Sunday, November 19, 2017

Clouds TV yaibuka na tuzo ya 'Kituo Bora cha Televisheni 2017'

Umoja wa Mataifa kupitia Umoja wa Vijana (YUNA) umetoa tuzo kwa Taasisi na watu binafsi wenye mchango mkubwa katika maisha ya watu barani Afrika.
Kupitia tuzo hizo zinazotambulika kama PAHA, kituo cha Televisheni cha Clouds kimetambuliwa kama kituo bora cha Runinga kwa mwaka 2017.
Hiyo ni kutokana na kurusha maudhui yanayomulika maisha ya watu na kutoa tumaini kwao kupitia vipindi na kampeni mbalimbali kama vile...
(#IshiNaMimi #Kipepeo #MalkiaWaNguvu #RudishaTabasamuMiaMoyo na nyinginezo)
Baada ya kupokea tuzo hiyo ya heshima Kampuni ya Clouds Media Group imeishukuru YUNA pamoja na umoja na umoja wa mataifa kutokana na Utambuzi huo.
Sambamba na hilo Clouds Tv imewashukuru Watanzania Kwa kuendelea Kuwaamini na Kuwachagua.
" Tunaahidi kuendelea kuwatumikia kwa moyo na nguvu zaidi kwani tulishakula kiapo cha kuwa Taasisi ya watu" sehemu ya taarifa hiyo ilieleza.
(#RedioYaWatu #ThePeoplesStation)
#TunakufunguliaDuniaKuwaUnachotaka

No comments:

Post a Comment

SEIF SHARIFF HAMAD AKIRI KUWA YEYE NI BABU KIZEE.

Seif Shariff Hamad Seif Shariff Hamad KWA mara ya kwanza Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Seif Shariff Hamad amek...