaro wa maji wenye urefu wa mita 475. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wanaoishi kwenye mpaka kati ya Buguruni Mivinjeni na Sharifu Shamba pamoja na Mtoni kwa Azizi Ali kuwa watunzaji wazuri wa mitaro ya maji kwani ni mali yao wenyewe na si ya serikali.

Makamu wa Rais aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kuta za bahari na mitaro ya maji jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais aliwaeleza wananchi hao kuwa mabadiliko ya tabia nchi yameathiri shughuli za kiuchumi, kijamii na kimazingira. Makamu wa Rais Makamu wa Rais alisema kila mmoja anapaswa kujishughulisha katika suala la kusafisha na kuhifadhi mazingira.

“ubaya wa mazingira ukiyaharibu yanakuadhibu,” alisisitiza  Makamu wa Rais

Mtaro wa Buguruni Mivinjeni una urefu wa mita 475 na ule wa kwa Azizi Ali una urefu wa mita 550.

Makamu wa Rais alisema nchi inapozungumzia uchumi wa viwanda ni mazingira “tukiharibu mazingira hamna uchumi wa viwanda” hata viwanda vitakavyojengwa vinahitaji kutunza mazingira, visafishe maji yake kabla ya kutiririsha.

Makamu wa Rais alitoa rai kwa yeyote atakayebainika kuharibu miundo mbinu wanachukuliwa hatua za haraka. Makamu wa Rais alimalizia kwa kusema kuwa Usalama wa Nchi, Amani, afya, mazingira bora hayana chama hivyo ni jukumu la kila mmoja kuwajibika ili maendeleo yaweze kupatikana.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuongezeka kwa watu katika jiji la Dar es Salaam na mabadiliko ya tabia nchi kutaendelea kutoa changamoto za miundo mbinu hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kujenga miundo mbinu itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli zao kwa kushirikiana na wadau wa Maendeleo.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...