Tuesday, February 27, 2018

WAHUDUMIENI WANANCHI BILA YA UBAGUZI - MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya kikundi cha Teleza wakati alipo wasili, Wilayani Newala, akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu, Mkoani Mtwara  Februari 27, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma wawatumikie wananchi kwa uweledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 26, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa wilaya za Masasi na Nanyumbu kwa nyakati tofauti.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi aliwasisitiza watumishi wa umma kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Alisema Rais Dkt. John Magufuli amesisitiza watumishi wa umma wawatumikie wananchi bila ya ubaguzi wowote pamoja na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“Watumishi wa umma lazima mtambue kwamba msimamo wa Serikali ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kiitikadi na kipato.”

Waziri Mkuu alisema ni vyema watumishi hao kuanza kujitathmini kwa sababu Serikali haitowavumilia watumishi watakaoshindwa kuwajibika kwa wananchi.

Pia aliwataka watendaji hao kuacha urasimu na wahakikishe kila fedha iliyotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inatumika kama zilivyoelekezwa.

Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji hao wawe na mpango wa kuwatembelea wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi. 

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...