Wednesday, January 31, 2018

Balozi wa Ujerumani Tanzania ashiriki maadhimisho ya wahanga utawala wa Hitler

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter akizungumza na wanafunzi walioshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani. Kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Wanafunzi hao wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter pamoja na Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo (mbele) pamoja na wanafunzi (nyuma) wakiangalia filamu zinazozungumzia kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika maadhimisho hayo wakiuliza maswali kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter kwenye mjadala juu ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

BALOZI wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter ameshiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa kidikteta wa Adolf Hitler nchini Ujerumani.

Akizungumza katika maadhimisho hayo, yalioshirikisha wanafunzi mbalimbali wa Shule za Sekondari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo aliwataka vijana kujitambua, kupenda kujifunza historia na pia kutokubali kutumika kuchochea vurugu katika maeneo yao.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya wahanga waliopoteza maisha katika vita vya moto vilivyotokea mwaka 1933 hadi 1945 chini ya utawala wa mfumo wa 'Nazism' uliolenga kuwateketeza Wayahudi kwa kuamini si binadamu bora yalipoteza uhai wa watu takribani milioni sita wakiwemo watoto. Mfumo ambao pia ulitokomeza watu wenye ulemavu na wafupi kwa kuangamizwa kwa kutumia gesi za sumu na pamoja na moto. 

Aidha alisema baadhi ya maeneo vijana wanaweza kujikuta wanatumika katika matukio yanayochangia vurugu hivyo kuna kila sababu ya wao kupewa elimu ya kujua historia kwa undani ili wasiweze kutumika kwa namna yoyote. 

"Upo umuhimu wa vijana kutokubali kushiriki katika masuala ya ukatili, vurugu za aina yoyote ile...alisema vijana wanapaswa kujitambua na kufahamu historia na jukumu lao la kulinda amani kwa faida ya mataifa yao," 

Vijana hao kutoka shule mbalimbali za sekondari jijini Dar es Salaam walipata elimu pia kutoka kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Dk. Detlef Waechter juu ya historia ya mauaji hayo, ambapo walipata fursa za kujadili na kuuliza maswali tofauti kutoka kwa balozi huyo raia wa Ujerumani.

KATIBU MKUU WA MIFUGO KUKABIDHI RASMI TAARIFA YA CHAPA YA MIFUGO

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na  wafugaji  kuhusu upigaji chapa mifugo kwenye Kijiji cha Makere Mkoani Kigoma.Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo akishiriki zoezi la Upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia  Sekta ya Mifugo nchini, Dk. Maria Mashingo (mwenye skafu) akiongea na baadhi ya wafugaji  kuhamasisha upigaji chapa mifugo katika siku ya mwisho ya zoezi hilo leo huko Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  

Dereva  wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bwana Athuman Ramadhani akishiriki katika zoezi la upigaji chapa katika Mkoa wa Kigoma. Kipindi cha kupiga chapa kitaifa knaiisha rasmi leo Januari 31.  (Picha na Ngailo Ndatta)
Na John Mapepele, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Mifugo nchini, Dkt Maria Mashingo amewataka Wakuu Wote wa Idara katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba  timu zote zilizosambaa kote nchini ziwe zimewasili mjini Dodoma leo na kwamba ifikapo saa kumi na mbili jioni ziwe zimewasilisha taarifa kuhusu zoezi hilo kwake ili akabidhi rasmi kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Mpina kwa ajili ya hatua zaidi  baada ya zoezi hilo kuisha rasmi leo.

“Wakuu Wote wa Idara, Mhe Waziri anataka Timu za Chapa zirudi Dodoma. Leo saa 12 jioni apate taarifa ya mwisho ya upigaji chapa. Mkurugenzi wa Mipango ratibu timu ya kukamilisha taarifa,” alisisitiza Mashingo kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Wakuu wa Idara.

Aidha amezitaka  Halmashauri zote nchini kuhakikisha wamemaliza zoezi la kupiga chapa mifugo yao yote  katika muda wa nyongeza uliotolewa na Serikali ambao uliamuliwa kuwa Januari 31mwaka huu.

Akizungumza katika siku za mwisho wakati anahitimisha ukaguzi na uhamasishaji wa zoezi la kupiga chapa katika Mkoa wa Kigoma, Dkt. Mashingo amewaonya baadhi ya wafugaji kutojiingiza katika matatizo ya kupiga  chapa  mifugo ambayo inatoka nje ya nchi  ambapo amesema wakibainika watachukuliwa hatua kali.

Aidha, Dkt. Mashingo amewataka wafugaji wote wasio raia wa Tanzania  waliyoingia  katika mikoa ya mipakani kuondoa mifugo yao mara moja kwa kuwa haitapigwa chapa badala yake watakamatwa na kufikishwa katika  vyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine Dkt. Mashingo ambaye pia ni mtaalam bobezi katika eneo la malisho ya mifugo amesema kufanikiwa kwa zoezi la kupiga chapa kutasaidia usimamizi wa Sekta ya Mifugo hapa nchini ambapo alisema awali  inakadiliwa kwamba  30% ya malisho yote nchini yalikuwa yakitumiwa na mifugo  toka nje ya nchi.
Ameutaka Uongozi wa Chama cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kutopingana na Serikali badala yake kuongeza ushirikiano  na kuwaelimisha wenzao kufuga kisasa ili kuondoa migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.

Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina wakati akihitimisha zoezi la upigaji chapa mifugo kitaifa lililofanyika katika wilayani Itilima mkoani Simiyu, Desemba 31mwaka jana  aliongeza siku 30 kwa halmashauri zote nchini ili kukamilisha zoezi la kupigaji chapa mifugo huku akiwavua nyadhifa maafisa wawili wa Wizara kwa kushindwa kusimamia zoezi hilo kikamilifu na  wengine wawili wakipewa onyo kali.

Alida kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi  ya changamoto zilizosababisha zoezi hilo kufanyika kwa asilimia 38.5 tu kwa nchi nzima baadhi ya watendaji wa serikali na viongozi walichangia kulikwamisha ambapo Halimashauri  ambazo zikamilisha zoezi la chapa chini ya asilimia 10 zilipelekwa majina ya watendaji wao kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu.

Siku kumi na tano baada ya muda wa nyongeza wa siku thelathini, Mhe. Mpina alitoa tathmini mbele ya Waandishi wa Habari mjini Dodoma, kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la upigaji chapa mifugo ambapo Mpina alisema hadi kufikia siku hiyo ya Januari 16 mwaka huu jumla ya ng’ombe 10,306,359 sawa na asilimia 59.3 ya lengo walishapigwa chapa ikiwa ni ongezeko la asilimia 20 ya tathmini ya awali iliyofanywa  Desemba 31 Mwaka jana.

Aidha alisema wafugaji wote nchini watakaoshindwa kupiga chapa mifugo yao ndani ya muda uliowekwa hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji Namba 12 ya mwaka 2010 ibara ya 4 kifungu cha 26.

GLOBAL FUND WAIMWAGIA TANZANIA TRIONI MOJA KUSAIDIA,MALARIA,UKIWI NA TB


 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora (kulia), na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban, wakisaini hati za makabidhiano ya sh. trioni moja zilizotolewa na Shirika la Global Fund kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia mapambano ya Ukimwi, TB na Malaria katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dar es Salaam leo. Wengine waliosimama katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  na viongozi wengine kutoka Global Fund.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya, akizungumza katika hafla hiyo.


Balozi wa Ufaransa Nchini Tanzania, Frederic Clavier, akizungumza kwenye hafla hiyo.


Mnufaika wa Global Fund, Joan akielezea jinsi alivyo nufaika na shirika hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine, akizungumza.


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamisi Shaaban (kulia), akimkabidhi hati ya makabidhiano Mwakilishi wa Global Fund Tanzania, Linden Morrison.


Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Makamu wa Rais (Sera na Uratibu), Profesa Faustine Kamuzora, akizungumza.


Taswira ya ukumbi wa mkutano katika uzinduzi huo.

Na Dotto Mwaibale

SHIRIKA la Kimataifa la Global Fund limetoa shilingi trioni moja kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya mapambano ya magonjwa ya ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa mwaka 2018-2020. 

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini makabidhiano ya fedha hizo baina ya mfuko huo na serikali Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema fedha hizo ni muhimu sana kwa nchi yetu.

Alisema fedha hizo zitaelekezwa katika kupambana na magonjwa hayo ambapo kwa ugonjwa wa ukimwi zimetolewa sh. bilioni 769, TB sh. bilioni 67 wakati malaria sh. bilioni 320.

Alisema fedha hizo zitatumika kikamilifu kwa lengo lililokusudiwa na zitasimamiwa na Ofisi ya Rais, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Afya na Mashirika Yasiyo ya kiserikali.

Alisema katika masuala ya ukimwi zitatumika kwa ajili ya vipimo, dawa za kurefusha maisha na kufubaza virusi kwa wagonjwa wa ukimwi na katika ugonjwa wa malaria fedha hizo zitatumika kwa ajili ya vipimo na matibabu pamoja na kununua vyandarua.


"Kwa upande wa wagonjwa wa TB ni asilimia 40 tu ndio waliofika kwenye vituo vya afya na kuthibitika kuwa na maambukizi na wamepatiwa matibabu lakini tunataka hadi ifikapo mwaka 2020 tunataka asilimia 70 ya watanzania watakaogundulika kuwa na maambukizi wajulikane na wapatiwe matibabu," alisema Ummy.

Ummy aliongeza kuwa kati ya wagonjwa 100 wenye maambukizi ya TB wagonjwa 90 waliothibitika kuwa na maambukizi walitibiwa na kupona kabisa.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy amewataka Katibu Mkuu wa Wizara yake, Tamisemi na Ofisi ya Rais kuhakikisha wanazisimamia vizuri fedha hizo ili kupata matokeo mazuri waliyo yakusudia.

Mratibu wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya Tanzania (TANPUD), Happy Assan alisema mradi huo utawasaidia sana na kuhakikisha hawataathirika ukizingatia kuwa fedha hizo zitawafikia walengwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu wanaishi na VVU-Ukimwi, Mwinuka Juastine alisema mradi Global Fund imewasaidia waathirika 900,000 kwa kuwapa dawa za kupunguza makali ya ukimwi ARV na kufubaza virusi vya ugonjwa huo.

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi aipa siku 3 TBA kumalizia bomoabomoa Tanesco

Bomoabomoa jengo la Tanesco.

KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga ameipa siku tatu Wakala wa Nyumba nchini (TBA), kuhakikisha inamaliza kazi ya uvunjaji wa jengo la ghorofa 10 la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).

Nyamhanga alitoa agizo hilo ikiwa ni takribani siku 63 tangu TBA kuanza ubomoaji wa jengo baada ya Rais John Magufuli Nevemba 15 kuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kuvunja jengo hilo na Ofisi ya Wizara ya Maji kwa kuwa zimejengwa katika hifadhi ya barabara.

Rais Magufuli alisema hakuna kumuonea mtu huruma au aibu katika kipindi hiki na kwamba kama Serikali imeenda kinyume na taratibu ivunjiwe kama walivyovunjiwa wananchi wengine.

Katibu mkuu alisema ubomoaji wa jengo hilo umechukua muda mrefu hivyo ikifika Februari mosi haitaji kuona jengo hilo likiwepo hivyo kuruhusu shughuli nyingine za ujenzi ziendelee.

“Wametoa maelezo ya kwanini wamechelewa kumaliza ubomoaji nimewaelewa ila ikifika Februari mosi sihitaji kuona sehemu iliyobakia tunataka ujenzi wa barabara ya kupishana uanze,” alisema.

Nyamhanga alisema mkandarasi amefanikiwa kuhamisha miundombinu mbalimbali ambayo ipo katika eneo litakalojengwa barabara za kupishana (interchange) hivyo kinachosubiriwa ni TBA kumalizika uvunjaji.

Alisema baada ya kukagua amegundua kuwa kati ya ghorofa 10 nane zimeshavunjwa hivyo amewaagiza kumalizia ghorofa mbili zilizobakia ili mradi wa barabara za ya kupishana eneo la Ubungo uanze kama inavyotakiwa.

“Nimekagua ubomoaji naona maendeleo ni mazuri hivyo nimewaagiza ikifika kesho kutwa Alhamisi wawe wamemaliza ili kazi zingine ziendelee kwani wakandarasi wanawasubiri,” alisema.

Alisema dhamira ya Serikali ni kuona mradi wa barabara za kupishana unamalizika kwa wakati kama walivyokubaliana ambao ni miezi 36.

Mhandisi Nyamhanga alisema kwa mujibu wa mkataba kati ya Wakala wa Barabara Tanzania Tanroads na Mkandarasi kampuni ya China Civil Engeneering Contract Corporation (CCECC) ujenzi wa barabara hiyo utagharimu zaidi ya sh. bilioni 177.

Aidha, Nyamhanga alisema ujenzi wa barabara ya kilomita 16 njia nne kutoka Kimara hadi Kiluvya unatarajiwa kuanza mapema mwezi Machi.

Alisema ni imani yake kuwa hatua zinahitajika ili kupatikana mkandarasi zitachukuliwa haraka kwani fedha zipo.

“Pamoja na ujenzi wa barabara za kupishana hapa Ubungo Serikali imedhamiria kuifungua Dar es Salaam ambapo mwezi Machi ujezi wa barabara ya njia nne utaanza kutoka Kimara hadi Kiluvia,” alisema.

Akizungumzia hatua zilizofikiwa hadi sasa kuhusu ujenzi huo Meneja wa Tanroads mkoa wa Dar es Salaam, Julius Ndyamukama alisema uchambuzi wawakandarasi wenyewe uwezo wa kutekeleza mradi umefanyika, usanifu umefayika na zabuni imetolewa kwa kampuni iliyokidhi vigezo ili kuwasilisha gharama za mradi.

Ndyamukama alisema kesho wanatarajia watarejeshewa majibu na ndani ya siku 14 hatua zote zitakamilika ili ujenzi uanze.

Meneja huyo alisema katika upanuzi wa barabara hiyo kutajengwa madaraja matatu katika maeneo ya Kilivia, Kibamba na Mpiji pamoja na kuwepo barabara za mchepuko.

Aidha, alisema katika mradi huo kutakuwa na barabara za kupishana eneo la Mlonganzila ili kurahisisha kufika katika Hospitali ya Mlonganzila.

“Hatua zote zikimalizika ndio tutao taarifa rasmi kuwa ujenzi utagharimu shilingi ngapi kwa sasa tunakamilisha hatua muhimu," alisema.

Tuesday, January 30, 2018

Prof. Mbarawa afungua mkutano Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Posta. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Posta, Dk. Haruni Kondo na kulia ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Dk. Haruni Kondo (wa pili kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa TPC, Joseph Ngowi (kulia), wakati wakimsubiri mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa. Katikati ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe.Wengine kushoto ni Maofisa waandamizi kutoka wizarani.


Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta, ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kulia ni mgeni rasmi, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.


Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo ya ufunguzi wa baraza hilo.   


Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri Profesa Mbarawa kuufungua mkutano huo. 


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi huo.


Baadhi ya Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akifungua  mkutano huo. 


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Mbarawa, akizungumza na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, wakati akiufungua mkutano wa baraza hilo, jijini Dar es Salaam leo. 



Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Mbarawa.


Wajumbe wa Baraza Kuu, wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.


Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Peter Bihume, Meneja wa Posta Mkoa wa Kigoma, akimuuliza swali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa katika mkutano huo.


Mjumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, Ahmed Kaumo, ambaye pia ni Mwenyekiti TEWUTA, akitoa neno la shukrani kwa Waziri Prof. Mbarawa.


Mkuu wa Kitengo cha uhusiano cha TPC, Elia Madulesi, akizungumza, wakati akifafanua jambo katika mkutano huo.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, mara baada ya kuufungua mkutano wao, jijini Dar es Salaam leo.  


 Mwenyekiti wa Bodi ya TPC Dkt. Haruni Kondo akisalimiana na wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi mara baada ya kuufungua mkutano wao huo jijini Dar es Salaam leo.


Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi, wakiwa katika mkutano huo, leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (katikati mbele), akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TPC, mara baada ya kuufungua mkutano huo, jijini leo. kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Dk. Haruni Kondo na kulia kwake ni Kaimu Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe. 

Monday, January 29, 2018

DK WILBROD SLAA AKUTANA NA RAIS MAGUFULI IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuanza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa kabla ya kuzungumza na wanahabaari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi Mteule Dkt. Wilbrod Slaa mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo ambaye aliambatana na Maafisa Wakuu (sita) wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ambao wanatarajiwa kustaafu.

MPINA AVITAKA VIWANDA VYA SAMAKI KANDA YA ZIWA KUANZA KAZI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina(mwenye miwani ) akishirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Bi Anarozy Nyamubi kuteketeza nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi  maalum alichokiunda hivi karibuni katika wilaya ya Musoma kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi, Emanueli Bulayi akishuhudia tukio hilo leo.(Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Joelson Mpina akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Anarozy Nyamubi baada ya kuteketeza nyavu haramu katika Wilaya ya Butiama leo. (Na John Mapepele)
Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney akimwaga mafuta kwenye nyavu haramu ili kuzichoma moto katika kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo. (Na John Mapepele)
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Joelson Mpina akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bwai Kumusoma wilayani Musoma leo ambapo alishiriki zoezi la kuchoma nyavu haramu zilizokamatwa na kikosi kazi  cha kudhibiti uvuvi haramu Kanda ya Ziwa Victoria  alichokiunda hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt. Vincent  Anney akisoma majina ya  Wavuvi Haramu (Na John Mapepele)

Asisitiza operesheni ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ziwa ni  ya kudumu
Na John Mapepele, Mara
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameagiza viwanda vinne vya kuchakata samaki na mazao yake vilivyofungwa  katika  Mikoa ya Mwanza na Mara kuanza kazi mara moja ifikapo Julai Mosi mwaka huu, ambapo amewataka wamiliki kupeleka mipango kazi ya namna ya kuvifufua  kabla ya  kufikia mwezi Machi mwaka  wizarani kwake.
 Alivitaja viwanda hivyo kuwa ni Tan Perch Limited na Supreme Perch Limited vilivyopo Mwanza na  Mara Fish Packers Limited na Prime Catch Limited  katika mkoa wa Mara.
Waziri Mpina alizungumza hayo jana wakati alipokuwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara na Mwanza kukagua operesheni maalum ya kutokomeza uvuvi haramu kanda ya Ziwa Victoria inayofanywa na kikosi kazi maalum alichokiunda hivi karibuni.
“Mimi kama Waziri mwenye dhamana ya Sekta ya Uvuvi nchini niliyepa kulinda raslimali za uvuvi nitahakikisha kwamba  ulinzi wa raslimali hizi ni wa kudumu, na usio na mwisho hadi uvuvi haramu utakapoisha  hapa nchini” alisisitiza Mpina
Waziri Mpina alipata fursa ya kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Kamati ya Ulinzi ya Mkoa huo, wananchi katika maeneo tofauti na hatimaye kushiriki katika zoezi la kuchoma nyavu haramu ambapo hadi sasa zaidi ya nyavu zenye thamani ya shilingi bilioni nne zimechomwa moto katika zoezi linaloendelea la kudhibiti uvuvi haramu mkoani Mara.
Kamanda anayeongoza kikosi cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi Kanda ya Mara, Bakari Lulela alimweleza Waziri Mpina kuwa operesheni hiyo imefanyika katika Wilaya za Musoma, Butiama, Rorya na Bunda na kufanikiwa kukamata na kuteketeza zana haramu zenye thamani ya sh. bilioni 3.2 huku wavuvi na wafanyabiashara wa samaki na mazao yake waliokiuka sheria ya uvuvi wakitozwa faini ya sh. milioni 189.
Waziri Mpina aliziagiza mamlaka zinazohusika kuwachukulia hatua Maafisa Uvuvi wa  Kijiji cha Bwai Kumsoma waliotuhumiwa kushirikiana na wavuvi haramu kuondolewa mara moja katika kijiji hicho ili kupisha uchunguzi na ikithibitika wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dk. Vincent Anney amesema kwamba hayuko tayari kuona Wilaya yake inaendelea kuishi na watumishi wanaojihusisha na uvuvi haramu  na kwamba sheria kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwa ni pamoja na kuwaondoa katika wilaya hiyo.
Aidha Waziri Mpina ameiagiza Wizara yake kuandaa bei elekezi ya kununua samaki itakayowezesha kuondokana na tabia ya wenye viwanda kushusha hovyo bei pindi samaki wanapoongezeka na hivyo kuwadhulumu wavuvi kupata malipo stahili yanayotokana na kazi yao.
Waziri Mpina alisema Ziwa Victoria ni hazina na raslimali kubwa kwa Tanzania ambapo inaaminika kuwa  ni la kwanza kwa ukubwa katika bara la Afrika kwa kuwa na eneo la 68,000Km2  na la pili duniani.
Alisema  pamoja  na umuhimu wa ziwa hili katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya watanzania bado linakabiliwa na shughuli za uvuvi haramu uliokithiri ambapo tafiti zinaonyesha kwamba kama hakutakuwa na jitihada za haraka za kutokomeza uvuvi haramu, ziwa hilo hali halitakuwa  na raslimali za uvuvi ikiwa ni pamoja na samaki katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Alitaja uvuvi haramu unaofanywa kuwa  ni pamoja na kuvua katika maeneo yasiyoruhusiwa, kutumia valiyombo visivyosajiliwa, kuvua bila leseni,kutumia sumu, kutumia nyavu za utali na kuvua samaki wachanga ama wazazi wasioruhusiwa.
Uvuvi haramu mwingini nikuvua kwa kokoro na  nyavu zenye macho madogo chini ya kiwango kinachokubalika kisheria, katuli, kumbakumba na gizagiza ambapo alisema Serikali imedhamilia kutokomeza  uvuvi huo haramu.
Aidha alisema operesheni hiyo katika kanda ya Ziwa Victoria dhidi  ya uvuvi  haramu ni ya kudumu na inafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na.22 yaMwaka 2003 na Kanuni 58(1) ya Uvuvi ya Mwaka 2009 na Sheria ya Mazingira Na 20 ya Mwaka 2004 kifungu Na(1), 65(1)a pia Sheria ya Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Na 29 ya Mwaka 1994 ili kudhibiti uvuvi haramu ulioshamiri kiasi cha kutoweka kwa raslimali ya samaki katika ziwa hilo kwa faida ya vizazi vya sasa na baadaye.
Waziri Mpina alisema Tanzania inamiliki 51% ya Ziwa hili ikifuatiwa na Uganda 43% na nchi ya Kenya inamiliki 6%. Ziwa hili ni moja ya maziwa yanayozalisha samaki kwa wingi duniani kwa makadirio ya takribani tani 1,000,000 kwa mwaka  ambapo asilimia 60 ya uzalishaji wa samaki wake unatoka Tanzania hivyo juhudi za pamoja za kutokomeza uvuvi haramu zinahitajika.

DK. KIGWANGALLA ATUMA SALAMU KWA WALIOVAMIA KIWANJA NJIRO...!


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akipata maelezo ya eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82 ndani ya eneo hilo kutoka Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Dk. Fredy Manongi (katikati). Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jinala Bodi ya Utalii Tanzania. 

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua eneo la kiwanja chenye hati namba 4091 kilichopo Njiro Jijini Arusha ambacho kimevamiwa na watu mbalimbali na kuanzishwa makazi yenye kaya 82. Eneo hilo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na hati halisi ya eneo hilo ipo kwa jina la Bodi ya Utalii Tanzania.

  Meneja wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Egidius Mweyunge (kulia) akimuongoza Waziri Kigwangalla kukagua eneo hilo.

Dk. Kigwangalla akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua eneo hilo.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...