Bw. Emmanuel Lymo akiwa na mkewe, Gudila katika hafla ya harusi yao iliyofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu mara baada ya kufunga ndoa kwenye Kanisa la KKKT Dar es Salaam Februari 27, 2011.
Bw. Emmanuel akiwa na mkewe Gudila, nyuma yao ni wasimamizi wa ndoa yao.
Bi. Harusi Gudila akicheza muziki akiwa na mpambe wake.
Baadaye Emmanuel na mkewe Gudila walifungua muziki rasmi.
Baada ya muziki kufungulia mambo yalikuwa hivi...
Angalia hapa warembo wakijimwaga na mduara.
Baadhi ya wageni waalikwa wakilisakata rumba.
Hii ilikuwa ni keki waliolishana maharusi, lakini kama unavyojua mambo ya kichaga kulikuwa na ndafu kama tatu hivi ambazo zote zilitumika kupamba sherehe ya maharusi hawa.
Wakati wa kufungua shampeni haikumlazimu mgeni kusogea mbele ili apate mvinyo huo, kwani kila meza ilikuwa na shampeni yake. Hapa mmoja wa wageni waalikwa akifungua kinywaji hicho kwenye meza yetu.
Ulifika wakati wa maakuli, cheki.
Walianza maharusi kwanza
Waalikwa wakiendelea kulisakata rumba
Cheki waalikwa walivyokuwa bomba..!
Baadhi ya wanakamati wakiwa mbele ya wageni waalikwa.
Wanakamati wakipiga picha ya pamoja baada ya kutoa bonge la zawadi kwa maaharusi.
MC wa harusi hii ya kukata na shoka alikuwa mwendeshaji wa kipindi cha Cherekochereko kinachorushwa na televisheni ya TBC.
Mambo ilikuwa ni kata mti panda miti kwa upande wa vinywaji, cheki hapa; Peter Uisso (kulia) akiwa mmoa wa wageni waalikwa huku wakibadilishana mawazo ilhali meza ikiwa imesheheni vinywaji.
Pedejee John Uisso alikuwa mmoja wa waalikwa wa karibu wa maharusi, pichani anaonekana akitabaruku zaidi.
Waalikwa mbalimbali wakiendelea kupata moja moto moja baridi.
Picha zote na mdau Mkuu wa Harusi na Matukio. Tutaingiza picha zaidi na kurekebisha picha na maelezo mara baada ya kupata maoni ya wahusika kwenye sherehe hii. Karibu.
No comments:
Post a Comment