Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi.
Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, amesema Serikali imeunda Kamati itakayokwenda Loliondo kumsaidia Mchungaji Ambilike Mwasapila kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaofika nyumbani kwake kwa ajili ya huduma.
Hata hivyo kiongozi huyo alifafanua kuwa Serikali haijazuia tiba hiyo kutoka kwa Mchungaji huyo, na wala haina mpango wa kuzuia ila kutokana na uwingi wa watu na magari yaliyokwama katika Kijiji hicho kuna kila sababu ya kuingila ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi hao kabla ya kutokea maafa eneo hilo.
Aidha alisema Serikali kupitia Kamati yake iliyoundwa kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, wamejipanga kuanza kuzuia magari yote yanayoingia kijiji hicho ili kupunguza msongamano uliopo na badala yake waruhusu magari kutoka tu hadi hapo yatakapopungua na kuhakikisha huduma hiyo inayotolewa kwa utaratibu kuepuka msongamano.
Lukuvi, aliwashauri Wananchi waliokwishafanikiwa kupata huduma hiyo kwenda katika vituo vya afya na kupima afya zao baada ya siku 14 tangu walipokunywa dawa ili kuweza kuona kama kunamabadiliko ama la, wakati Serikali kupitia Kamati yake ikiendelea na kuifanyia kazi dawa hiyo kuweza kubaini ubora wake na Dozi yake kwa ujumla, ili iweze kuwa katika kiwango.
Mbali na Kamati hiyo Serikali imejipanga kupeleka magari ya kubebea wagonjwa eneo hilo ili kuweza kutoa huduma ya kuwawaisha waliozidiwa katika mahospitali, pamoja na kuandaa huduma za afya kama vyoo na mahema ya kupumzikia wananchi wanaokuwa wakisubiri kupata huduma.
No comments:
Post a Comment