Thursday, September 17, 2015

CCM Yakubali Mdahalo wa Wazi na Mgombea wa Chadema, Lowassa

Aliyekuwa mbunge wa Nkenge, Asumpta Mshama akizungumza na wananchi na wanaCCM katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza, Bi. Samia Hassan Suluhu Mtwara Vijijini.
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan Suluhu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika moja ya mikutano ya kampeni Mtwara Vijijini.

Na Joachim Mushi, Mtwara

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekubali ombi la msemaji wa kambi ya ushirikiano wa vyama vinavyounda UKAWA la kufanya mdahalo wa wazi kati ya wagombea urais wa nafasi za urais yaani John Pombe Magufuli wa CCM na Edward Ngoyai Lowassa wa CHADEMA.

Kauli ya CCM imetolewa leo na mgombea mwenza wa urais Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu katika hotuba zake alizozitoa kwa nyakati tofauti kwenye mikutano yake ya hadhara ya kampeni ya CCM aliyoifanya Wilayani Newala na Jimbo la Mtwara Vijijini.

Bi. Suluhu alitoa kauli hiyo akijibu hoja ya kambi ya UKAWA iliyotolewa jana na msemaji wa kambi hiyo, James Mbatia alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jana akieleza kuwa kuna haja ya kuomba mdahalo wa wazi kati ya wagombea hao kwa lengo la kuwasikia nini wanataka kuzungumza.

Mgombea huyo mwenza alisema Chama Cha Mapinduzi kipo tayari kufanya mdahalo na mgombea wa CHADEMA, lakini ikiwa mdahalo huo utakuwa kati ya wagombea hao ili kuwapa nafasi ya kujieleza kiunaga ubaga kujua nini wagombea hao watajitolea kufanya ili kuendelea jamii ya Watanzania endapo wakifanikiwa kuingia madarakani.

Mgombea huyo mwenza akifafanua zaidi katika mikutano yake ya kampeni Jimbo la la Mtwara Vijijini alisema Serikali ya CCM imepanga kuijenga na kuiboresha Bandari ya Mtwara ili iweze kuleta tija zaidi kwa watumiaji wake. Aliongeza kuwa Serikali ya CCM endapo itapita imepanga kujenga barabara ikiwemo ya Mtwara-Newala- Masasi, hospitali, pamoja na kuukamilisha mradi wa 'Makonde Water Sapply' ambao unasaidia kuleta maji mjini.

Alisema kwa wakulima wa korosho Serikali itakuwa ikitoa pembejeo na dhamana kwa mahitaji ya wakulima ili kuchochea uzalishaji wa wakulima. Alisema dhana ya ruzuku za kilimo itatekelezwa kwa upangilio maalumu kwa lengo la kumuwezesha mdhamini.

Mgombea mwenza huyo amekuwa akipata wakati mgumu njiani akitokea Mtwara mjini kuelekea Wilaya ya Newala ambapo wananchi wamekuwa wakifunga barabara kumsimamisha ili aweze kuzungumza nao, huku wakitaja baadhi ya kero katika maeneo yao wakiomba azitatuwe endapo atafanikiwa kuunda dola.
 
Mgombea mwenza Bi. Samia Suluhu akimtambulisha na kumuombea kura mgombea Ubunge, Mathias Chikawe katika moja ya mikutano ya kampeni. 
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu (kulia) akimtambulisha mgombea ubunge wa chama hicho Rashid Akbar (kulia). 
Baadhi ya wagombea udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakitambulishwa kwenye mkutano wa kampeni.
Mgombea mwenza Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na wanachama na wananchi mara baada ya kuzinduwa tawi la wakereketwa la Kitama 1.  
Mgombea mwenza Bi. Samia Suluhu (katikati) akizungumza na wanachama na wananchi mara baada ya kuzinduwa tawi la wakereketwa la Kitama 1.  
Bi. Samia Suluhu katikati akipokea kadi ya mwanachama mpya wa Chama Cha Mapinduzi baada ya uzinduzi wa Shina la Wakereketwa Kitama 1, Mtwara Vijijini.
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan Suluhu.
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan Suluhu.
Mmoja mwa makada wa CHADEMA, Greison Mtemi Nyakarugu ambaye kwa sasa yupo Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM.
Baadhi ya wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea mwenza wa chama hicho, Bi. Samia Hassan Suluhu.
Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika moja ya mikutano ya kampeni Mtwara.

Mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza na wanaCCM na wananchi katika moja ya mikutano ya kampeni Wilaya ya Newala.

Baadhi ya vijana wanaCCM wakizunguka wakiimba kwenye moja ya mikutano ya kampeni iliyokuwa ikifanyika Wilaya ya Newala.
Bi. Samia Suluhu (kushoto) akizungumza na mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia.
Kulia ni Mathias Chikawe (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani (kulia) wakijadiliana jambo kwenye moja ya mikutano ya kampeni..

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...