Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam. |
Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma. |
Na Mwandishi Wetu
BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huza
huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na
msaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi ya
Mtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogeza
huduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.
"...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa na
kesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona
kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"
alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya
akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa na
muitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwa
vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.
Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili za
matuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikia
muafaka juu ya mvutano wao.
Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa
huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapo
huduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ na
ushauri wa kisheria utatolewa.
"...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji huduma
hizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa
kuja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwa
pia," alisema Bi. Chonya.
No comments:
Post a Comment