Wednesday, January 17, 2018

MAGUFULI AKUTANA NA MAWAZIRI WA ELIMU, APIGA MARUFUKU MICHANGO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli (katikati) akisisitiza jambo mara baada ya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kulia) pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kushoto). Picha na IKULU.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli leo Ikulu jijini Dar es Salaam amekutana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo. Katika mazungumzo hayo Rais ameendelea kusisitiza azma yake ya kupiga marufuku aina yoyote ya michango katika shule za serikali ziwe za msingi na zile za sekondari na amewaagiza mawaziri hao kuhakikisha wanasimamia agizo hilo ipasavyo. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli (katikati) akiwa katika mazungumzo leo Ikulu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (kulia) pamoja na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo (kushoto). Picha na IKULU.




No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...