Tuesday, January 16, 2018

Diwani wa CCM Kata ya Kihesa akabidhiwa hati ya ushindi

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa wakifurahia kukabidhiwa kwa hati kwa diwani wa chama hicho tukio hilo lilifanika katika ofisi ya kata ya kihesa likihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa Jully Sawani wakizungumza na wananchi waliohudhulia tukio hilo.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas, diwani halali wa kata ya kihesa  Jully Sawani wakiwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa kata ya kihesa.

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiongea na wananchi walijitokeza kushudia tukia na kupewa cheti Diwani wa Kata hiyo Jully Sawani.

Na Fredy Mgunda, Iringa.

KATA ya Kihesa Manispaa ya Iringa imeanza kupata neema ya mamilioni ya fedha za kimaendeleo mara baada ya kumpata Diwani mpya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kupita bila kupigwa kutoka na vyama vingine vya siasa kutoweka wagombea.

Akikabidhiwa hati ya utambulisho wa kuwa ndio diwani halali wa Kata ya Kihesa, Jully Sawani alielezea mikakati ya kimaendeleo ya kata hiyo ambayo ataanza nayo ni kukarabati miundombinu ya barabara kwenye baadhi ya mitaa ya kata hiyo.

“Ukipita kwenye mitaa yetu utagundua kuwa mtaa kama mtaa wa mafifi miundombinu ya barabara sio nzuri kabisho akahidi kuwa ndani ya wiki hii atapeleka kata pila lianze kazi ya kuzikarabati bara bara hizo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wake kwa kuwa wamemtuma kufanya kazi” alisema Sawani

Sawani aliongeza kuwa amejiandaa kuhakikisha anatatua kero za wananchi kwa kushirikiana na Serikali ya Manispaa ya Iringa ambayo inatekeleza sera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 huku ikiwa na kauli mbiu inayosema kuwa hapa kazi tu.

“Naomba niseme ukweli wananchi wangu wote wa kata ya Kihesa sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio mchezo mchezo mliokuwa mnaufanya nimeomba kuwa diwani kwa lengo la kuhakikisha kila mwananchi wa kata hii anafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa familia yake haiwi masikini,ninasema kuwa kila ukilala hakikisha unaukataa umasikini kwa kuutamka wakati unalala tena kwa zaidi ya mara tisa hapo ndio utafanya kazi” alisema Sawani

Aidha Sawani alitoa kilio chake cha kwa kuomba msaada wa kimaendeleo kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ambapo alimwambia kuwa wananshida ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na kusaidiwa kumalizia ujenzi wa jingo la kibiashara ambalo lipo jirani na ofisi za kata ya hiyo.

“Mheshimiwa MNEC Salim Asas nipo hapa naomba utusidie msaada wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari ya Kihesa na jengo hili ambalo lipo mbele yetu unaliona linahitaji kumaliziwa ili kuweza kuongeza ajira kwa wananchi wa kata yangu hivyo naomba sana msaada wako kukamilisha hivi vyote kwa awamu hii ya kwanza” alisema Sawani

Akihutubia mamia ya wananchi walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa kata hiyo Jully Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya saruji kwa ajili ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto nyingine.

“Leo naanza kwa kutoa mifuko miambili ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za shule hiyo ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa uhuru kwa lengo la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa katika kuleta maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo hivyo nitasaidia sana kwenye elimu” alisema Asas

Asas aliwakata viongozi wa kata hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na kuacha kuishi kimazoea.

“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas


Asas alisema vijembe na malumbano ya kisiasa katika kata hiyo yanatosha na akawataka vijana hao kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakavyowawezesha kufikiwa kirahisi na mipango mbalimbali ya maendeleo 

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...