Karibu kwenye blogu yetu yenye habari, picha na matukio mbalimbali yakiwemo ya harusi na mitindo. Kwa kuwa ni blogu ya jamii tunakaribisha maoni kutoka kwako. Tutumie habari na picha za harusi, mitindo na maelezo yake au maoni kupitia; mushijoa@gmail.com / hilder_mwaipopo@yahoo.com au Simu;- 0717030066/ 0756469470.
Monday, February 12, 2018
UNESCO KUADHIMISHA SIKU YA RADIO DUNIANI DODOMA
Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani. Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari.
Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo, usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo.
Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni, Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani.
Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio.
Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki.
Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya. Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi.
Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika. Si tu redio inatumika kubadilishana Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika.
Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii.
Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO.
Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo.
Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii, kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na kuboresha uwezo wao katika kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.
Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...
-
Baadhi ya wanamuziki wa kundi la taarab la 5 Star wakiwa pichani. Na Mwandishi Wetu TAARIFA zilizotufikia muda mfupi uliopita zinasema ...
-
Mke wa Ridhiwani Kikwete (aliyembeba mtoto) akipiga picha na mkwewe Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) katika hafla ya kumpongeza baada y...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dk. Ally Simba (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Kampuni ya Agano Safi, Iyaloo ...
No comments:
Post a Comment