Thursday, March 31, 2011

Harusi ya Moshi Mbully na mkewe Mwashada


Februari 11, 2011 itabaki siku maalumu na kumbukumbu ya milele kwa Bw. Moshi Mbully wa Kinondoni Dar es Salaam na mkewe Bi. Mwashada wa Kigogo Mbuyuni Dar es salaam, kwani ndiyo siku waliounganishwa rasmi kama mke na mume.


Mwashada akimuongoza mumewe kwenda kuwaaga wazazi wake kabla ya kuondoka na mumewe baada ya ndoa yao.


Wageni waalikwa wakitoa mkono wa kwaheri kwa maharusi kabla ya kuondoka ukumbini.


Mama wa Bi. Harusi, Mrs Ewald Mushi akiwa katika pozi siku ya harusi ya mwanae.



Shangazi wa bibi harusi, Mrs G. Ishengoma (katikati) akiwa pamoja na wageni waalikwa


Shughuli mbalimbali zikiendelea ukumbini



Mambo ya maakuli ilikuwa ni uwezo wako tu


DJ wa harusi hiyo Frank Bush (kulia) akiwa na Mrs Herry aka Mama Rose ambaye ni mdogo wa Bi. harusi wakiwa kwenye mapoz ya picha. Picha zote na Mdau Mkuu wa HM.

Tuesday, March 29, 2011

Obama aeleza sababu za kumpiga Gadhafi


Rais wa Marekani, Barrack Obama

RAIS Barrack Obama wa Marekani, ameeleza sababu za kuingilia mgogoro uliokuwa ukiendelea nchini Libya, kati ya Rais wa nchi hiyo, Moammar Gadhafi na waasi waliokuwa wakimpinga na maandamano yaliokuwa yakifanywa na makundi ya wananchi nchini humo.

Miongoni mwa sababu ya msingi ambazo Obama amewaeleza waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, ni kwamba waliamua kufanya hivyo ili kunusuru maisha ya wana-Libya waliokuwa wakiuawa na majeshi ya Serikali yaliokuwa yakiwazuia waandamanaji waliokuwa wakimpinga Gadhafi.

Obama alisema nchi yake isingelipenda kuona wananchi wakiuawa na kunyanyasika ilhali hawana hatia na ndio maana yeye (USA) na washirika wake walifanya uamuzi wa kuivamia Libya kwa lengo la kumuondoa Gadhafi madarakani.

"Tunamalizia kufanya mashambulizi ya mwisho kwenye mji ambao ulikuwa makazi na ngome ya Gadhafi lakini baada ya hapo tutakabidhi madaraka ya kuiongoza nchi ya Libya kwa Jeshi la NATO, ili waweke utaratibu wa nchi kurudi wakati wake," alisema Obama akionekana kujiamini.

Monday, March 28, 2011

Ujumbe maalumu wa Rais Omar el Bashir kwa JK


Rais Jakaya Kikwete akipokea ujumbe maalumu wa Rais Omar El Bashir wa Sudan kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan,  Ali Ahmed Karti aliouwasilisha Ikulu Dar es Salaam. (PICHA NA MDAU FREDDY MARO)

Saturday, March 26, 2011

BREAKING NEWZZZ; Roho za Watanzania zaendelea kuteketea

*Ajali mbaya yaua tena 9, yajeruhi wengine

IKIWA ni siku chache tangu ajali ya wasanii wa kundi la five star kutokea Mkoa wa Morogoro na kuua wasanii 13 wa kundi hilo na nyingine kutokea tena eneo jirani na lile na kuua watu watatu na wengine kujeruhiwa, imetokea nyingine mbaya na kuua watu tisa.

Kwa mujibu wa taarifa tulizozipata muda huu kutoka kwa shuhuda ambaye yupo safarini eneo hilo, gari aina ya coaster namba T 566 AZP lililokuwa likitoka Chalinze kwenda Dar es Salaam limegongana na lori namba T 535 AAG; na imedaiwa watu tisa wamekufa papo hapo na wengine kujeruhiwa vibaya.

Akizungumza na shuhuda huyo amesema coaster ililikuta lori limesimama njiani na likitaka kulipita lilitokea lori lingine mbele ndipo dereva alipoamua kulivamia lori lililosimama akijaribu kukwepa kugongana uso kwa uso na lori la mbele yake.

Shuhuda huyo amesema kuwa waliokufa wote wametoka kwenye coaster na maiti zinaondolewa na inadaiwa zinapelekwa hospitali ya Tumbi, Kibaha.

“Ajali hii imehusisha gari aina ya coaster ambalo lilikuwa likitokea Chalinze kwenda Dar es Salaam, limegongana na lori lenye tela dereva wa coaster inaonekana kavunjika miguu yote…na gari imebondeka vibaya mbele…,” anasema na kuendelea.

“Hapa kwa sasa magari hayatembei maana ajali imeziba barabara foleni ni ndefu kuanzia maeneo ya Daraja la Ruvu hadi eneo la ajali,” alisema shuhuda huyo liyejitaja kwa jina moja la Ally akizungumza kwa njia ya simu Harusi na Matukio (HM).

Aidha alisema eneo ilipotokea ajali ni kilomita chache kabla ya kufika Kiluvya ukitokea Chalinze majira ya saa tano na tayari askari wa usalama barabarani wamefika kutoa msaada kwa wahusika, huku wakijitahidi kuongoza magari kwani barabara ilifungwa na ajali hiyo.

Tunaendelea kukusanya taarifa na tutawaleteeni kadri zinavyotufikia kutoka kwa vyanzo vya HM.

Tuesday, March 22, 2011

Jambo Leo wawafanya vibaya TBC1 kombe la NSSF



Baadhi ya wachezaji wa Jambo Leo katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo wao na TBC1.


TIMU ya Soka ya Gazeti la Jambo Leo, linalomilikiwa na kampuni ya Jambo Concepts Ltd, imeshindilia timu ya Soka ya Shirika la Habari Tanzania (TBC 1) mabao 3 kwa moja.

Wakicheza mpira ulioonekana wa hali ya juu kiasi cha kuwapa tabu muda wote, TBC1 Jambo Leo ndio walioanza kuanza kufungua mvua ya magoli baada ya muda mfupi tangu kuanza kwa pambano hilo.

Goli la kwanza la Jambo Leo, liliwachanganya zaidi washambuliaji wa TBC1 na kujitahidi kusawazisha muda mfupi baadaye kabla ya mapumziko. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi hasa kwa wachezaji wa Jambo Leo ambao walionekana kuwaelemea zaidi TBC1 na kuandika mabao mawili mengine ya harakaharaka.

Hadi mwisho wa mchezo huo Jambo Leo 3 na TBC1 waliambulia goli moja.


Benchi la ufundi la Jambo Leo pamoja na wachezaji wa akiba. Watatu kulia waliokaa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Jambo Concepts Ltd, Benny Kissaka akifuatilia vijana wake.




Kikosi kizima cha timu ya Jambo Leo kikiwa na kocha wake (wa kwanza kushoto waliosimama) na kiongozi wa benchi la ufundi (wa pili waliosimama) kabla ya kuanza kwa pambano kati ya TBC1 na timu hiyo.

Waamuzi wa mchezo huo wakiwa katika picha ya pamoja, kabla ya kuanza kwa pambano.




Kikosi cha TBC1 kilichoshindiliwa 3-1 katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Picha na Mdau Mkuu wa Harusi na Matukio.

BREAKING NEWS: Issa Kijoti wa 5 Star, wenzake wa 5 wafariki kwenye ajali Morogoro, walikuwa safarini kurudi Dar


Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani.


Na Mwandishi Wetu

TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema kuwa, wanamuziki wa kundi la 5 star wamepata ajali mbaya eneo la Mikumi Morogoro na watu watano akiwemo muimbaji maarufu wa kundi hilo Issa Kijoti wamefariki dunia.

Taarifa zinasema ajali hiyo imetokea baada ya gari lililokuwa limewabeba wanamuziki wa kundi la taarabu la 5 Star, kugongana uso kwa uso na roli la mbao, wakati wakitokea mikoani kuja Dar es Salaam.

Inasemekana waliotambuliwa kufariki dunia mpaka sasa ni pamoja na Issa Kijoti, Hamisa Omary, Husna Mapande, omary Hashim, Nasor na Shaby Juma. Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zinasema tayari miili ya marehemu hao imeondolewa eneo la ajali na kupelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Morogoro.

Mdau mmoja wa masuala ya muziki amethibitisha kupatwa na ajali kwa wanamuziki hao, kwani amedai simu zao zinapigwa na kuita bila majibu kati ya kundi lililokuwa likisafiri katika gari hilo.

Inadaiwa jumla ya watu sita (6) wamefariki dunia katika ajali hiyo. Taarifa zaidi zitatolewa na HM kadri zitakavyotufikia, endelea kufuatilia.




Thursday, March 17, 2011

Picha mbalimbali za ziara ya NSSF Bukoba na Mwanza kukagua miradi yao



Meneja wa Kiwanda cha Sukari Kagera, Nestory Ruchungura (wa kwanza kulia aliye nyoosha mkono mbele) akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea kiwanda hicho juzi mjini Kagera. 


Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana akitoa maelezo mafupi ya kiwanda hicho kwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF walipotembelea kiwanda hicho hivi karibuni.








Meneja wa Kiwanda cha Sukari Kagera, Nestory Ruchungura (wa kwanza kulia aliye nyoosha mkono mbele) akitoa maelekezo kwa baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) walipotembelea kiwanda hicho juzi mjini Kagera. 


Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF (waliosimama msitari wa mbele) wakipiga picha ya pamoja ya kumbukumbu na baadhi ya viongozi wa juu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera (waliosimama nyuma). Wapili kushoto mbele ni Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda, Buddana Rau. Nyuma ni moja ya matrekta ya kisasa yalionunuliwa na kiwanda hicho baada ya mkopo wa NSSF kwa kiwanda hicho, matrekta hayo yanauwezo wa kufanya kazi yenyewe kwa msaada mdogo wa dereva.


Miongoni mwa matrekta ya kisasa yaliyonunuliwa na kiwanda hicho baada ya kupata ufadhili wa mkopo wa takriban bilioni 12 kutoka NSSF



Kutoka kushoto ni Mwenekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajab (mwenye koti), Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Mudhihir Mudhihir wakiwaongoza wajumbe wengine wa NSSF kutembelea kiwanda hicho. NSSF imetoa ufadhili wa mkopo wa sh. bilioni 12 kwa kiwanda hicho.








‘Hakuna uhaba wa Sukari Tanzania’

Kutoka kushoto (mbele) ni Mwenekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Abubakar Rajab (mwenye koti), Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NSSF, Mudhihir Mudhihir wakiwaongoza wajumbe wengine kutembelea kiwanda hicho. NSSF imetoa ufadhili wa mkopo wa sh. bilioni 12 kwa kiwanda hicho.

Na Joachim Mushi
Kagera
MENEJA Mkuu wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera, Ashwin Rana amesema hakuna upungufu wowote wa bidhaa hiyo nchini, kwani kiwanda hicho pamoja na kile cha Mtibwa kina akiba ya kutosha kusambaza nchini.
Amesema Kiwanda cha Sukari cha Kagera na kile cha Mtibwa (Mtibwa Sugar) ambavyo vyte ni vya mmiliki mmoja vina akiba ya bidhaa hiyo iliyoko stoo ya kutosha kukabiliana na mahitaji ya nchini pamoja na wajeja wake wengine.
Rana alitoa taarifa hiyo juzi mjini hapa alipokuwa akitoa ufafanuzi mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), walipofanya ziara kukitembelea kiwanda cha Sukari cha Kagera kuona uzalishaji wake.
Kauli hiyo imekuja wakati idadi kubwa ya Watanzania wakiamini nchi ina upungufu wa bidhaa hiyo kutokana na kupanda bei mara dufu maeneo mbalimbali ya nchi, na tayari Serikali imekusudia kuagiza bidhaa hiyo kutoka nje.
Alisema kiwanda hicho kilichoanza kazi baada ya kubinafsishwa mwaka 2001 kimefanyiwa ukarabati mkubwa wa miundombinu, mitambo anuai ya kiwanda, ununuzi wa nyenzo za kisasa na upanuzi kwa baadhi ya maeneo umekiwezesha kuzalisha tani 120 za sukari kwa saa tangu mwaka 2010.
“Sukari ipo ya kutosha kwenye godauni zetu zote mbili…hadi ninavyoongea hivi tuna takribani tani 5500 za sukari zimekaa, hakuna tatizo lolote, zinasubiri wanunuzi,” alisema Rana akiwaeleza wajumbe wa NSSF waliotembelea kiwanda hicho.
 Aliongeza kuwa shehena hiyo kubwa ya sukari ipo pia katika kiwanda cha Mtibwa ambacho kipo chini ya mmiliki mmoja pamoja na cha Kagera. Alisema kulingana na hali ya uzalishaji upungufu wa bidhaa hiyo huenda ukajitokeza kuanzia mwezi Mei.
Akitoa ufafanuzi zaidi kwa wajumbe, Rana alisema awamu ya pili ya ukarabati wa kiwanda inayotarajia kukamilika Juni, 2012 itakiongezea ufanisi kiwanda hivyo kuwa na uwezo wa kuzalisha tani 200 za sukari kwa saa tofauti na ilivyo sasa.
Hata hivyo alibainisha kuwa lengo la kiwanda ni kuhakikisha kinakuwa na uwezo wa kukamua tani 100,000 moja kwa saa ifikapo mwaka 2013, hali ambayo itaongeza ufanisi kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyo sasa.
Awali akitoa taarifa fupi kwa wajumbe hao wa bodi ya NSSF kabla ya kutembelea mitambo na mashamba ya kiwanda, Rana alibainisha kuwa lengo la kiwanda ni kufanya uzalishaji kwa kutumia teknolojia ya kisasa itakayoongeza uzalishaji kwa kiasi kikubwa.
Alisema jumla ya hekari 1,500 za mashamba mapya ya kiwanda yanaendelea kuandaliwa katika hatua mbalimbali tena kwa teknolojia ya kisasa na tayari kiwanda kimepanda hekari 1150 za zao la miwa kama mali ghafi ya kiwanda.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NSSF, Abubakar Rajab akitoa shukrani kwa niaaba ya bodi ya shirika baada ya ziara hiyo, alisema bodi imeridhika na kazi nzuri inayofanywa na menejimenti ya kiwanda ikiwa ni pamoja na uzalishaji wa kisasa.
“Tumetembelea tumeona kazi nzuri inayofanyika hapa, kuna haja ya wakulima na wawekezaji wengine kuja kujifunza hapa kilimo cha umwagiliaji, ni mradi mkubwa na mnaendesha kisasa…hiki ndio Kilimo Kwanza kweli kweli,” alisema. NSSF imekifadhili kimkopo kiwanda cha Sukari Kagera kiasi cha sh. bilioni 12.
Mwisho.

Sunday, March 13, 2011

Serikali kuungana na Mwasapile kutoa dawa ya maajabu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, William Lukuvi.


Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, amesema Serikali imeunda Kamati itakayokwenda Loliondo kumsaidia Mchungaji Ambilike Mwasapila kuendelea kutoa huduma kwa wananchi wanaofika nyumbani kwake kwa ajili ya huduma.

Hata hivyo kiongozi huyo alifafanua kuwa Serikali haijazuia tiba hiyo kutoka kwa Mchungaji huyo, na wala haina mpango wa kuzuia ila kutokana na uwingi wa watu na magari yaliyokwama katika Kijiji hicho kuna kila sababu ya kuingila ili kuweza kunusuru maisha ya wananchi hao kabla ya kutokea maafa eneo hilo.

Aidha alisema Serikali kupitia Kamati yake iliyoundwa kwa kushirikiana na Serikali ya Kijiji hicho pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, wamejipanga kuanza kuzuia magari yote yanayoingia kijiji hicho ili kupunguza msongamano uliopo na badala yake waruhusu magari kutoka tu hadi hapo yatakapopungua na kuhakikisha huduma hiyo inayotolewa kwa utaratibu kuepuka msongamano.

Lukuvi, aliwashauri Wananchi waliokwishafanikiwa kupata huduma hiyo kwenda katika vituo vya afya na kupima afya zao baada ya siku 14 tangu walipokunywa dawa ili kuweza kuona kama kunamabadiliko ama la, wakati Serikali kupitia Kamati yake ikiendelea na kuifanyia kazi dawa hiyo kuweza kubaini ubora wake na Dozi yake kwa ujumla, ili iweze kuwa katika kiwango.

Mbali na Kamati hiyo Serikali imejipanga kupeleka magari ya kubebea wagonjwa eneo hilo ili kuweza kutoa huduma ya kuwawaisha waliozidiwa katika mahospitali, pamoja na kuandaa huduma za afya kama vyoo na mahema ya kupumzikia wananchi wanaokuwa wakisubiri kupata huduma. 

Hali ilivyo kijijini kwa babu Loliondo


Dawa aina ya mugaruga ikichemshwa





Dawa ya babu wa Loliondo ikiwa imehifadhiwa kwenye ndoo na mabeseni tayari kunywewa.


Babu Mwasapile akigawa dozi kwa wagonjwa wake.



Wagonjwa wakiendelea kupata kikombe cha dozi ya dawa ya ajabu.



Ukisha pata kikombe cha dawa unapumzika. Baadhi ya wagonjwa wakiwa wamepumzika baada ya dozi.



Umati ni mkubwa ile mbaya. Baadhi ya wagonjwa na ndugu na marafiki walioleta wagonjwa wanasubiri kikombe cha babu.



Babu sasa ni maarufu zaidi ya unavyofikiri. Baadhi ya wanahabari wakifanya mazungumzo na Mchungaji Mwasapile.

Picha zote na mdau wa Harusi na Matukio, LOLIONDO.







Wednesday, March 9, 2011

Dawa ya maajabu yazidi kuvuta wengi Loliondo

                                                      
Ndoo na mabeseni ya dawa aina ya mugariga ikiwa imechemshwa tayari kwa kunyweshwa wagonjwa.

*Yadaiwa kutibu Ukimwi, Kansa, Kisukari

Na Mwandishi Wetu,
Loliondo


MCHUNGAJI mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Ambilike Mwasapile amesema licha ya umati wa watu kuendelea kufurika nyumbani kwake ataendelea kutoa dawa hiyo kwa wagonjwa kadri wanavyokuja.

Hadi jana takribani watu zaidi ya 3,000 walikuwa wakiendelea kufurika nyumbani kwa mzee huyo anayedaiwa kuwa na dawa aliyooteshwa na Mungu ambayo inatibu magonjwa matano sugu kwa pamoja, yaani Kisukari, Ukimwi, Presha, Kansa na Pumu kwa lengo la kupata huduma ya dawa hiyo.

Ambilike Mwasapile amesema bado ataendelea kuwahudumia watu watakaofika nyumbani kwake. Pamoja na hayo amewaonya baadhi ya watu wenye magari ya usafiri ambao wamekuwa wakipandisha bei ya nauli kutokana na idadi kubwa ya watu kutaka kwenda kijijini kwake.

Akizungumza nyumbani kwake na vyombo vya habari juzi Mchungaji Mwasapile, amesema, hivi sasa zaidi ya watu 3,000 wanakwenda nyumbani kwake katika Kijiji cha Samunge wilayani Ngorongoro kwa ajili ya kunywa dawa kwa gharama ya Sh. 500 kama alivyoagizwa na Mungu katika ndoto.

“Watu ni wengi wanakimbilia uponyaji na hawa bado ni tone katika wale wanaondelea kuja hapa, nisingependa kuona wafanyabiashara wakianza kuwaumiza watu wanaokuja kunywa dawa.

“Hii ni agizo kutoka kwa Mungu kwamba dawa hii itolewe kwa kiwango cha sh. 500 kwa hiyo hata wao wanapaswa kuwatoza gharama za kawaida kabisa za nauli watu wanaokuja huku,” alisema Mchungaji Mwasapila ambaye hivi sasa amejizoelea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.

Onyo la Mchungaji Mwasapile limekuja muda mfupi baada ya umati wa watu kukimbilia katika Kijiji cha Samunge ambacho kipo umbali wa takribani kilomita 400 kutoka Arusha mjini, ili kufika huko ni lazima abiria watumie usafiri wa magari aina ya Toyota Land Cruiser na mabasi.

Nauli za magari kuelekea kijijini Samunge zimepanda ghafla na kufikia kiasi cha sh. 100,000 hadi 130,000 kwa mtu mmoja kwa safari ya kwenda na kurudi wakati nauli ya awali ilikuwa ni Sh. 37,500. Na kwa upande wa magari aina ya Land Cruiser imepaa hadi kufikia sh. 150,000 na 200,000 kwa mtu mmoja kutoka sh. 35,000 ya awali.

Kwa upande wa bei za vyakula kijijini hapo imezidi kupaa na kufikia sh.1,000 kwa sahani hadi sh. 3,000 kwa sahani, wakati nyama ya mbuzi ya kuchoma ikipanda kutoka sh. 4,000 kwa mguu hadi sh 20,000. Maji ya kunywa yanauzwa kwa sh.1,000 hadi sh. 1,500 kutoka sh 500.

Wakizungumzia ongezeko hilo pamoja na Mchungaji Mwasapile akitoa onyo kali kwa watoa huduma hiyo kushusha bei haraka, baadhi ya watu waliokwenda kunywa dawa wanasema
wafanyabiashara wamegeuzia gharama za dawa hiyo kwenye mahitaji ya kibinadamu.

“Unajua binadamu tuna matatizo sana mchungaji amepewa huduma hii na Mungu bure na yeye ameamua kutoa bure, lakini imefika kwetu waananchi wanaona hapa ndoyo mahali pa kutajirikia jambo hili si sahihi kabisa.

“Hii yote inatoa taswira kwamba kama ingekuwa si Mungu ndani ya mchungaji na zawadi, akapewa mtu mwingine au ikawa ni geresha kwa watu hakika wangekuwa wanaitoa dawa hii kwa gharama kubwa haijawahi kuonekana,” alisema mgonjwa mmoja.

Hata hivyo baadhi ya watu wengine wameiomba Serikali kuingilia kati kwa kusimamia bei za bidhaa na nauli katika eneo hilo kwani zitazidi kuwaumiza zaidi, ilhali wao wamekwenda kwa ajili ya kupata huduma ya dawa.


Saturday, March 5, 2011

Harusi ya Francis Lyimo na mkewe Rahabu Palangyo


Pichani wakiwa na nyuso za kutabasamu ni maharusi Francis Lyimo na mkewe Rahabu Palangyo wakiwa kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Istana & Catering ilipofanyika hafla yao baada ya kufunga ndoa Februari 19, 2011 katika Kanisa la Martin De Porres Mwananyamala Dar es Salaam. Bwana harusi ni Mfanyakazi wa East African Televition na Bi. harusi ni Hakimu. (PICHA NA
MDAU WA HM)

Send Off ya Doreen Kessy


Bi. Doreen Kessy (kushoto), akiwa na mpambe wake Roda Kalinga, wakiwapungia mikono wageni waalikwa katika sherehe yake ya kuagwa (Send Off) iliyofanyika Februari 19, 2011 katika Ukumbi wa Hoteli ya Istana & Catering uliopo Mwananyamala Dar es Salaam, Doreen alifunga ndoa Machi 5, 2011 Marangu Kilimanjaro. (PICHA NA MDAU WA HM)


Washiriki wa Miss Utalii wakiangalia baadhi ya vivutio vya utalii


Washiriki Miss Utalii Tanzania 2011, wakishangaa nyani anayetembea kwa miguu miwili, Manyara Mto wa Mbu wakati wa ziara yao hivi karibunikutembelea baadhi ya vivutio vya utalii nchini. Picha kwa hisani ya Miss Utalii Tz 2011.

Friday, March 4, 2011

Angalia, haya ndio maisha bora kwa kila Mtanzania?

Akina mama wenye umri wa makamo maeneo ya Ukonga Dar es Salaam wakisukuma baiskeli ya mkokoteni wakisafirisha bidhaa zao, kazi hii mara nyingi hufanywa na vijana wa kiume wasio na ajira ya uhakika. Picha na mdau Dotto Mwaibale. 

Rais Kikwete ateua makatibu wakuu

Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya  Kikwete amefanya uteuzi wa Makatibu Wakuu watano wapya na kuwahamisha wengine wanne kutoka wizara moja  kwenda nyingine. Uteuzi na uhamisho huo unaanza mara moja.
Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo inasema mabadiliko hayo yanatokana na Muundo mpya wa Serikali ambapo Wizara ya Miundombinu imegawanywa katika wizara mbil na baadhi ya Makatibu Wakuu kustaafu kazi kwa mujibu wa Sheria.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Kikwete amemteua Fanuel  Mbonde kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Ikulu. Kabla ya uteuzi wake, Mbonde alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu.
Wengine walioteuliwa ni Hussein A. Kattanga kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;John Haule kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
 Herbert  Mrango ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi; na  Eric K. Shitindi kuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira.
Kabla ya uteuzi wake, Kattanga alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto; Haule alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha;
 Mrango alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Shittindi alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Kuhusu uhamisho, Rais Kikwete amemhamisha Sazi B. Salula kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenda kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais;
Maimuna K. Tarishi ametoka Ofisi ya Waziri Mkuu kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii; Injinia Omar Chambo amekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Uchukuzi akitokea Katibu Mkuu wa Wizara ya zamani ya Miundombinu;
 Bibi Kijakazi R. Mtengwa amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ladislaus C. Komba aliyekuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii anapangiwa kazi maalum katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 Taarifa hiyo imesema Rais Kikwete amemhamishia Elizabeth Nyambibo Wizara ya Fedha na Uchumi ambako anachukua nafasi ya Naibu Katibu Mkuu iliyoachwa wazi na John H. Haule.
 Kabla ya uhamisho wake, Nyambibo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Taarifa ya Luhanjo imesema Makatibu Wakuu wapya wataapishwa saa tatu asubuhi leo Ikulu.


Katibu Mkuu, Philemon Luhanjo, wa pili kushoto akisalimiana na makatibu wakuu wapya kabla ya hafla ya kuaapishwa Ikulu. Picha kwa hisani ya Ikulu.



Makatibu wakuu wapya wakiwa wameketi kabla ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete. Picha na Ikulu.

Tuesday, March 1, 2011

Waziri Mkuu Pinda awatembelea Gongo la Mboto


Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda akizungumza na wakazi wa Gongo la Mboto (hawapo pichani) wakati wa ziara ya kuwatembelea waathirika wa milipuko ya mabomu iliyotokea katika kambi ya JWTZ Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambapo ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika na ugawaji wa misaada kuhakikisha kuwa misaada inawafikia walengwa. Picha kwa hisani ya Ikulu.

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...