Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi, Kheri Denice James akizungumza na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake wilayani Nzega Mkoa wa Tabora (hawapo pichani). |
Na Mwandishi wetu, Tabora
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) umesema umeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya afya inayotokana na ahadi katika ilani ya uchaguzi katika halmshauri za wilaya mji wa Nzega na Nzega vijijini mkoani Tabora.
Pia Umoja huo umeeleza kikubwa kasi hiyo inatokana na kuwepo kwa mashirikiano makubwa kati ya viongozi wa chama, Halmashauri za wilaya na serikali kuu.
Matamshi hayo yametamkwa jana na Mwenyekiti wa Taifa wa UVCCM Kheri Denise james mara baada ya kumaliza kutembelea mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Kazogolo katika Halmashauri ya Mji wa Nzege.
Kheri alisema kitendo cha serikali ya awamu ya tano kupeleka jumla ya shilingi milioni mia tano toka serikali kuu oktoba mwaka huu kwa ajali ya ujenzi wa kituo hicho ni kielelezo kuwa serikali inajali maisha ya wetu wake .
"UVCCM tumeridhishwa na ujenzi wa miradi ya afya katika Halmashauri ya Mji wa Nzega na Halmashauri ya Nzega vijijini. Ilani ya uchaguzi ya chama imetekelezwa kwa vitendo. Hii ndiyo tafsiri halisi ya hapa kazi," Alisems Kheir .
Aidha alisema kazi ya kuwatumikia wananchi haina mjadala badala yake inamhitaji kila kiongozi dhamana kuwa nafasi yake kuwajibika na kuwatumikia wananchi.
"Kuimarika kwa huduma za jamii na watu kupata huduma bora ndiyo malengo ya kisera yanayotakiwa kufanikishwa. Tuna wajibu kila mmoja kwa nafasi yake kumsaidia Rais na serikali yale." Alisisitiza.
Kheri akiwa mkoani Tabora ametembelea mradi mkubwa wa usambazaji maji toka ziwa Victoria mkoani mwanza kupitia shinyanga hadi Tabora, kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya kazogolo na kuzumgumza na wananchi katika halmashsuri ya mji wa nzega na nzega vijiijini.
No comments:
Post a Comment