Tuesday, September 1, 2015

PAUL MAKONDA KATIKA UZINDUZI WA KITABU

Paul Makonda akizindua vitabu 

Mkuu wa Wilaya Kinondoni Mh.Paul Makonda siku ya jana katika kanisa la Living Water Center chini ya mtumishi wa Mungu Apostle Onesmo Ndegi alikuwa mgeni wa heshima katika uzinduzi wa vitabu vitatu  "MJUE MWANAMKE,USIIPE HOFU NAFASI na RAFIKI ANAYEKUFAA vilivyoandikwa na Mwl Lilian Ndegi wa Kanisa la Living Water Center Kawe.

Ibada hiyo ya uzinduzi wa vitabu ilipambwa na vikundi vya uimbaji sifa kama Living Waters wenyeji Upendo Nkone,GUG Dancers na More Than Enough Band.


Mkuu huyo wa wilaya ndiye aliyezindua vitabu hivyo na kuendesha zoezi zima la uuzaji wa vitabu hvyo,kwa kuanza alinunua vitabu hivyo vitatu kwa shiling Milioni 5 ikiwa ni kuchangia na kusapoti huduma hiyo ya uandishi wa vitabu vya Mwl Lilian Ndegi ambaye ni Mama yake kwa malezi ya kiroho kanisani hapo Living Water Center Kawe.


Katika uzinduzi huo uliambatana na kukata keki ikiwa ni ishara ya kufurahia mafanikio ya kazi ya uandishi wa Mwl Lilian Ndegi na ugawaji wa zawadi katika tukio hilo ulifanyika kwa watu ambao wamekuwa wakihusika katika ufanikishaji kwa namna moja au nyingine au kumuwezesha Mwl Lilian kufanikisha uandishi wake wa vitabu.


Mh Paul Makonda aliwasihi washirika wa Kanisa la Living Water Center Kawe kusapoti kazi ya Mwl Lilian ikiwa ni kwa kununua na kuvisambaza vitabu vyake ili viwafikie wasomaji wengi ikiwa vitaleta matokeo mazuri katika maisha yao kutokana na ujumbe ulio ndani ya vitabu hivyo.


Apostle Onesmo Ndegi kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na mme wa mwandishi wa vitabu Mwl Lilian Ndegi katika kuzungumza kwake alikuwa akijivunia Mkuu huyo wa Wilaya na kusema ni kijana wake anamfahamu vizuri siku nyingi tangu bado anasoma na kusema amelelewa hapo na kusema kuwa alikuwa msikivu,na mpaka Mh Rais kumteua kwa nafasi hiyo ya kuwa Kiongozi wa Wilaya hakukosea.


 Mh.Paul Makonda alipokuwa akionesha vitabu baada ya kuzindua
Baadhi ya wageni waliokuwa wamealikwa katika uzinduzi huo wa vitabu wa kwanza kush Mchungaji Deborah Ntepa,Mama Mchungaji Tumwidike koka Mbeya na Mwl. Lilian ndegi mwenyeji
.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Mzee wa Kanisa vitabu baadhi ya watu walionunua baada ya kuvizindua
.Paul Makonda alipokuwa akiwakabidhi Kiongozi wa mabinti Kanisani hapo Magreth vitabu baada ya kuvizindua

Mama Mchungaji Tumwidike kutoka mbeya alikuwepo katika uzinduzi huo
Upendo Nkone alipokuwa akihudumu katika ibada ya uzinduzi wa vitabu iliyoongozwa na Mh. Makonda
Mh.Paul Makonda wa kwanza kushoto,katikati ni Apostle Ndegi Kiongozi wa Kanisa la Living Water Center na wa mwisho ni Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi 
Mwandishi wa vitabu Mwl. Lilian Ndegi katika picha ya pamoja baadhi ya wakina mama wa  kanisani hapo.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...