Na Emanuel Madafa, Mbeya
SERIKALI imewataka wafanyabiashara wa mbolea nchini
kuhakikisha wanafuata bei elekezi ya uuzaji wa mbolea iliyowekwa na serikali ili
kumsaidia mfanyabiashara mdogo aweze kuuza kwa rejareja.
Kauli hiyo imetolewa jijini Mbeya na Naibu waziri wa
Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa wakati
akifungua mkutano wamakatibu Tawala na
washauri wa kilimo wa Mikoa ya Nyanda za juu Kusini .
Amesema kuwa endapo itagundulika kwamba kuna
mfanyabiashara wa jumla anamuuzia mfanyabiashara wa rejareja kwa bei
itakayomfanya ashindwe kuuza kwa bei elekezi wizara itamchukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni
pamoja na kumfungia biashara yake
Mwanjelwa amesema ofisi yake inaushahidi kwamba wapo
baadhi ya wafanyabiashara wa jumla wamekuwa wakiwauzia mawakala wanaouza kwa bei elekezi ya serikali hivyo kuleta mkanganyiko na kuwafanya wauze mbolea
hiyo kwa bei zaidi ya elekezi .
Amesema katika Mikoa ya Ruvuma,Lindi ,Mtwara ,Mwanza na
Geita wapo wafanyabiashara ambao sio waaminifu wamekuwa wakifungua mifuko na kuuza mbolea ya kupandia (DAP) kwa Shilingi 2,000 kwa kilo kwa lengo
la kujipatia kiasi cha shilingi laki
moja (100,000) kwa mfuko wa kilo 50
badala ya bei elekezi ya shilingi
elfu hamisini na moja.
Aidha Naibu Waziri huyo amesema pamoja na kuwauzia
wakulima mbolea iliyopoteza ubora wake kwa kufunguliwa kwa kuachwa wazi
wafanyabiashara hao wanawaingizia hasara kubwa wakulima hasa katika kipindi cha mavuno.
Kutokana hali hiyo Naibu waziri huyo ametoa wito kwa
wafanyabiashara kote nchini kuacha tabia
hiyo mara moja ili kumpa fursa Wakala
aweze kuuza kwa bei ya rejareja na kwa bei elekezi bila kuathiri biashara zao .
Mkutano huo unalenga
kuongeza uelewa wa pamoja kuhusu
mifumo mipya iliyoanzishwa ya
uagizwaji wa mbolea kwa pamoja (Bulk Procurement system-BPS )na usimamizi wa
mbolea kwa lengo la kumuwezesha mkulima kupata mbolea bora kwa bei nafuu sanjali na kuongeza usalishaji wenye
tija.
Mwisho.
Mshiriki akichangia katika Mkutano huo........ |
Mgeni Rasmi Naibu Waziri wa Kilimo Dkt Mary Mwanjelwa katika Piha ya Pamoja na washiriki wa semina hiyo. |
No comments:
Post a Comment