Monday, November 13, 2017

Tatu Mzuka, Naibu Waziri wachangia ujenzi wa shule za msingi

NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde  mwishoni mwa wiki amekabidhi matofali 3000 na mifuko ya saruji 100 katika Kata ya Makutupora kwa ajili ya kuanza awamu ya kwanza ya ujenzi wa Shule za Msingi Mpya za Mbande na Muungano Wilaya ya Dodoma mjini mkoani Dodoma.

Msaada huo alioukabidhi umetoka kwa kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka  ambayo ilikabidhi zawadi kwa washindi katika droo ya michezo hiyo,Mavunde aliishukuru kampuni hiyo kwa msaada huo na kuwaomba wadau wengine kujitokeza zaidi ili kusaidia kuboresha Elimu nchini.
 
Waziri Mavunde alisema kuwa ujenzi wa shule hizo utasaidia kupunguza adha inayowapata wanafunzi kutembea umbali mrefu  wa zaidi ya kilomita 7 kufuata shule katika eneo la Veyula.



 "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakikabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa mmoja wa viongozi katika kata ya Makutupora  kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Kwa ajili  ya ujenzi wa madarasa mawili  kila moja.


  "TATU MZUKA kwa ushirikiano na  Naibu Waziri, Kazi, Ajira na Vijana Mh.  Anthony Mavunde  (Mbunge Dodoma Mjini) wakiwashukuru baadhi ya wakazi na viongozi mbalimbali wa kata ya Makutopora mara baada ya kukabidhi  matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi  wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.


Baadhi ya Wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoka kijiji cha Makutopora na Mbande kushuhudia tukio la makabidhiano ya matofali 3000 na mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule za msingi Mpya za Muungano na Mbande,iliyotolewa na kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Tatumzuka ikishirikiana na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana Antony Mavunde.


No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...