Sunday, November 26, 2017

Naibu Waziri Mavunde agawa mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amegawa mashine 31 za aina mbalimbali kutoka kampuni ya HiTECH International kwa vikundi 31 katika jimbo lake la Dodoma Mjini. Mashine alizozitoa Naibu Waziri ni pamoja na mashine za kutotolea vifaranga (incubators- mayai 1056 na mayai 528) mashine za matofali (umeme na manual), mashine za Popcorn zenye matairi, vyerehani, mashine za kutengeneza chaki (chaki 50,000-80,000 kwa siku), mashine za kunyonyolea kuku mpaka kuku 500 kwa siku. Mavunde ametoa mashine hizo zenye thamani ya milioni 55.8 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi yake katika uchaguzi wa mwaka 2015 kuwezesha wananchi ili wajikomboe kiuchumi lakini pia kuunga mkono mpango wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde akikabidhi mashine kwa vikundi mbalimbali vya Dodoma Mjini. Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya HiTECH International, Paul Mashauri akizungumza jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde wakati wa hafla ya kukabidhi mashine 31 kwa wananchi wa Dodoma Mjini.

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...