|
Mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (kulia) juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. |
|
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray akizungumza na wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. |
|
WanaCCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mikumi Morogoro . |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa nafasi ya urais Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu Hassan katika Jimbo la Mikumi Morogoro. |
|
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (katikati) akijadiliana jambo la baadhi ya wasanii wenzake wanaoisapoti CCM katika kampeni zake. |
|
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray akipanda jukwaani kuwasalimia wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. |
|
Msanii Ray akishuka jukwaani baada ya kuzungumza na wananchi juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro baada ya msanii huyo kukihama Chadema na kuanza kuinadi CCM. |
|
Msanii Ray na Anti Ezekiel jukwaa kuu wakisalimiana na mgombea mwenza na viongozi wa CCM jukwaa kuu juzi katika Jimbo la Mikumi Morogoro. |
|
Msanii maarufu wa Bongo Movie nchini, Vicent Kigosi a.k.a Ray (katikati) akijadiliana jambo la baadhi ya wasanii wenzake wanaoisapoti CCM katika kampeni zake. |
|
Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie ma kada wa CCM waliojitolea kukinadi chama hicho wakiwa katika moja ya mikutano ya kampeni za CCM. |
MSANII maarufu wa uigizaji sinema nchini Vicent Kigosi au kwa jina maarufu Ray pamoja na mwenzake Anti Ezekiel wameanza rasmi kukinadi Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kutangaza kuihama kambi ya upinzani (UKAWA) ambako awali walikuwa wakikipigia chapuo chama cha Chadema.
Ray ambaye juzi ameanza kupanda jukwaa la CCM akikiunga mkono Chama Cha Mapinduzi katika mikutano ya kampeni alisikika akisema awali alikuwa amepotea kuwa upinzani lakini sasa amestuka na kuamua kurudi nyumbani 'CCM' chama alichokiita makini chenye sera na ilani za kueleweka.
"...CCM oyeeeee, Mama Samia Suluhu oyeeeee...Magufuli oyeeeee, Mnenionaaaa...nimerudi nyumbani (CCM) kule (upinzani) nilikuwa nimepotea hivyo nimestukia mchezo na kurudi nyumbani," alisema Ray huku akishangilia na idadi kubwa ya wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo wa kampeni uliofanyika Jimbo la Mikumi Mkoa wa Morogoro juzi.
Ray ambaye katika msafara huo aliambatana na msanii nyota na maarufu wa uigizaji nchini Anti Ezekiel pamoja na kundi la wasanii linalojulikana kama "Mama Ongea na Mwanao" ambalo linaiunga mkono CCM, walisema wataendelea kukiunga mkono chama hicho kwa kuwa kimefanya mengi kwa wananchi na wasanii kwa ujumla.
Katika mkutano huo wa kampeni uliohutubiwa na mgombea mwenza nafasi ya urais CCM, Bi. Samia Suluhu aliwaomba wananchi wa Jimbo la Mikumi kuichagua CCM kwani ilani mpya ya uchaguzi imepanga kufanya mengi eneo hilo ikiwa ni pamoja na kukagua mashamba pori kuyapima na kuwagawia wananchi ili kuondoa migogoro kati ya wakulima na wafugaji.
Alisema tayari kwa sasa kuna mashamba manne ambayo yamefutwa hati kwa wawekezaji na yatagawiwa kwa wananchi wa eneo husika, kwani awamu ya serikali ya tano ni kuhakikisha inamaliza na kukomesha migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji. Aliongeza kuwa kero ya maji itamalizika muda mfupi mara baada ya chama hicho kuingia madarakani kwani mradi wa husambazaji maji eneo hilo umekamilika kwa asilimia 80 kwa sasa mkandarasi anasubiri kiasi kidogo cha fedha toka serikalini ili kumalizia mradi huo.
Alisema serikali itakayoundwa na CCM imejipanga kukabiliana na suala zima la wanyama kuharibu mazao ya wakulima eneo hilo ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa miundo mbinu ambapo itaijenga barabara ya Ludewa - Kilosa kwa kiwango cha lami na tayari shilingi bilioni 10 za ujenzi wa barabara hiyo zimetengwa.
Bi. Suluhu alisema uboreshaji maslahi ya wazee na wafanyakazi pia ni suala ambalo ilani mpya ya uchaguzi ya CCM imepanga kulifanyia kazi ili makundi hayo yaweze kuishi kwa kumudu changamoto za maisha.