Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mtwara, Mohamed Sinani akizungumza na wananchi pamoja na wanaCCM wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan.
|
|
| Na Joachim Mushi, Mtwara |
| MKUTANO wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi |
| (CCM), Bi. Samia Hassan Suluhu umefanikiwa kuvuna wanachama 180 kutoka vyama |
| mbalimbali vya upinzani Mkoani Mtwara. |
| Katika mkutano huo uliofanyika leo Manispaa ya Mtwara Mikindani jumla ya wanachama |
| 180 kutoka vya CUF, Chadema, NCCR-Mageuzi, TLP na ACT Wazalendo wamerudisha kadi |
| zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi ambapo wamepokewa na Bi. Samia Suluhu. |
| Akizungumza katika zoezi la kuwapokea wanachama hao wapya mgombea mwenza Bi. Suluhu |
| aliwaomba wanachama wa CCM Mtwara kuwapokea vijana hao na kuwatumia kufanya kazi za |
| kampeni kwani wamerudi nyumbani hivyo hakuna haja ya kuwatenga. |
| Akimnadi mgombea wa urais wa chama hicho, Dk. John Pombe Magufuli, Bi. Suluhu |
| aliwaomba wanaMtwara kumpigia kura mgombea huyo kwani ana mambo makubwa aliopanga |
| kuyafanya kwa Mji wa Mtwara ili kuhakikisha unakuwa kiuchumi pamoja na wananchi |
| wake. |
| Alisema Serikali ya CCM imepanga kujenga reli itakayotoka Mtwara kwenda Songea hadi |
| Mbambabay ambayo itakuwa mtaji mkubwa kiuchumi wa viwanda kwa mkoa huo, kwani |
| itakuwa ikisafirisha makaa ya mawe kutoka Songea Mkoani Ruvuma kuja katika viwanda |
| vitakavyojengwa Mkoa wa Mtwara. |
| Aliongeza kuwa wamepanga kujenga maegesho ya meli kubwa manne mkoani Mtwara hatua |
| ambayo itaongeza ukubwa wa Bandari na wingi wa meli zitakazokuwa zikiingia na |
| kutoka mkoa humo jambo ambalo alisema litachangia kukuza uchumi wa nchi hiyo. |
| Aliongeza kuwa watahakikisha wananchi ambao viwanja vyao vimechukuliwa kwa ajili ya |
| shughuli nyingine katika maeneo ya Magomeni, Ufukweni, Matengo pamoja na Mji Mwema |
| wanalipwa fidia kulingana na soko la sasa. |
| Alisema Serikali ya CCM inapigana na umasikini na sio masikini hivyo lazima |
| iendelee kuwalipa vizuri wananchi ambao viwanja vyao vimetwaliwa kwa shughuli |
| nyingine. "...Tunapigana na umasikini wala si masikini, lengo ni kuwawezesha," |
| alisema Bi. Samia Suluhu. |
| Mgombea huyo mwenza leo anamaliza ziara yake ya kuinadi ilani ya Chama Cha |
| Mapinduzi mikoa ya kusini ambapo alipita majimbo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara |
| kuelezea nini watawafanyia wananchi wa maeneo hayo endapo watapata ridhaa ya kuunda |
| dola tena. |
No comments:
Post a Comment