Saturday, September 12, 2015

PPF YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI

 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, (kushoto), na Afisa wa Fedha Mwandamizi wa Mfuko huo, Angel Mukasa, (kulia), na Mfanyakazi mwingine wa Mfuko huo, Omari Bundile, (wapili kushoto), wakigawa mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi, pamoja na sare za shule na viatu kwa wanafunzi hawa wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2015. Katika kutekeleza sera ya mfuko ya kusaidia jamii, PPF, imetoa vifaa mbalimbali ikiwemo, sare za snhule, viatu na mafuta hayo maalum, Meneja Uhusiano wa Mfuko huo Lulu Mengele aliwaambia waandishi wa habari. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
 Latifa Musa,(kulia), akitoa shukrani kjwa niaba ya wenzake baada ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu, Kurasini jijini Dar es Salaam, kupatiwa msaada na Mfuko wa Pensheni wa PPF

Watoto wenye ulemavu wa ngozi, wakiteta jambo, baada ya kupatiwa msaada wa vifaa yakiwemo mafuta maalum yanayotumiwa na watu wenye ulemavu wa ngozi
 Picha ya pamoja ya maafisa wa PPF, Walimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Jeshi la Wokovu
 Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya Jeshi la Wokovu, Flora Millinga, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Lulu akiwa na baadhi ya watoto
 Meneja Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Lulu Mengele, akizungumza na watoto hao wakati wa kutoa msaada wa vitu mbalimbali Septemba 11, 2015
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Janet Ezekiel, (kulia), akizungumza jambo na baadhi ya watoto hao
 Kikundi cha Kwaya kikitoa burudani
Angel Mukasa, akizungumza na baadhi ya watoto

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...