Wednesday, January 31, 2018

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na  wafugaji  kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dk. Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji  kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  

Dereva  wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  (Picha na Ngailo Ndatta)
Na John Mapepele, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba  timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi  baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara, Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma. Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa,” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka  Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote  katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga  chapa  mifugo ambayo inatoka nje ya nchi  ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania  waliyoingia  katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika  vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali  inakadiliwa kwamba  30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo  toka nje ya nchi.
Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano  na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana  aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na  wengine wawili wakipewa onyo kali.

Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi  ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri  ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.

Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa  Desemba 31 Mwaka jana.

Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...