Monday, February 12, 2018

Waziri Mwakyembe akutana na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo SMZ kujadili ugeni wa viongozi wa FIFA na CAF

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Yusuph Singo (kulia) akizungumza wakati wa kikao cha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) na Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma (wapili kulia) kujadili maandalizi ya ujio wa viongozi wa FIFA na CAF wanaotarajia kuja nchini tarehe 21 mwezi Februari mwaka huu leo Jijini Dar es Salaam.

Na Genofeva Matemu –WHUSM

WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe ameitaka Tanzania kuitendea haki heshima ya kupewa nafasi ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa FIFA na CAF hapa nchini unaotarajiwa kufanyiaka kwa siku mbili mwishoni mwa mwezi Februari.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia  ujio wa viongozi wa FIFA na CAF nchini kwa ajili ya kufanya mkutano hapa nchini ambao wanatarajia kuwasili nchini na kufanya mkutana wao  tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari mwaka huu.

Mhe. Mwakyembe amesema kuwa Seriakali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wameona ni vyema kukutana kujadili namna ya kupokea ugeni huo  mkubwa kwani Tanzania ina sifa ya kupokea wageni kwa ukarimu wa hali ya juu hivyo kuhakikisha  kuwa watakachokifanya wakifanye kwa hadhi na hali ya juu ya taifa letu bila ya migogoro ya aina yoyote.

“Ugeni unaokuja kwa kweli ni mkubwa hivyo fursa hii tuliyoipata tuitumie vizuri ili ugeni huo uamue tena kwa mara nyingine kuja hapa nchini kufanya vikao vyake na kuitangaza Tanzania duniani kote” amesema Mhe. Mwakyembe.

Naye Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Rashid Ali Juma amesema kuwa hii ni fursa ya aina yake kwetu sisi kwani itatupa nafasi ya kutangaza vivutio vya utalii tulivyonavyo na kuona ni namna gani michezo inaweza ikasaidia katika kukuza na kuongeza uchumi kupitia utalii.

“Tunaamini kuwa wageni hao watakua mabalozi wazuri kwa kutuletea watalii kupitia michezo na kuitangaza nchi katika mataifa mbalimbali”  amesema Mhe. Juma.


Ujio wa viongozi wa FIFA na CAF ni bahati kubwa kwa nchi yetu na unatokana na matokeo chanya ya utendaji kazi mzuri unaofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Serikali lakini pia upigaji vita wa masuala ya rushwa na upangaji wa matokeo wakati wa mechi.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...